Uchunguzi wangu wa awali kuhusu mgodi wa siri uliopo ndani ya pori la hifadhi Singida-Tabora

Uchunguzi wangu wa awali kuhusu mgodi wa siri uliopo ndani ya pori la hifadhi Singida-Tabora

Kuna picha za air strip na nyumba.
Lakini hakuna picha cha mgodi.
Kama ni active mining tuliegemea mleta habari aweke picha zinazoonyesha shughuli za uchimbaji kama mitambo ya uchimbaji na watu.

Airstrip kwenye game reserve sio Jambo la ajabu Sana, maana hizo ni starehe za matajiri wasiopenda bughudha.
 
Watanzania wenzangu mtakumbuka kwamba 4 March 2024 niliripoti kuhusu uwepo wa mgodi wa siri huko Singida - Tabora baada ya kupewa taarifa na mmoja wa wachimbaji wadogo.

Timu yangu ilifanikiwa kufika eneo hilo kwa lengo la kujiridhisha. Baada ya kufika eneo la tukio ikawa ngumu timu yetu kuingia kwenye huo mgodi baada ya kugundua kwamba mgodi huo uko ndani ya pori la Kizigo Game Reserve lililoko mkoani Singida na hakuna njia wala barabara inayoweza kukupeleka ndani ya mgodi huo. Na pori hilo hilo linalindwa na askari wanaohusika kulinda mapori na hifadhi za taifa.

Kutokana na mazingira hayo timu yetu ililazimika kutumia technology ambayo ilisaidia kujua mambo yafuatayo.

1. Ni kweli mgodi huo uko ndani ya hifadhi au pori la Kizigo Game Reserve lililopo Singida na linaingia mpaka Tabora.

2. Ni kweli kwamba karibu na mgodi huo kuna uwanja wa ndege (airstrip) kilomita 1.3 kama ambavyo technology imetuonyesha pamoja na picha za uwanja huo.

3. Kwa muda ambao timu yetu iliweka kambi ya wiki moja ndege ilitua na kuondoa mara 2. Kwa hiyo kwa wiki ndege hutua na kuondoka mara mbili kwa ajili ya kushusha na kubeba mizigo.

4. Tumejiridhisha kwamba Kizigo Game Reserve pia inapakana na hifadhi zingine mbili Muhesi Game Reserve na Rungwa Game Reserve.

5. Kuna njia zinatoka kwenye huu uwanja wa ndege kwenda kwenye hayo hizo hifadhi za jirani nilizozitaja hapo juu. Hii inaashiria kuwa kuna biashara nyingine haramu ya kusafirisha wanyama Wildlife trafficking katika eneo hilo. Ndio maana kuna njia za kuingia kwenye mapori mengine ya hifadhi katika eneo hilo.

6. Kuna nyumba zimejengwa umbali wa mita 800 kutoka katika uwanja huo wa ndege.

7. Hakuna barabara yoyote inayoingia katika mgodi huo isipokuwa huo uwanja wa ndege ambao sijui kama unatambulika rasmi.

Katika mazingira tuna mashaka kwamba serikali au viongozi wa serikali binafsi wanaweza kuwa wanahusika na biashara haramu zinazoendelea katika eneo hilo. Kwa sababu hizo Game Reserve zina askari wanaozilinda muda wote hivyo ni ngumu serikali kutokujua uwepo wa mgodi huo.

Bado timu yangu inaendelea na uchunguzi ili kupata picha clear lakini na wamiliki wa biashara haramu ndani ya msitu huo pamoja na washirika wake. Tutajua tu kama biashara hiyo wameuziwa wazungu au waarabu na wahusika wenye mamlaka ya kuuza au kukodisha eneo ndani ya nchi.

Mdude Nyagali 7 x 70 Sumu ya Nyigu.
View attachment 2946548View attachment 2946549
aisee iko kazi. Sasa ndio ujue hatutaelewa tena wala mapigo yanatokea wapi maana fisadi ndio wameshika nchi.
 
Quote: Hayo mambo ni kuangalia na kuacha kwa salama wa uhai wako.
Hii ndo Shida kubwa ya waTz wengi - UOGA. Mtu anaogopa kusema ukweli na kile anachokijua eti anahatarisha maisha yake. Tunasahau hakuna atakayeishi milele hapa duniani.
Ni kweli wanaweza "wakamshughulikia" lakini kwamba sasa habari iliyowekwa eti ni siri itakuwa sasa imeanikwa hadharani. Watapatikana au watajitokeza wengine kuishikilia bango mpaka kieleweke kinachoendelea hapo porini.
We need more Mdude in this country otherwise hawa viumbe wa ajabu wa kijani watatufanya nchi yetu nzuri iwe kama congo
 
We need more Mdude in this country otherwise hawa viumbe wa ajabu wa kijani watatufanya nchi yetu nzuri iwe kama congo
Not only like Congo, but in the near future it may become more than Palestina.
Kwa bahati mbaya sana wao kama wao hawatakuwepo kwani muda wa uhai wao utakuwa umeisha watakuwa RIP wote. "Ole" watawaachia vizazi vijavyo ambao maskini ya rabi, hata hawajui kilichojiri.
 
Sioni shida ya mgodi kuwa na ndege
Sio lazima kuwepo barabara
Kujenga barabara yaweza kuwa gjatama kubwa kulliko faida ya mgodi wenyewe
Umedandia mada. Hujui imeanzia wapi na sidhani pia unaelewa inakoelekea
 
Back
Top Bottom