UCL FAINAL 2018: Liverpool baada ya kuwatoa AS Roma sasa kukwaana na Real Madrid katika mchezo wa fainali

We jamaa Liverpool kuingia Final inaonekana imekuuma sana Kama vipi si uandamana kabisa
Hainiumi, ila napenda mfungwe sababu mnaongea sana, sio nyie tu bali hata waingereza na wana habari wao, hamuwapi timu zingine heshima zinazostahili, hivyo nataka timu ziwadhihirishie kuwa wako vizuri zaidi yenu. Na sasa mmefika tamati, Real anawaua!!
Pia mmekuwa na wivu ulioputiliza Real kuingia fainali raundi ya tatu mfululizo na kwenda kuchukua ndoo raundi ya tatu mfululizo. Hii imewapa chuki moja mbaya sana.
 
May 26th, 2018 I hope utakuwa mchapo wa nguvu wenye ushindani mwanzo mwisho kwa dakika zote 90, kama itabidi extra time na maguu 12 ya mtu mzima mwenye akili timamu.
Hiyo match lazima tuiangalizie magheton kwenye projector huku cocktail na popcorn zikishushwa.
 
Huna point hata moja Zaidi ya ushabiki uchwara na wivu tu uliokujaa Acha kufata mkumbo
 
Mkuu usisahau mpira hudunda. Mwezi July 2017 wapenzi na mashabiki wengi wa soka duniani ungewaambia Liverpool watacheza na Madrid kwenye UEFA Finals asilimia kubwa wangekataa.

Kwenye paper Liverpool hawawezi kushinda kwenye mechi hiyo lakini wanaweza kuja na ari kubwa sana na kosa moja tu la Madrid likawapa bwawa la maini ubingwa. Tusubiri May 26 tuone Mkuu.

Dj BAKI hamna hiyo kitu. Sioni nafasi ya liver.

Kwa madrid hii iliyokuwa sirias na UEFA.

Fainali rahisi saana
 
Et final nyepes? Uyo Madrid mbona nae ni ovyo tu kwenye defense
Uliangalia mechi ya marudiano kati ya bayern munich na real madrid??? Pale ni pengo la carvagal tuu but defense ilikua vema saana kiasi cha kuwatoa mchezoni wakina lewondosk na muller
 
Huo mpira wa Madrid ninaouona mkimsifia kwa kufata ukubwa wa majina ya wachezaji mnajifariji bure!
Hii ndoo ni ya Liverpool bila ubishi
Hamna beki. Bek gani inaweza kufungwa magoli sita, magoli manne ya hovyo katika mechi ya round ya pili
 
Naiona fainali ya mteremko kwa Real, liver ina mapungufu makubwa sana kwenye defense.!
Mapungufu ambayo kina Leroy Sane, Sterling, Aguero, De Bruyne na Pep wao walishindwa kuyaona? Madrid nao hawapo gado kama last season na defence yao ina nyufa za kutosha sana tu. Hata kuchomoka mbele ya Bayern ilikuwa bahati na Zidane amekiri hilo.

Liverpool wanakwenda kubeba ile ndoo bila taabu kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…