Udhalimu wa Utumwa Zanzibar na Pemba: Mababu zetu waliteswa, walihasiwa, walibakwa, na kuuawa kinyama

Thank you brother Mohamed for the useful information.
 
Ama kweli akili ni mali.

Eti unaleta rejea kutoka Wikipedia!

Hiyo Wikipedia mtu yeyote anaweza kuhariri (hata mie naweza kwenda hapo nikaandika wazungu wabaya)

Hahaha

Waovu ni viongozi wetu waliosababisha tz kuwa masikini mpaka leo, hao ndio waovu wa kweli.
 
Maneno yako ni kweli kabisa. Shukran.
 

Kwanza watu wa pwani sio wavivu.

Pili watu wa pwani ndio walioendelea na Wastaarabu zaidi in tz. Waungwana sana na watu wa dini wenye utu.

Tatu, Nyerere alikuwa anawafelisha wanafunzi wa Kiislamu kwa makusudi, ndio maana Waislamu hao wa Pwani hawana shahada za kupata kazi nzuri serikalini.
 
Mkuu Maalim, naomba sana tujikite kwenye mada!. Hii ni mada kuhusu andiko hili, kwa yaliyotokea Zanzibar!. Kitendo cha kuleta madhila mengine mabaya zaidi, yaliyofanywa na watu wengine mahali pengine duniani ni kutaka kuhalalisha udhalimu wa Waarabu, kwa kuonyeshea, waliyoyafanya Waarabu ni madogo, shuhudieni makubwa!.

Unachotakiwa kufanya ni kwanza kukiri, Waarabu wa enzi zile walikuwa ni watu madhalimu!, kisha ndipo ukasema, pamoja na udhalimu wao, kuna watu humu duniani ni madhalimu na makatili kuliko Waarabu, ndipo ukatuletea mifano, ili kuhusianisha hoja zako na hoja iliyoko mezani!.

Pasco
 
Pasco,
Mimi mzito sana kutumia maneno makali lakini kuna
watu hapa wamekuambia kuwa elimu yako ni ndogo
sana.

Kinachokusukuma ni chuki dhidi ya Uislam ambayo
umeificha nyuma ya pazia la Waarabu.

Unasema Waarabu wa enzi zile...
Kwani Transatlantic Slave Trade imefanyika leo?

Unaijua historia ya Spaniards na unyama waliofanya
Latin America?

Hawa waliishi leo?
Pasco,
Hebu fanya bidii usome kwanza.
 


Naheshimu michango yako lakini nikusaidie tu wewe bado sana.

Endelea kujifunza kabla ya kuanza kujadili na watu.
Uko too shallow, biased na unakimbilia kichaka cha dini, huku umejaa matusi. Sioni kama dini ikiwa imekusaidia chochote.

Jifunze kwanza historia ya dunia halafu ujifunze kujadili. Matusi, kebehi, dharau, chuki za kidini huwa zinahamisha watu kwenye mada husika.
 

Asante kwa kutoa msimamo wako.

Wengi wanaojificha ktk kichaka cha dini na chuki za kidini wajifunze historia na kuelewa mambo ya dunia.
Kwamba WAARABU na WAZUNGU kwa namna, style na vipindi tofauti tofauti walituonea, kutunyanyasa, na kutukandamiza watu weusi. Huu ni ukweli ambao hakuna atayefanikiwa kuuficha.

Kitu ambacho nimejifunza watu wengi ni rahisi kujadili matatizo yote haya lakini tukifika kujadili utumwa wa Afrika Mashariki watu mnakuwa wakali kama pilipili, au humu JF kuna wabia wa hiyo biashara ya utumwa?
 
Mkuu Maalim
Mohamed Said
, chuki na Waislamu itoke wapi, hata hawa Waarabu niliowaandika hapa, sina chuki nao kabisa!, kwa taarifa tuu, mke wangu wangu mkubwa ni Mwislamu!, nilipoanza anza kazi RTD, nilipikwa na safu ya Watangazaji mahiri wote Waislamu, Suleiman Hegga, Abdul Ngarawa, Ahamed Jongo, Salim Seif Mkamba, Juma Ngodae, Ahamad Kipozi, Sekioni Kitojo, Salama Mfamao, Siwatu Luanda etc, niwachukie kwa lipi?!.

Nipoanza kazi, nilipangishwa nyumba ya Mwislamu pale Ilala Sharif Shamba, Mwajuma Mchuka wa ATC, nikiishi na Muislamu Aboubakar Liongo, nilikuwa napikiwa kwa Da Mwajuma, mwaka mzima na mwezi Mtukufu nilifunga, kanzu na kofia hadi leo ninavaa!. Alipohama kuamia Masaki, Mdogo wake Halima Mchuka (RIP) aliendelea kutuhudumia hadi ... sasa niwe na chuki na Waislamu za nini?!.

Nilipoondoka RTD, niliajiiwa DTV, waajiri wangu ni Waislamu watupu na Waarabu, Nilipoondoka DTV, nilitunza na kulelewa na Sheikh Jabir, nimefanyiwa mema mengi na Waarabu/Waislamu!. Japo mimi ni Mkristo Mkatoliki lakini naukubali sana Uislamu, hapa nilipo nina wake 3 bado mmoja nitimize nguzo!. Kwenye hoja ya mahakama ya kadhi, nimewatolea hoja muruwa kuhusu ufumbuzi wake kulikoni hata nyinyi Waislamu wenyewe, hebu kanisome hapa, kweli mtu mwenye kuuchukia Uislamu anaweza kutoa ushauri kama huu,
Mwarobaini wa Kweli wa Mahakama ya Kadhi ni Huu?.

Kuna tatizo la baadhi ya Waislamu waliofilisika kuusianisha Uislamu na Uarabu!, hivyo ukizungumziwa udhalimu wa Waarabu, wao wanatafsii ni udhalimu wa Waislamu!. Udhalimu ni udhalimu, hauna dini , rangi, wala kabila!. Kama hoja ni Lugha ya Kiarabu, hata Nabii Issa Bin Maryam, alizungumza Kiarabu.

Mada hapa ni kuhusu unyama wa Waarabu waliowafanyia babu zetu!, sasa ili kuupunguza unyama wa Waarabu, sasa ndio unatuletea unyama mkubwa zaidi ya huo wa Waarabu, ili sote kwa pamoja tuseme, afadhali ya Waarabu?!, kama Spaniards nao ni wanyama kuliko Waarabu, na unyama waliofanyia Latin America?, pandisha uzi wake, tutachangia!. Uzii huu ni kuhusu unyama wa Waarabu!.

Pasco
 
Inawezekana ulikirimiwa na kupata malezi ya kiungwana na ukawa na chuki ndani ya moyo kwa waislamu na ukweli unadhihiri unapojenga na kujibu hoja kwa kujificha kwenye kivuli cha hayo unayoyasema
 
Pasco ni Jembe. Kaanzisha uzi, umejaza walaji kwasababu una mantiki sana.

Huu uzi hata mimi nimejifunza.
Nashangaa watu wengine humu wanakuja kuwatetea wakoloni kwa kukompea na kushindanisha ukoloni.
Ukoloni ni ukoloni tu. Kuna tofauti ya uhuru na ukoloni.
Acheni uzi wa pasco kama hamma hoja za ou argue.
Ad hominem zimejaa humu. Pasco kawavua kanzu wakoloni wa kiarabu [emoji3].
Adumu mtu mweusi.[emoji119]
 

Hapana, si kweli. Pasco hakuanzisha huu uzi, Pasco kajibu uzi ulioanzishwa na Mohamed Said.

Na majibu yenyewe aliyojibu ni utumbo mtupu wa ujinga aliojazwa, hamna ukweli hata chembe.
 
Pasco,
Sijamsafisha yeyote nimekuwekea historia ya dunia na ukatili wa uliofanywa.

Labda nikuwekee ni hii hapo chini:
Vietnam War casualties - Wikipedia, the free encyclopedia

Hoja hapa ni unyama ulopitika hatubagui.
Brutal Exposure: the Congo - International Slavery Museum, Liverpool museums
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…