Udhaifu wa Ripoti ya CAG 2021/2022

Udhaifu wa Ripoti ya CAG 2021/2022

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Ripoti ya CAG inaongelea ufisadi na wizi wa mali za umma pamoja na hasara za mashirika kama ATCL au TTCL kwa ujumla wake. Inaonyesha ufisadi umefanyika katika shirika au ofisi fulani tu bila kuonyesha au kupendekeza mtu halisi anayepaswa kuwajibika au kuwajibishwa katika dai husika.

Ripoti zijazo za CAG zikionyesha ufisadi au wizi zitaje kabisa na mtu au watu halisi wanaopaswa kuwajibika. Iseme wazi kama ni mkurugenzi, katibu mkuu, waziri, afisa masuhuli, mwenyekiti wa bodi n.k wanaohusika katika wizi husika.

Isiache uwajibikaji hewani tu bila kuonyesha mhusika wa kubebeshwa kesi husika na kuchukuliwa hatua.
 
Ripoti ina makosa mengi Sana. Mfano huwezi sema Taasisi inadai bilioni kadhaa lakini mdaiwa hajulikani .. seriously? Ukaguzi gani usijue source ya deni?

Halafu CAG lazima ajifunze kusema waziwazi bilioni zilizoibiwa ni zipi na hasara ni ipi...kuna hasara ambayo Haina wizi na kuna wizi hata kama Taasisi haina hasara, lazima CAG asaidie serikali kuona wapi kuna "criminal activity" na wapi kuna "uzembe"
 
Serikali pendwa ya CCM imejaza mijizi! CCM ni wezi, wanafiki, waongo, walafi. CCM wanahitaji toba
 
Hata kama imejaa majizi bila kuonyesha mwizi au wezi husika zinakuwa porojo tu za kuwatoa watu povu kwa muda kisha kupuuzwa na kutupwa kapuni.
kwahiyo unataka CAG aje akwambie Nape na Makamba ni wezi?
 
Hata kama imejaa majizi bila kuonyesha mwizi au wezi husika zinakuwa porojo tu za kuwatoa watu povu kwa muda kisha kupuuzwa na kutupwa kapuni.
Mtu unaweza tokwa povu kuwa Taasisi imepiga bilioni kadhaa kumbe ni matumizi Tu ya vimemo.

Ripoti haijasema hata ofisi ya Rais matumizi yake ..nna wasiwasi hata vimemo vyao huko ATCL na kwingineko ndo kumeongeza hasara iliyotajwa.

Kwanza ofisi ya CAG inakaguliwa na nani?
 
Mfano huwezi sema Taasisi inadai bilioni kadhaa lakini mdaiwa hajulikani .. seriously?
Ukaguzi gani usijue source ya deni?..
Ignorant mwingine huyu hapa. Kwani tafsiri ya fictitious receivables ni nini? Umewahi kusikia kuhusu manipulation of financial accounts by overstating assets?

Kama wanafoji madeni hewa kwa nini washindwe madai hewa? Kama ni hewa nani mwenye wajibu wa kuthibitisha kama ni halisi? Kama responsible party wameshindwa kuthibitisha ulitaka CAG asemeje zaidi ya kusema fictitious debtors. Acha porojo broo.
 
Ignorant mwingine huyu hapa. Kwani tafsiri ya fictitious receivables ni nini? Umewahi kusikia kuhusu manipulation of financial accounts by overstating assets?! Kama wanafoji madeni hewa kwa nini washindwe madai hewa? Kama ni hewa nani mwenye wajibu wa kuthibitisha kama ni halisi? Kama responsible party wameshindwa kuthibitisha ulitaka CAG asemeje zaidi ya kusema non-existing debtors. Acha porojo broo
et anakwambia CAG anakaguliwa na nani,
ni sawasawa na kujiuliza hivi mahakama inashitakiwa wapi

Tume iundiwe tume
 
Kama nchi, tunapigwa na was...i wachache.

Ina maana TRA ni safi sana? Au ndo......

Kichere naye akaguliwe
 
Hata kama imejaa majizi bila kuonyesha mwizi au wezi husika zinakuwa porojo tu za kuwatoa watu povu kwa muda kisha kupuuzwa na kutupwa kapuni.
Wawataje kwa majina? Report? Sidhani kama ni part of ToR yao! Hio nadhani inaenda kwa TAKUKURU na Polisi, Wale sidhani kama Wana investigate.

Sometimes wanachoonyesha ni ile Hali ya watumishi kutokufuata taratibu sahihi za manunuzi
 
Ukiwa CCM usipokua tajiri wewe ni mbwa! Hakuna Wala rushwa kama Hawa simblisi
 
CAG ametaja alipo kagua akakuta mambo yameenda mrama, kwahivyo sio kazi CAG kufanya upelelezi ili kubaini mtuhumiwa ni nani.

Kwahivyo alipo ishia yeye basi mamlaka inayo fuata itekeleze wajibu wake.
 
Back
Top Bottom