Udhalilishaji kwa wanaume mbona haupigiwi kelele?

Udhalilishaji kwa wanaume mbona haupigiwi kelele?

Baada ya ile video ya binti wa Yombo akibakwa na wanaume 5 kusambaa mitandaoni, watu walipaza sauti na wanaendelea kupaza sauti kudai haki itendeke.

Lakini, kuna video nyingine inasambaa mitandaoni na ilikuwepo kabla hata ya ile ya yule binti kusambaa, ikimuonesha jamaa mmoja akidhalilishwa kwa madai ya kutembea na Mke wa mtu.

Inasikitisha sana, maana jamaa anaonekana uso umevimba, anavuja damu, yuko uchi wa mnyama na analazimishwa kucheza taarabu huku akikata mauno. Jamaa anaomba maji, lakini ananyimwa huku akitukanwa matusi ya nguoni.

Soma Pia:

Najiuliza swali, Je, ni sahihi Mwanaume kudhalilishwa lakini siyo sahihi mwanamke kudhalilishwa?

Kwanini tunakuwa na double standards ?

Kama tunataka haki, basi haki hiyo iwanufaishe wote pasipo kupendelea jinsia moja.
Upepo wa sasa ni KE usijichanganye kabisa utakachofanya ni kuondoka zako km yamekushinda or achana nae km ni mahusiano km ni makazini tafuta kijiwe kipya tu otherwise uwe chawa wake hapo utapewa cheo chochote kikubwa
 
Sio kosa? Nani amekwambia? Na wewe ni miongoni mwa wanasheria NGULI au WASOMI?

Kama na wewe ni Mwanachama wa TLS basi siwezi shangaa TLS kuwa ilivyo sasa na kabla ya sasa
Hakuna kosa linalo tambulika kisheria kuwa kufanya mapenzi na mke au mume wa mtu nikosa kisheria ikiwa tuu wamekubaliana kwa hiyari yao wenyewe wote kwa pamoja na ndio maana jambo hilo halina adhabu inayo tambulika kisheria , bali hayo mambo hubebwa kijamii zaidi
 
Hakuna kosa linalo tambulika kisheria kuwa kufanya mapenzi na mke au mume wa mtu nikosa kisheria na ndio maana jambo hilo halina adhabu inayo tambulika kisheria , bali hayo mambo hubebwa kijamii zaidi
Ndio maana kesi zake hugeuzwa ubakaji/unyanyassji kijinsia kwakua sheria ya kutembea na either haipo
 
Ndio maana kesi zake hugeuzwa ubakaji/unyanyassji kijinsia kwakua sheria ya kutembea na either haipo
Na zaidi ya hapo ikiwa wote wawili wakakiri kupendana basi hapo ndipo madai ya talaka huanza ,

Hata huyo binti wanae dai amebakwa na watu watano , kama ana umri zaidi ya miaka 18 anaweza kusema nilikubaliana nao kwa hiyari yangu ili nipate faragha nao na hakuna sheria inayo mkataza kufanya hivyo, na hapo kunakuwa hakuna kesi tena dhidi yao kwa jambo hilo, ila sasa litakuja shitaka la kimtandao la kurekodi na kusambaza video za utupu ambalo nalo litakuwa la aliye rekodi na kupost.
 
Mifumo ya Dunia imemtenga mwanaume, haya ndo matokeo ya 50/50. Miaka ijayo litakuja vuguvugu la kutetea haki za wanaume maana hali itakuwa mbaya zaidi na tutakuwa tumechelewa. Shetani kazini, kafanikiwa kupindua mfumo halisi wa maisha.
Bado hajafanikiwa
 
Akuna wewe wanaume tunastahili hichi kikombe baadhi yetu wameshakuwa wajinga, mashoga na wenye chuki wao wanadhamini nyeg* tu
Hapana, hili ni kosa kisheria. Kujichukulia sheria mkononi sio sahihi.

Hata hivyo, Mke akizini nje ya ndoa mwenye makosa ni Mke au ni yule Mwanaume aliyezini naye?

Mimi naamini mwenye makosa ni Mke sababu amekubali kwa hiari yake mwenyewe kumsaliti Mumewe.
 
Udhalilishaji sio ishu sana kwa wanaume bali ni moja ya matokeo tuu ya mfumo jike.

Kumdidimiza mwanaume kiuchumi, kimawazo na kiutawala kwa kigezo cha haki sawa.. Inamkatili sana mwanaume na ni kwenda kinyume nature ya maisha ya viumbe hai
Sisi Wanaume tumeruhusu mfumo "jike" kutawala dunia.
 
Sambaza hiyo video ili iwafikie watetea haki, inawezekana hawajaiona tu

Sambaza hiyo video ili iwafikie polisi na watetea haki, inawezekana hawajaiona tu
Kusambaza video ya udhalilishaji ni sehemu ya kushiriki udhalilishaji. Sitaki kuamini vyombo vyetu vya ulinzi na usalama hawajaiona hiyo video.
 
Upepo wa sasa ni KE usijichanganye kabisa utakachofanya ni kuondoka zako km yamekushinda or achana nae km ni mahusiano km ni makazini tafuta kijiwe kipya tu otherwise uwe chawa wake hapo utapewa cheo chochote kikubwa
Mbona unakubali kushindwa kinyonge namna hiyo?

Mimi nafikiri sisi Wanaume bado tunayo nafasi ya kurudisha heshima yetu hata kama dunia imeegama upande wa jinsia ya kike.
 
Mbona unakubali kushindwa kinyonge namna hiyo?

Mimi nafikiri sisi Wanaume bado tunayo nafasi ya kurudisha heshima yetu hata kama dunia imeegama upande wa jinsia ya kike.
Sijasema nimeshindwa ila nimemuelezea mleta mada, timiza wajibu wako na sio kushindana nao kwakua mzani umeegemea kwao so u won’t win ila ww fanya yaliondani ya uwezo wako
 
Usimsingizie shetani huo ni mpango halisi wa Mungu, madhara yamekua mengi sana duniani tangu mwanaume alivyopewa mamlaka , na sasa ni muda wa kukaa pembeni ili dunia ibaki salama
So baada ya kuanza kuwapa hiyo nguvu Dunia imekuwa salama au ndo imekuwa hatari zaidi? Mwanamkd hajaumbwa kuongoza, mifano tunayo...msitake tuandike mengi tutafutwe.
 
Hakuna kosa linalo tambulika kisheria kuwa kufanya mapenzi na mke au mume wa mtu nikosa kisheria ikiwa tuu wamekubaliana kwa hiyari yao wenyewe wote kwa pamoja na ndio maana jambo hilo halina adhabu inayo tambulika kisheria , bali hayo mambo hubebwa kijamii zaidi
Ni kosa la madai. Anayedaiwa ni mgoni. Unaenda kufungua kesi ya madai makakamani. Faini yake unaweza ikwa hata 25k. Ni kupoteza muda kwenda kudai mgoni mahakamani
 
Back
Top Bottom