Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Ripoti ya CAG inaongelea ufisadi na wizi wa mali za umma pamoja na hasara za mashirika kama ATCL au TTCL kwa ujumla wake. Inaonyesha ufisadi umefanyika katika shirika au ofisi fulani tu bila kuonyesha au kupendekeza mtu halisi anayepaswa kuwajibika au kuwajibishwa katika dai husika.
Ripoti zijazo za CAG zikionyesha ufisadi au wizi zitaje kabisa na mtu au watu halisi wanaopaswa kuwajibika. Iseme wazi kama ni mkurugenzi, katibu mkuu, waziri, afisa masuhuli, mwenyekiti wa bodi n.k wanaohusika katika wizi husika.
Isiache uwajibikaji hewani tu bila kuonyesha mhusika wa kubebeshwa kesi husika na kuchukuliwa hatua.