Udhaifu wa Serikali hii tutakuja ona madhara yake baadaye. Leo ni ishara ndogo mojawapo

Udhaifu wa Serikali hii tutakuja ona madhara yake baadaye. Leo ni ishara ndogo mojawapo

Wenawe!

Sasa simba na yanga ni swala la kitaifa...!!? angalia ushabiki wa mpira utakuua bure
Je watu waliotapeliwa viingilio pale wangeamua pachimbike TFF wana vyombo vya ulinzi kuwazuia wale wahanga?

Watu wametoka Zambia, mikoani tokea asubuhi wapo kwa MKAPA, mama ana sababu za kukwepa lawama,bahati nzuri WATANZANIA ni wa kimya sana ila tuliowapa mamlaka wanatuchukulia poa kama vile kilichofanyika leo ni kizuri.
 
Serikali ina ahirisha match ya Simba na Yanga eti sababu Mwinyi anazindua kitabu. Huu ni wendawazimu.

Anayetaka kuhudhuria Uzinduzi wa Mwinyi si aende na anayetaka kwenda angalia mpira si aende?

Huu ndo udhaifu ambao tunaukataa miaka yote. Kuchanganya mambo binafsi ya Serikali na Wananchi. Suala la Mwinyi kuzindua kitabu si issue ya Kitaifa kwa nchi hii kama suala la Simba na Yanga.

Kwenye Simba na Yanga ndipo ambapo Chadema na CCM husahau tofauti zao na kurudi kwenye team zao. Ndo maana hata chadema,act wanavaa jersey za yanga pamoja na kuwa ni za Njano na Kijani.

Huu ni mwanzo wa kuonesha udhaifu ambao miaka yote tunaupigia kelele. Haya angekuwa ni Magufuli ameamua hili tungemwita ni dhaifu na dikteta. Lakini kwa Samia tusemeje? Tuendelee kusifu na kuabudu?
Tunapopelekwa sijui, ni mapema sana kumjaji huyu mama, serious wanaomsifia bado mapema sana, hao hao watarudi kumponda, hakuna wa kumfananisha na JPM bandidu.
 
Je watu waliotapeliwa viingilio pale wangeamua pachimbike TFF wana vyombo vya ulinzi kuwazuia wale wahanga?

Watu wametoka Zambia, mikoani tokea asubuhi wapo kwa MKAPA, mama ana sababu za kukwepa lawama,bahati nzuri WATANZANIA ni wa kimya sana ila tuliowapa mamlaka wanatuchukulia poa kama vile kilichofanyika leo ni kizuri.
Ushauri wangu mechi ijayo isiwe na kiingilio, waingie watakao wahi, uwanja ukijaa pafungwe.
 
Hahahaha... Misukule ya Jiwe bana.
Eti afanye kazi kama Mwendazake.

Zama zenu zimekwisha kupita, hii ni awamu nyingine.
Kama ndio hiyo ya kukaribisha waKenya kuwekeza Tz na kupewa ardhi kwa kuwa wana mitaji, mimi nasema ni mawazo ya upotolo.

Kwa kutambua udhaifu huo, Rais Uhuru ameagiza waTz wanaotaka kuwekeza huko, rukhsa bila vibali vyoyote, akijua kuwa hawana mitaji na uwezo wa kuwekeza Kenya, hata dukawala, kwani ardhi ni mali ya wenye nacho huko Kenya.
 
..hapo inabidi uilaumu ccm na serikali zake.

..kwanini hawakuwaandaa na kuwawezesha Watz kuchangamkia fursa za ndani na nje ya mipaka yetu?
 
Mama aliambiwa avunje bunge akawa haelewi somo na watamuharibia hadi Spika ampigishie kura ya kutokuwa na imani... ila kwa suala la Yanga Serikali haihisiki... ila sio ya kushindana nayo... jamaa wa Kigoma ndio namuonea huruma bora ajengewe sanamu lake maana hana tofauti na Dr. David Livingstone
 
ndio maana nasema unaongozwa na muhemko.

lini watu walijifungia ndani wakiogopa kutekwa??
lini watu waogopa kuweka fedha benk wakiogopa zitapotea??
vyombo vya dolar vinafuata sheria ipi??
Miaka 5 iliyopita ndiyo maisha tuliyoishi, wapi Ben Saanane na Azory Gwanda. Nani aliua wale watu kwenye viroba na kuwatupa baharini?
Nani alimteka Roma Mkatoliki na Mo Dewji? Nani alimshambulia Tundu Lissu?
Kwa nini wafanyabiashara walikimbia nchi? Nani kajaza watu rumande kwa kesi zusizo na ushahidi?
 
Kinachonisikitisha ni kwamba vyote, mechi ya simba na yanga na uzinduzi wa kitabu vyote hivyo haikuwa ni dharura. Sasa kama walkua wanajua tokea sikutano nyuma kwann hawakuchukua maamuzi ya kufuata sheria hata kama wangeamua mechi iwe jumapili na kitabu kiwe jumamosi. Lakini sio kusubiri mpk siku ya tukio tena bado masaa machache ndio mnaahirisha
 
Miaka 5 iliyopita ndiyo maisha tuliyoishi, wapi Ben Saanane na Azory Gwanda. Nani aliua wale watu kwenye viroba na kuwatupa baharini?
Nani alimteka Roma Mkatoliki na Mo Dewji? Nani alimshambulia Tundu Lissu?
Kwa nini wafanyabiashara walikimbia nchi? Nani kajaza watu rumande kwa kesi zusizo na ushahidi?
kama hamjajifunza siasa za kihuni sio dili mtaendelea kipotea.

mwanzo ni hiyo kauli ya juzi kwamba majambazi na vibaka msimjaribu,sasa subirini watendaji nini watawafanya.
 
Serikali haina issue kwenye hili Yanga waoga.
Waoga? Ungeleta timu saa 11 km mwanaume kweli nilikaa nusu saa nzima kukusubiri mtani mkachungulia na tff wenu mkaona mbadili muda fasta hizo njia sisi wenyewe watu wa mipango tunazijua karia simba kidau simba ndio maana simba wao wameona fresh tu sababu ina maslahi kwao na simba usnitch kawaida yenu hamjawahi kusimama pamoja nasi kwenye suala la maslahi miaka 7 iliyopita Manji aliwahi kugomea m100 za Azamtv simba mkaongea sana cha ajabu juzi kati hapa bosi wenu akatweet kuhusu suala lilelile tuliloligomea yanga miaka 7 iliyopita Yanga pia iliwahi kugomea hela ya kagame simba mkaingiza timu na kutangaza tumewaogopa cha ajabu baadae nanyi mkaja kuona kagame michosho msonye alikuwa pale kwa maslahi lakini sisi tunapopigania wenzetu huwa mnakaa pembeni masnitch kishenzi nyie
 
daaahhh Simba wameonesha unafiki... walipaswa kufika saa ile ile iliyopangwa
Usnitch hawajaanza leo 1939 timu za wazawa walitaka kuanzisha chombo cha kusimamia timu zao maana chombo kilichopo kiliongozwa na wageni watupu wakati wapo kwenye hzo harakati Sunderland(baadae Simba) wakawasnitch Yanga na kuungana na timu ya kiarabu(Arab sports) hii ilizima kabisa ndoto ya wazawa kuwa na ligi yao kitendo hiki kiliwaudhi sana Young Africans na kuwaona wenzao km wasaliti
 
Hoja za kitoto
 
kama hamjajifunza siasa za kihuni sio dili mtaendelea kipotea.

mwanzo ni hiyo kauli ya juzi kwamba majambazi na vibaka msimjaribu,sasa subirini watendaji nini watawafanya.
Hilo Ni dua la nyani tu. Wasukuma mumepigika na bado
 
Back
Top Bottom