Udhalilishwaji wa waislam na vyombo vya dola

Udhalilishwaji wa waislam na vyombo vya dola

attachment.php


attachment.php


attachment.php


1. Mkuu hongera, ongeza column ya wapagani:

2. Ongera column ya PhDs.

3. Ongeza column ya Master degree

4. Ongeza column ya 1st (class) degree

5. Column ya (lawyers) private advocate

6. Column ya Madaktari bingwa na interns

7. e.t.c.
 
Ustaadh Moh'd Said. Habari yko hii kuileta hapa JF ni vizuri sana ili wote tupate habari ya kinachojiri TZ na dunia kwa ujumla. Info is power.
Kinachonitatiza hasa ktkt habari yako ni ku asssociate tukio hilo lililokukuta weye na ukandamizwaji wa uislam. Kwanini akili zetu zinatuelekeza huko ktk uonevu wa uislam?
Kuna mchangia mada mmoja ametoa hadi data za uongozi ktk ngazi mbali mbali ikionyesha wakristo wanaongoza kwa wingi. Sasa kweli hiyo ni yard stick ya kuhitimisha kuwa waislam wanakandamizwa? Sitaki kusema kuwa elimu ni mojawapo ya kigezo cha wakristo kushika nyadhifa nyingi manake ndugu zangu mtasema shule nyingi ni za mission na tumebaguliwa.
Nakumbuka miaka ya 1980 shule kubwa ya kiislam iliyokuwa inawika ilikuwa ni 'Kinondoni Muslim' (nilikuwa naishi mitaa hiyo) lakini utashangaa wanafunzi waliokuwa wanaongoza kwa vurugu na mambo mengine ambayo siwezi kuyataja hapa, ni wa K'ndoni muslim. Shule ile hakuna mtu ambaye alikuwa hajui kuwa ilikuwa ni mojawapo ya shule iliyokuwa inafelisha vibaya sana.
Nadhani kuna haja ya kutafakari upya na kuja na takwimu sahihi ku justify hii allegation ya waislam kuonewa. Otherwise tutakuwa tunajirahisisha sana na kuonekana ni watu wa kutaka favour na kupenda malumbano.

Bwana Wagaba,

Yote ulosema ni sawa kabisa na ningeweza kujibu hoja moja baada ya nyingine isipokuwa nitakuwa najirudia tena na tena.

Yaelekea hufahamu mengi katika historia ya nchi yetu na ndiyo maana umekuja na mtazamo huo.

Katika Vita Vya Pili Vya Dunia Wajerumani waliwaweka Wayahudi katika ghetto kule Poland. Kwenye ghetto hakuna maji wala vyoo.

Wajerumani hawa wakawa wanawasema Wayahudi kwa uchafu.
Nadhani umenielewa kwa kukupigia mfano huo.

Sasa wewe umesema Shule ya Kinondoni ilikuwa inaongoza kwa tabia mbovu. Kweli kabisa na ukatunasibisha na shule hiyo.

Ukweli ni kuwa Waislam hawahusiki na chochote na shule hiyo.

Ungeliijua historia ya nchi hii ungeelewa ukweli huu.

Kwa kukusaidia tu.
Hapana haja ya mie kutoa darsa humu ndani.

Wewe mwenyewe uliza watu, fanya utafiti.
Utaupata ukweli.

Na hayo mengine ambayo sikukupa majibu ni hivyo hivyo.
 
Mkuu wangu Mohamed Said, tembo ni mnyama mkubwa sana lakini hapiti akijisifu kwa ukubwa wake, wanaomuona ndio hukiri kuwa kweli tembo ni mkubwa.

Majisifu si uungwana.
Ikiwa umeona hapo nimejisifu ukweli ni kuwa sijafanya hivyo.

Aliyetoa sifa za usomi si mie mimi nimejibu tu kuwa sijasimama katika mada ya usomi.
Kasifiwa mtu kwa "nondo" na "usomi" kuwa nimeshindwa kumjibu huyo msomi.

Ndipo nakasema sijasimama katika usomi.

Hayo unayoita "majisifu" ni maelezo yangu nifahamike kwa wasionijua.
 
ukiangalia baaadhi wanaita wakristu kama wagala

wengine wakiita waislamu kama "osama" au mujahidina itakua no makosa?
 
Bwana Wagaba,

Yote ulosema ni sawa kabisa na ningeweza kujibu hoja moja baada ya nyingine isipokuwa nitakuwa najirudia tena na tena.

Yaelekea hufahamu mengi katika historia ya nchi yetu na ndiyo maana umekuja na mtazamo huo.

Katika Vita Vya Pili Vya Dunia Wajerumani waliwaweka Wayahudi katika ghetto kule Poland. Kwenye ghetto hakuna maji wala vyoo.

Wajerumani hawa wakawa wanawasema Wayahudi kwa uchafu.
Nadhani umenielewa kwa kukupigia mfano huo.

Sasa wewe umesema Shule ya Kinondoni ilikuwa inaongoza kwa tabia mbovu. Kweli kabisa na ukatunasibisha na shule hiyo.

Ukweli ni kuwa Waislam hawahusiki na chochote na shule hiyo.

Ungeliijua historia ya nchi hii ungeelewa ukweli huu.

Kwa kukusaidia tu.
Hapana haja ya mie kutoa darsa humu ndani.

Wewe mwenyewe uliza watu, fanya utafiti.
Utaupata ukweli.

Na hayo mengine ambayo sikukupa majibu ni hivyo hivyo.

Bwana Mohamed Saidi
Unajichanganya na kujidharaulisha sana mbele ya medani ya wasomi; nina uhakika kabisa una agenda za kisiasa na unataka kuwatumia waislamu wenye fikra finyu kimawazo; bado najiuliza ikiwa unaandika utumbo kama huu huko kwenye makongamano unayoalikwa unaongea kitu gani? Iweje leo hii wamerekani na wazungu wa Ulaya ni wabaya kwako ilhali unpokea posho zao haya makongamano si kwamba mnaongea bure kuna posho mnapewa mbona huzikatai? Au pale wanapokuletea tiketi mbona huoji ubaya wao? Hapo kwenye red inaonyesha ni jinsi gani unavyotaka kupotosha jamii; hivi Kinondoni Muslim inaendeshwa na baraza la maaskofu Tanzania?

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Mohamed Said, kubali kuwa hadi sasa umechemsha vibaya sana! yaani kama utasoma post ya Nguruvi3 na Mzee
mwanakijiji basi majibu ya malalamiko yako yote yako post hizo. Yaani kama ni ngumi basi wamekupiga za uso. Utaki unaacha.

Kwa ufupi Brother MS akisoma post za akina Nguruvi3 Mzee Mwanakijiji KipimaPembe na chama kama ataendelea na mnakasha basi atakuwa ni mbishi tu...
 
Last edited by a moderator:
Barubaru, mbona huwa hupendi kujibu maswali ya msingi na kukimbilia kulialia kama mtoto mdogo?!!! Tuambie wewe binafsi ulipokuwa unafanya kazi wizara ya fedha, uislam wako ulikusaidiaje kuleta ufanisi wa kazi? Mbona hututajii makabila ya hao wanaofanya kazi baraza la mitihani? Wewe na huyo kizee Mohamed Saidi ni watu hatari sana katika nchi yetu. Bora hata wewe uliyeukataa utanzania maana ingekuwa fedheha sana kwa mtanzania mwenye mawazo ya kipuuzi kama yenu!

Gwalihenzi;
Barubaru asikuumize kichwa ni mmoja kati ya wanafiki wakubwa hao ndio wanaodai mfumo kristo cha ajabu yeye watoto wake wanaishi na kusoma Marekani kwenye mamilioni ya wakristo; Barubaru huyu huyu amesoma chuo kikuu cha Dar es Salaam kwa sera za Mwalimu Nyerere; Barubaru amesoma Canada kwa pesa za walipa kodi wakristo wa Canada; hana jipya; kama si sera za Mwalimu Nyerere Barubaru angekuwa mvuvi Pemba au anauza Ice Cream kwa Bakhresa

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Bwana Mohamed Saidi
Unajichanganya na kujidharaulisha sana mbele ya medani ya wasomi; nina uhakika kabisa una agenda za kisiasa na unataka kuwatumia waislamu wenye fikra finyu kimawazo; bado najiuliza ikiwa unaandika utumbo kama huu huko kwenye makongamano unayoalikwa unaongea kitu gani? Iweje leo hii wamerekani na wazungu wa Ulaya ni wabaya kwako ilhali unpokea posho zao haya makongamano si kwamba mnaongea bure kuna posho mnapewa mbona huzikatai? Au pale wanapokuletea tiketi mbona huoji ubaya wao? Hapo kwenye red inaonyesha ni jinsi gani unavyotaka kupotosha jamii; hivi Kinondoni Muslim inaendeshwa na baraza la maaskofu Tanzania?

Chama
Gongo la mboto DSM

"On 28 April, 1993 bizarre occurrence took place. In desperation and in its effort to salvage BAKWATA the Minister of Home Affairs and Deputy Prime Minister Augustine Mrema convened a meeting between Muslims and Christians at the Diamond Jubilee Hall, Dar es Salaam. The agenda was not known. The Church sent a strong delegation.

Muslims abstained except BAKWATA. The few Muslims who turned up were there out curiosity rather than conviction that the meeting would bear fruits. When the time for introduction between the two parties came, Muslims present at the meeting refused to shake hands with the Church leadership.

This was an embarrassment to the government propaganda machinery sent to the meeting by the Christian Lobby to record and broadcast the event. Mrema addressed the meeting in which in his speech it was revealed that elections for BAKWATA were long overdue and could not be held because of lack of funds.

The Church volunteered to provide money to BAKWATA to enable it hold its elections.
The Minister for Home Affairs Augustine Mrema also helped to collect money from the business community to fund BAKWATA elections.

When eventually BAKWATA met in Dodoma from 10 th-12 th May the guest of honour was Augustine Mrema. Instead of conducting elections BAKWATA passed some constitution changes to empower the Grand Mufti Sheikh Hemed bin Hemed with absolute powers to fire any executive member without being answerable to anyone.

Baraza Kuu has survived alongside BAKWATA and has full support of Muslims but all the succeeding governments have refused to recognise it as true representative of Muslims of Tanzania Mainland."

Inatoka katika mada "Christian Hegemony and the Rise of Muslim Militancy in Tanzania." Mada hii ilitolewa Zentrum Moderner Orient, (ZMO) Berlin, March 2011.
 
Sio hazijibiki, huwezi kujibu hata hoja moja wewe! Kama nimetukana na nifungiwe!

Kwanza nunua kamusi, usitupotoshe na tafsiri za viingereza vibovu hapa, sio wewe peke yako "uliyefika chuo kikuu kutokea Kariakoo." Kazi kupandikiza chuki za kidini, hoja zenyewe nyepesi ka boya.




cock.jpg

Nacheka peke yangu maana huwezi kuamini siku zote katika fikra zangu huwa nikitumia neno "cock" nikiwaza kuku jike kumbe jogoo.

Ahsante sana.
Umeninufaisha.
 
Brother MS...

Salaam sana Mkuu, baada ya kusoma maandiko yako kwenye hii thread, naendelea kujiuliza maswali mengi...kwa jinsi unavyo-draw conclusion zisizo na mishiko hata kidogo......katika uliyoandika hapo juu hakuna hata sehemu moja uliyoweza dhihirisha kuwa treatment uliyoipata pale terminal building, ilikuwa na lengo la kudhalilisha uislam/waislam.....

maneno uliyoandika wakiyasoma watu ambao sio wazoefu wa kusafiri....may be wanaweza kuamini...hata hivyo mtu mwenye akili timamu na mwenye uelewa....hatakubaliana nawe.....

Juzi juzi tu baada ya uchaguzi kule Egypt nilipata fursa ya kupitia Uturuki....nikawekwa pembeni kwa ajili ya kupekuliwa, nilipoteza muda mwingi sana airport hata kuchelewa ndege iliyokuwa nisafiri nayo.....sasa sijui nami niseme nilidhalilishwa kwa kuwa "I'm Black"....maana suala la uislam halikuwepo!
 
"On 28 April, 1993 bizarre occurrence took place. In desperation and in its effort to salvage BAKWATA the Minister of Home Affairs and Deputy Prime Minister Augustine Mrema convened a meeting between Muslims and Christians at the Diamond Jubilee Hall, Dar es Salaam. The agenda was not known. The Church sent a strong delegation. Muslims abstained except BAKWATA. The few Muslims who turned up were there out curiosity rather than conviction that the meeting would bear fruits. When the time for introduction between the two parties came, Muslims present at the meeting refused to shake hands with the Church leadership. This was an embarrassment to the government propaganda machinery sent to the meeting by the Christian Lobby to record and broadcast the event. Mrema addressed the meeting in which in his speech it was revealed that elections for BAKWATA were long overdue and could not be held because of lack of funds. The Church volunteered to provide money to BAKWATA to enable it hold its elections. The Minister for Home Affairs Augustine Mrema also helped to collect money from the business community to fund BAKWATA elections. When eventually BAKWATA met in Dodoma from 10 th-12 th May the guest of honour was Augustine Mrema. Instead of conducting elections BAKWATA passed some constitution changes to empower the Grand Mufti Sheikh Hemed bin Hemed with absolute powers to fire any executive member without being answerable to anyone. Baraza Kuu has survived alongside BAKWATA and has full support of Muslims but all the succeeding governments have refused to recognise it as true representative of Muslims of Tanzania Mainland."

Inatoka katika mada "Christian Hegemony and the Rise of Muslim Militancy in Tanzania." Mada hii ilitolewa Zentrum Moderner Orient, (ZMO) Berlin, March 2011.

Bwana Mohamed Saidi
Hebu tamka bayana kwamba BAKWATA si chombo cha waislamu; sioni ni wapi kwenye hiyo article inakanusha kwamba BAKWATA si chombo cha waislamu; hapo kwenye red hamaanishi kwa Kanisa kutaka kusaidia kufanyika uchaguzi kunaondoa dhana nzima ya BAKWATA kama chombo cha Waislamu; na pia haoinyeshi kama BAKWATA walipokea pesa za kanisa; na sioni lipi jipya katika jamii yetu ya watanzania wapo wakristo wamechangia ujenzi wa misikiti na wapo waislamu wamechangia shughuli nyingi za makanisa; je unataka kusema wanaoswali kwenye misikiti hiyo si waislamu?

Na hiyo kama ni hoja wapo mafundi waashi na waezekaji, pamoja na vibarua wao ni wakristo wamejenga misikiti je tukiswali kwenye misikiti hiyo tunapoteza Uislamu wetu? Nimekuuliza hizi posho mnazopewa kwenye warsha na makongamano yanayoandaliwa na serikali za Marekani na Ulaya mbona huzikatai?

Hebu nipe jibu la msingi; na kataa bayana kwa herufi kubwa kwamba BAKWATA si chombo cha Waislamu ili tuwahoji BAKWATA wanamwakilisha nani; tafadhali nijuze kwenye hayo machache nataka kauli yako na si nukuu kutoka kwa watu wengine.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Wanajamvi,
Nimefuatilia mjadala huu nikidhani kuwa tunaijadili mada kama ilivyoletwa. Tofauti, naona takwimu za elimu na mengine yasiyo na uhusiano na mada. Ukifutailia utagundua kuwa MS anakwepa kujibu hoja na kutumbukiza mengine au zile mada zake zimewaingia vema baadhi yetu na kila mara wanazifikiri bila tafakuri.

Wanakosa tafakuri kwasababu makala za MS zinachanganya na zinahitaji utulivu na fikra kuzielewa na kuzinyumbulisha ili upate hitimisho alilokusudia. MS anauwezo sana wa kufanya majumuisho yanayoeleweka kiurahisi sana kwa wale aliokusudia (Conclusion) hata kama hawaielewi mada.

Mathalani, katika hii mada hii hitimisho lake ni uonevu kwa waislam unaotokana na mfumokristo uliowekwa na Nyerere unaowadhalilisha viongozi wa dini kwa kutumia vyombo vya dola vinavyoongozwa na mfumo unaopinga na kupiga vita uislam. Hitimisho kama hilo litamtia hasira asiyebahatika kuelewa maandiko ya MS hili likiwemo.

Wanasaikolojia wanasema njia rahisi sana ya kumshinda mpinzani wako ni kwanza kumfanya dhalili (inferior).
Kwa bahati mbaya MS yeye ndiye anawafanya watu wake inferior na wala si mwingine.

Amefanya Waislam wa Tanzania wajione dhalili(inferior) hata kwa yale wanayoweza.
Udhalili ni kuwafanya wawe wanalalamika, wanadai hata kilicho ndani ya uwezo wao, kuwafanya wajione ni watu duni na wanaohitaji upendeleo maalumu na hata kuwadhalilisha kwa maamuzi yao(hili la mwisho nitalifafanua)

MS amefanya watu wafikiri kuwa ili ufanikiwe ni lazima uwe na waziri mwislam, katibu mkuu mwislam au mkurugenzi mwislam. Unaposhindwa kufanikiwa basi tatizo lako ni dini yako na wala si jitihada zako.
Huku ni kuwapoteza watu na kuwafanya wasijitambue. Matokeo yake ni yale ya wazee wa Bagamoyo kama alivyosema Rais Kikwete.

Wazee wa Bagamoyo walimuomba awasaidie vijana wao kupata kazi na hili wala si kosa ni privilege yao.
Tatizo ni pale Rais alipowaambia walete vyeti, na kwa mshangao watarajiwa wakampelekea vyeti vya udereva!!
Rais akawauliza hivi hili kweli linahitaji msaada! kwamba vijana waliokosa kazi ndio hawa na Rais awatafutie udereva! Hawa ndio wanaolalamika mfumo mbaya! Hawajaliona tatizo kwasababu wana hitimisho- uonevu

Kuna kijana mmoja alikuja Dar es Salaam, baada ya kumaliza shule akapania kuwa mtu wa kompyuta.
Masikini hakujua kutumia key board zaidi ya kubofya herufi. Nia yake ilimpelekea asaidiwe kujiunga na chuo cha Diploma (NIIT). Akamaliza diploma na kujiunga na program ya degree inayotolewa kwa ushirikiano na chuo cha UK.
Kwa nia iliyothabiti akahitimu utaalam na maisha yake leo hii yamebadilika (180 Degree)
Anatafutwa kwa kazi hatafuti kazi, amevuka vizingiti vyote kwasababu ana silaha inayoitwa elimu.
Huyu hakutegemea waziri, mkuu wa baraza la mitihani, wala katibu mkuu mwenye jina la Mohamed, Hussein au William

Tatizo la MS ni kuwapa watu conclusion ili waifanyie kazi. Matokeo ya hayo ni watu kudhani kuwa dunia ya leo bila jitihada unaweza kufanikiwa tu uwe mkristo au mwislam. Kuwaaminisha watu kuwa mtu anayeitwa Juma Abdul katibu wa baraza la mitihani ndiye chachu ya mafanikio ni kuwadanganya.

Wataalam wa Engineering wana misemo yao (nisahihishwe kama nimekosea) ya kupata majibu ya tatizo.
Wanasema ili uweze kupata chanzo cha tatizo ni vema ukajiuliza neno kwanini (why) si chini ya mara tano.

Nitoe mfano;
1. Kwanini (why) kilwa ina umasikini mwingi, jibu ni kuwa hawana silaha ya kupambana na mazingira(elimu)
2. Kwanini (why) hawana elimu, jibu ni kuwa hawakufanya mitihani ya kuwasadia kwenda mbele
3.Kwanini (Why) hawakufanya mitihani, jibu ni kuwa hawakujiandikisha
4. Kwanini (why) hawakujiandikisha, jibu ni kuwa shule ilifungwa
5. kwanini(why) shule ilifungwa, jibu ni kuwa wanafunzi walitoroka wote
6. Kwanini (why) walitoroka, jibu hawana msukumo wa elimu
7. Kwanini (why) hawana msukumo wa elimu, jibu wazazi hawana hamasa

Hadi hapo tatizo la Kilwa si umasikini, tatizo ni wazazi kutokuwa na msukumo wa elimu.
Badala ya kuwaambia Wakilwa kuwa ni masikini eti kwasababu waziri wa elimu tangu uhuru ni mmoja na katibu wa baraza hajawahi kutokea kuwa mwislam, Wakilwa wanapaswa kuelezwa chanzo cha tatizo lao la kukosa hamasa.

Ukishajua tu tatizo basi una ufumbuzi wa tatizo. MS anachowambia watu wa Kilwa ni kuwa uwepo wa waziri mwislam ndiyo suluhisho la matatizo yao na wala si kujenga shule, vyuo vya ufundi na kuwasukuma watoto kama yule niliyemtolea mfano hapo juu wa kompyuta.

Ukirejea hapo juu nimesema MS anawadhalilisha waislam. Anaposema bunge limefanya maamuzi kwa shinikizo la wakristo, anatachotaka kueleza ni hitimisho (conclusion) kwa wasomaji na wasikilizaji. Asichowaambia ni kuwa wabunge hawateuliwi bali wanachaguliwa. Wanachaguliwa kwa hoja zao na wananchi wanaoamini watawawakilisha bila kujali dini zao au makabila.

Asichowaambia Watu ni kuwa chama cha CUF hakikuwa na mbunge wa kuchaguliwa hata mmoja licha ya kujinasibisha na dini. Watanzania wote wanajua kwanini wanachagua kiongozi. Anaposema bunge la wakristo anawadhalilisha waislam waliotumia haki yao kumchagua wanayemtaka. Anachotaka kusema hapa ni kuwa mfumo kristo ndio unawafanya wasiwepo wabunge wengi waislam. Hakika sipendi mada za udini lakini ni vema tuelezane ukweli.
MS tafuta (why) zisizopungua 5 utapata jibu na wala jibu si kumshambulia Nyerere au imani yake! Nitty gritty.

Eleza ukweli,chanzo na sababu na si hitimisho.
Huhitaji kuwa na wakuu wa elimu wa mikoa, unahitaji vijana wliofuzu kada mabali mbali na hao wataijengea jamii yao uwezo wa kuwa na wabunge na mawaziri.

Unahitaji watu wa kupambana na dunia hii ya ushindani na si viti maalumu au nafasi za upendeoe.
Unahitaji technicians 100 na si katibu mkuu mmoja.Haya hayapatikani hadi utakapoeleza ukweli.

Wazungu wana msemo wao ya kuwa
''If you have a problem and you can't solve you're the problem to begin with''
 
Kuna vitu nimejifunza kwenye mjadala huu

- Rais, Makamu wa Rais, Rais wa znb na makamu wake wawili wote ni waislamu na wakristo hawalalamiki.
- Mara ya kwanza kumsoma MM akichangia topic ya kidini.
- ATM card ya Mohd Said ilikatataa kutoa hela kwenye ATM kwa siku moja kwa sababu ni Muislam.....du!!
- Wakristo hawajalalamika kuteswa Dr. Ulimboka kwa minajili ya udini.
- Shule ya Kinondoni Muslim inabidi iwe na management mpya kuibadilisha taswira yake mbele ya jamii.

Pamoja na hayo, bado sijajua kama ni kweli huko Uarabuni makanisa hayaruhusiwi?
 
Brother MS...

Salaam sana Mkuu, baada ya kusoma maandiko yako kwenye hii thread, naendelea kujiuliza maswali mengi...kwa jinsi unavyo-draw conclusion zisizo na mishiko hata kidogo......katika uliyoandika hapo juu hakuna hata sehemu moja uliyoweza dhihirisha kuwa treatment uliyoipata pale terminal building, ilikuwa na lengo la kudhalilisha uislam/waislam.....

maneno uliyoandika wakiyasoma watu ambao sio wazoefu wa kusafiri....may be wanaweza kuamini...hata hivyo mtu mwenye akili timamu na mwenye uelewa....hatakubaliana nawe.....

Juzi juzi tu baada ya uchaguzi kule Egypt nilipata fursa ya kupitia Uturuki....nikawekwa pembeni kwa ajili ya kupekuliwa, nilipoteza muda mwingi sana airport hata kuchelewa ndege iliyokuwa nisafiri nayo.....sasa sijui nami niseme nilidhalilishwa kwa kuwa "I'm Black"....maana suala la uislam halikuwepo!

Bwana Ogah,

Ulichosema ni kweli lakini mfano huo haujafanana na wangu hata kidogo.
Mie nina mengine sijayasema.

Ama kwa kuwekwa katika mahojiano uwanja wa ndege...miaka ishirini na moja iliyopita niliwekwa chini Heathrow Terminal Four kwa sababu pasi yangu ilionyesha nasafiri sana nje ya Tanzania.

Jingine mkoba wangu ulikuwa na nguo nzuri nzuri. Hili liliwatia wasiwasi kuwa nina fedha nyingi. Nimezipata wapi?

Kwa muhtasari nilipata "body search" na viatu vyangu vilipelekwa kufanyiwa X Ray.
Walidhani ni "muuza unga."

Maelezo kuwa nasafiri huko kote kwa ajili ya masomo hayakuwaingia hata kidogo.

Nikajapita tena hapo baada ya miezi mitatu baadae wakaniuliza kuwa safari hii unaingia Uingereza kufanya nini?
Nikawaambia nakwenda shule.

Nikajapita tena baada ya miaka miwili nikitokea Ufaransa wakanambia wewe umewahi kuishi hapa. Nikajibu ndiyo. Sasa kimekuleta kitu gani?

Nikawaambia nimekuja kutembea. Nikapita. Siku zile hatuingii Uingereza kwa visa.

Kwa hiyo haya mambo nayajua vyema.

Yalokuja kunifika kuanzia 2006 kila ninaposafiri hayana mfano na hayo ya miaka ya 1990.
 
Wanajamvi,
Nimefuatilia mjadala huu nikidhani kuwa tunaijadili mada kama ilivyoletwa. Tofauti, naona takwimu za elimu na mengine yasiyo na uhusiano na mada. Ukifutailia utagundua kuwa MS anakwepa kujibu hoja na kutumbukiza mengine au zile mada zake zimewaingia vema baadhi yetu na kila mara wanazifikiri bila tafakuri.

Wanakosa tafakuri kwasababu makala za MS zinachanganya na zinahitaji utulivu na fikra kuzielewa na kuzinyumbulisha ili upate hitimisho alilokusudia. MS anauwezo sana wa kufanya majumuisho yanayoeleweka kiurahisi sana kwa wale aliokusudia (Conclusion) hata kama hawaielewi mada.

.........''

Hoja nzuri na zinahitaji majibu ambayo yatamfahamisha msomaji ukweli wa mambo.

Waislam wamegundua mengi katika mfumo wa serikali yetu na wameitahadharisha kuwa kuna upendeleo kwa Wakristo na hujuma dhidi ya Waislam.

Ushahidi upo.

Rejea tu matatizo ya hivi karibuni yaliyogunduliwa NECTA achilia mbali utafiti wa Warsha wa mwaka 1991 na aliyoyagundua marehemu Prof. Malima ndani ya Wizara ya Elimu.

Ingependeza kama serikali yenyewe ikatoa majibu.
Serikali iko kimya majibu yanatolewa na watu wengine kabisa kama hivi humu JF.

Somo hili mimi nimeliandikia kitabu kizima.
Itakuwa vigumu kukupa jibu humu JF.

Hata hivyo ukiwa una wasaa soma kitabu changu "Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes...." sehemu ya tatu ya kitabu inaitwa, "Njama Dhidi ya Uislam."

Hapo utasoma nilichosema kinachofanyika kwa miaka mingi dhidi ya Waislam kuanzia ukoloni wa Wajerumani hadi hivi sasa.

Kitabu hiki ndicho kilichonifanya nikajulikana kwingi.
Maudhui yaliyo ndani ya kitabu hiki yamegusa fikra za wasomi wengi duniani.

Haijafanyika utafiti wowote kuhusu siasa za Tanzania sharti mtafiti apitie kitabu hiki.
Hapa jamvini kitabu hiki ni mashuhuri.

Mimi niko tayari kusimama na yeyote na mahali popote kuhusu mada hii.
 
Bwana Mohamed Saidi
Hebu tamka bayana kwamba BAKWATA si chombo cha waislamu; sioni ni wapi kwenye hiyo article inakanusha kwamba BAKWATA si chombo cha waislamu; hapo kwenye red hamaanishi kwa Kanisa kutaka kusaidia kufanyika uchaguzi kunaondoa dhana nzima ya BAKWATA kama chombo cha Waislamu; na pia haoinyeshi kama BAKWATA walipokea pesa za kanisa; na sioni lipi jipya katika jamii yetu ya watanzania wapo wakristo wamechangia ujenzi wa misikiti na wapo waislamu wamechangia shughuli nyingi za makanisa; je unataka kusema wanaoswali kwenye misikiti hiyo si waislamu? Na hiyo kama ni hoja wapo mafundi waashi na waezekaji, pamoja na vibarua wao ni wakristo wamejenga misikiti je tukiswali kwenye misikiti hiyo tunapoteza Uislamu wetu? Nimekuuliza hizi posho mnazopewa kwenye warsha na makongamano yanayoandaliwa na serikali za Marekani na Ulaya mbona huzikatai? Hebu nipe jibu la msingi; na kataa bayana kwa herufi kubwa kwamba BAKWATA si chombo cha Waislamu ili tuwahoji BAKWATA wanamwakilisha nani; tafadhali nijuze kwenye hayo machache nataka kauli yako na si nukuu kutoka kwa watu wengine.

Chama
Gongo la mboto DSM

Bwana Chama,

Ikiwa kwa hakika uanpenda kujua historia ya Bakwata kwa undani wake nakuomba tafadhali soma kitabu changu. Kisa kizima nimekieleza humo.

Hapa nafasi itakuwa ndogo na nitawachosha wanaukumbi.
 
Mimi niko tayari kusimama na yeyote na mahali popote kuhusu mada hii.
What a challenge!
Ningependekeza kuwa aidha mmoja wa upande wa pili ajitokeze na tufungue thread kuhusu hili (suala hili ni muhimu sana ktk mustakbali wa Taifa) au Waislamu tukisema tunahujumiwa tueleweke kuwa tunahujumiwa.
 
Usiwe Duyusi hata katika kufikiria yaliyotunzunguka katika Ulimwengu Adof hitler amefariki lakini amewacha wafuasi wake na ajenda zake zikiendelea na kama alivyokufa Kambarage amewacha wafuwasi wake waendeleze

Haaahaaa Sonara! Endeleeeni tu na mbio hizi. Maana mbio za sakafuni tunajua huishia ukingoni. Kamwe hakuna mtu atakayepata kitu asichofanyia kazi....kamwe hakuna mtu atakayevuna pale asipopanda. Who are you to violate the natural laws and principles that govern our universe?
 
Last edited by a moderator:
Ndio maana makundi kwa makundi ya watu wanaingia na kufata mfumo wa Maisha wa Mwenyeezi Mungu nao ni Uislaam.

Lie,lie ,lie .angalia syria ,iraq ,yemen ,afghanistan,lebanoon .somalia. Wanauwana kilasiku ,sijui mungu gani huyo unae mzungumzia . Njoo huku tukubatize kwa jina la yesu
 
Back
Top Bottom