Udhalimu wa Utumwa Zanzibar na Pemba: Mababu zetu waliteswa, walihasiwa, walibakwa, na kuuawa kinyama

Rangi gani tofauti na mwafrika aliyetutawala huku akitufanyia mazuri?




Tembeleeni mkoa kwa mkoa andikeni mauwaji yanayofanyika baina ya utawala na wananchi au wananchi kwa wananchi.

Zanzibar inadaiwa kuna ulawiti mwingi kupitia media za mitandaon.


Je ushawahi sikia wameuwa albino au wamechomana moto sababu ya ushirikina vipi hawa watanzania wana roho nzuri ndan ya NCHI HURU,wanajua thaman ya mtanzania mwenzao?

Hao waarabu walijuaje sisi dili?


Mwembe yanga mtanzania hakujua umuhimu wa mtanzania mwenzake.

Mauwaji ya Zanzibar muafrika hakujua umuhimu wa mwafrika mwenzake.

Migodini Wazungu na watanzania( watawala WAARABU WA KIPINDI HIKI) hawajui umuhimu wa watanzania wenzao.



Kuna ajabu mgeni kutokujua umuhimu wako?


KILA JAMBO NA WAKATI WAKE tusilishane chuki.



HESHIMA KWAKO MKUU P.
 
Pascall ni mjinga kama wajinga wengine , mm sikushangai kuleta uzi huu kwa mbwembwe lakini hauna mashiko isipokuwa kutaka kuwaaminisha kwamba CCM na Serikali zake wanayofanya simakubwa,
Mkuu Raskazone, kwanza naomba kukubali kwa moyo safi na roho nyeupe kuwa mimi ni mjinga. Ujinga ni ile hali ya kutokujua, ukielimishwa ukajua, Ujinga unakutoka unakuwa mwerevu, hivyo naendelea kujielimisha, mwisho wa siku Ujinga utanitoka nitakuwa mwerevu.

Kwanza hili jina la Paskali sio jina la kujiita, bali ndilo jina langu kweli na ni verified member. Jina la kujiita ni alias au a.k.a, hivyo mimi ni Paskali na sio ninajiita Paskali.

Baada ya kule mwanzo kukubali mimi ni mjinga, lakini pamoja na ujinga wangu wote, kila nipatapo fursa kujielimisha hujielimisha na kuelimisha wengine kile ninachojua kama lilivyo bandiko hili ni la uelimishaji.

Kwenye hoja ya biashara ya utumwa makanisani na kutolea mfano Kanisa la Mkunazini lenye hadi makumbusho ya utumwa, wewe ndio mjinga!.

Hapo lilipo kanisa, ndilo lilipokuwa soko kuu la watumwa Zanzibar.

Baada ya kupigwa marufuku biashara hii dhalimu, wamiliki wa watumwa waliowanunua waligoma kuwaachia huru. Hivyo Wamasionari walitoa fedha kuwarudishia hao wamiliki ndipo watumwa wale wakaachiwa huru na wakawa hawana pa kwenda hivyo kujikuta wamerudi tena lilipokuwa soko ili kujihifadhi huku Wamasionari wakiwalisha na kuwatunza.

Kwa vile biashara hiyo imepigwa marufuku na soko la watumwa hakuna biashara tena bali limejaa watumwa huru, ndipo Kanisa likaomba eneo hili toka kwa Sultani wa Zanzibar, ili kuwajengea makao ya kuwahifadhi watumwa huru, wakapewa ndio wakajenga Kanisa na kuacha eneo kidogo kuhifadhi historia ya utumwa na sio kwamba biashara dhalimu ya utumwa ilifanywa makanisani!.

Jamii yote ya Wakristu wa Zanzibar ni waliokuwa watumwa wakagombolewa na Wamasionari na kuingia Ukristo.

Natumaini sasa bandiko hili litakuwa limekufungua macho, hivyo kukutoa katika ule ujinga wako na kukuleta kwenye werevu.

Paskali
 
Hizi pic ha niwatumwa waliofanywa na wajerumani Tanganyika ,halafu zikageuzwa kuficha udhalimu wa wazungu,Kwa sababu za kidini
Wajerumani na waingereza walifanya mambo makubwa Kwa waafrika wa Tanganyika lakini yanafichwa Kwa Sababu ya udini .
Mkuu Abuha, hizo picha nilizizungumza ila pia humu JF ukisema lolote kuhusu Waarabu, huibuka wafia dini muflisi kama wewe, hivyo tayari niliisha toa angalizo

Nawe umetembea mule mule! .

Paskali
 
 
Mkuu Pascal ninaheshimu dini zote,haswa kwa Kwa vile,Nina wandugu wenye imani tofauti,tatizo hapa wewe Ni mdini,umeelezea mengi ya utumwa,lakini umeshidwa kuwagusa washiriki wakuu wa utumwa Kwa Tanganyika,kama wajerumani na waingereza, nakadhalika,ambao waliwatesa waafrika wa watanganyika na sehemu kubwa ya Afrika,Kwa kuwafanyisha makazi katika mashamba ya pamba na mikonge nakadhalika,kwa jina la umisionari/ukristo,tatizo lako umekua unbalance katika maelezo yako,Kwa kuuficha ukweli,sababu ya utashi wako wa kiimani,hilo umejaribu kulificha sana,Kwa kujaribu kuchanganya uarabu,uislamu,ukristo,Abraham,isaac,Ishmael,katika historia iliyopita,na mwisho wake ukaangukia pale pale,kwenye kusudio lako la udini,uzanzibari,uisilamu,uarabu,pascal asili ya jina lako linatokana na utumwa wa wajerumani,waingerezi,waliojificha kutekeleza mbinu zao za kuwafanya watumwa,wazee wetu wa kiafrica,Pascal jaribu sana kuelezea uhalisia wa ushahidi tosha,sisemi hivi Kwa sababu ya kutetea ama waislamu au waarabu,lakini tujiulize kwa nini unakosa kuwaingiza washirki wakuu wa biashara ya utumwa Kwa tanganyika ,sababu wanagusa imani yako ??inaendelea
 
Mkuu Abua, kuna njia kuu 3 tuu za kupata maarifa kwa kujifunza
1. Kuwepo mwenyewe na kushuhudia
2. Kuhadithiwa au kufundishwa na wanaojua.
3. Kujisomea toka maandishi, filamu, simulizi etc hivyo kukuondoa ujinga na kukupatia ufahamu.

Biashara ya utumwa imefanywa kwa miaka mingi na mahali pengi. Mfano Waisrael walikaa utumwani Misri kwa muda wa miaka 400!.

Kwa upande wa biashara ya utumwa kwa bara la Africa imefanywa kwenye routes mbili kuu. Trans Atlantic Slave Trade iliyofanywa kutumia bahari ya Atlantic, watumwa walikamatwa kutoka nchi za West Africa, na kupelekwa bara la Ulaya, Marekani na America ya Kusini, wale watu weusi wote wa Latin America ni hadi America ya Kati ni watumwa kutoka Africa. Kule japo nako waliteswa ila waliachwa kuendelea kuzaliana. Biashara hiyo ilipopigwa marufuku, nchi za Marekani na Uingereza zikatoa fursa kwa watumwa wanaotaka kurejeshwa Africa warejee. Marekani ikatengeneza nchi inayoitwa Liberia na kuwarejesha watumwa kutoka Marekani. Na Uingereza ikafuatia ikatengeneza nchi ya Sierra Leone ikawarejesha watumwa huru wa Uingereza.

Route ya pili ni Indian Ocean Slave Trade ni biashara ya utumwa iliyoendeshwa kwenye bahari ya Hindi. Hawa ndio watumwa kutoka Afrika Mashariki. Soko kuu la watumwa lilikuwa Zanzibar. Biashara hii haikufanywa na wazungu bali ilifanywa na Waarabu, na watumwa hawa walipelekwa Arabuni na India. Watumwa hawa ndio mababu zetu na kiukweli waliteswa!. Kitu cha kwanza walipofika tuu, watumwa wote wanaume wali hasiwa!. Hivyo kizazi chote cha watumwa weusi wa Arabuni na India ni wazalia wa watumwa wanawake waliokuwa vijakazi tena kwa kupewa mimba kwa kubakwa au kuingiliwa kwa nguvu!.

Biashara hii ilipopigwa marufuku, hakukuwepo watumwa wowote wa kurudishwa Africa toka Arabuni na India, badala yake waliwafanyia genocide na kuwauwa wote waliotaka uhuru!.

Paskali
 
Nimesema kwamba wewe Ni mdini,sasa kidogo unakuja katika Imani yako na chuki za udini,maelezo yako yako katika kutetea imani yako na Ustashi wako ,zilizokuandama na kukufanya,ukubali Kuwa mtumwa wa Kuwatetea,wale wale waliowafanya watumwa mababu zetu,utumwa ulifanywa kwa jamii,hilo unaonesha uzaifu wako kutokana na imani yako,inayowapendelea wazungu,kwamba hawakuwafanya watu watumwa,afrika mashariki,huko Ni uzushi wa wazi,wajerumani na wazungu wengine waliwatesa na kuwafanya watumwa,Kama hufahamu kuna vita na wahehe na vita vya majimaji .
Mkuu Pascal ni lazima ujirekebishe,kama unataka kuungwa mkono, mzalendo wa kweli,anahukumu haki katika masuala na maandishi kwa faida ya wote,ukikataa kwamba wazungu hawakufanya watumwa,wazee wetu,huo si ukweli,wazungu,wamisionari/wakristo wamewafinyia wazee wetu ushenzi mkubwa,katika vita ya maji maji waliwauwa watanganyika zaidi ya laki mbili,kabla ya kusalimu amri,na mwisho wameondoka mali zetu nyingi na kutuachia dini,halo chini Ni moja ya mateso ya wajerumani kwa watumwa wao.
 
Nakupongeza mkuu. Kesha koma huyo harudii tena
 
Kwa kutumia tu akili ya kawaida na kwa kuangalia maisha ya leo tunavoish utakundua kuhusu tofaut ambayo bado ipo mpaka leo.....
Waarabu na Wahindi wapo radhi waoane ndugu ili mradi tu usio au kuolewa na Rangi nyeusi na ikitokea umeoa au kuolewa bas ujue unatengwa na familia. Hi inaonyesha tu jins gan hali ilivyo sasa pata picha enzi hizo ilikuaje.? Hapo ujaongelea mauaj na manyanyaso wanayofanyiwa ndugu zetu uko kwao....!

Pia Wazungu wenyewe ni wabaguzi wakubwa ata kwa Watu nyota weusi na mifano iko wazi tu, kutoka na kuendelea mapema ktk technologia basi kumekua na uahahid mkubwa na wawazi kuhusu waliowafanyia babu zetu...

Watu wasijenge hoja kwa misingi ya udini, kujifanya mfia dini apa, au mwarabu au mzungu akati uku uswahilin tunaishi wote, na tunaishi poa na tunashikiana kwenye raha na matatizo klko ata ao weupe wenu....

Akuna Mtu mweupe yoyote dunian mwenye nia njema na mtu mweusi, tena asa wanyonyaji wakizungu.....
 
Ndugu zangu,
Huu uzi tuliujadili kwa kirefu sana siku za nyuma sijui vipi tena
umerudishwa upya.

Hii picha hapo chini aliyoweka Paskali nilimweleza huko nyuma
kuwa haina uhusiano na utumwa ni picha ya Vita Vya Maji Maji
1905 - 1907.

 
dooh
Waarabu watu wabaya sana
 
Ndugu zangu,
Huu uzi tuliujadili kwa kirefu sana siku za nyuma sijui vipi tena
umerudishwa upya.

Hii picha hapo chini aliyoweka Paskali nilimweleza huko nyuma
kuwa haina uhusiano na utumwa ni picha ya Vita Vya Maji Maji
1905 - 1907.

Bwana Mohammed ,ikiwa hii Ni picha,tofauti na anayoeleza,kwa hiyo,kusudia lake haswa Ni upotoshajji
Ndugu zangu,
Huu uzi tuliujadili kwa kirefu sana siku za nyuma sijui vipi tena
umerudishwa upya.

Hii picha hapo chini aliyoweka Paskali nilimweleza huko nyuma
kuwa haina uhusiano na utumwa ni picha ya Vita Vya Maji Maji
1905 - 1907.

Bwana Mohammed,ahsante kwa kutusaidia,kuweka wazi upotoshaji wake.
 
Bwana Mohammed ,ikiwa hii Ni picha,tofauti na anayoeleza,kwa hiyo,kusudia lake haswa Ni upotoshajji

Bwana Mohammed,ahsante kwa kutusaidia,kuweka wazi upotoshaji wake.
Abuha,
Nimepata siku za nyuma kumshauri Pascal kuwa itakuwa vyema
kama angejituliza kabla ya kuandka.
 
Ndugu zangu,
Huu uzi tuliujadili kwa kirefu sana siku za nyuma sijui vipi tena
umerudishwa upya.

Hii picha hapo chini aliyoweka Paskali nilimweleza huko nyuma
kuwa haina uhusiano na utumwa ni picha ya Vita Vya Maji Maji
1905 - 1907.

Mzee wangu
Tatizi sio picha, nachokiona ni mtu kutete weupe kwa Misingi ya Dini na kutoa point ndogo ambazo kiualisia si kweli......

Ndo maana nkasema awa Wazungu au Warabu wote ni walewale tu, Wazungu wa leo ndo awa wanatunuonya, Waarabu wa leo ndo ao wanau Tembo na Faru wetu........

Ni wazi mtumwa ni mtumwa tu, mtumwa hana say, mtumwa atanyanyaswa, aatateswa na wapo watakao uawawa tu kwa kubisha au kutolewa kama mifano. Labda mtu aniambie kua Waarabu awajawai kifanya biashara ya utumwa kabisa... Ili hali Waarabu wapo Africa Masharik around karne ya 7......

Wote mko vizuri sana ila nawomba mtumie kalamu zenu vizuri kuleta umoja wa kitaifa, kuleta umoja na kumfumbua mtu mweusi apo alipokwamwa asogee mbele na si upotoshaji wa kugawanyiaha watu kwa misingi ya kidini na kufanya watu waendelee kua ma bwege mbele ya watu weupe
 

Ndugu zangu,
Kwa takriban miaka 144 utumwa ulikomeshwa Zanzibar.

Huyo Muarabu anaetafutwa Zanzibar hayupo.
Mchanganyiko wa damu ulikuwa mkubwa kupita kiasi.

Mifano tunayo mingi tena ya viongozi waliopigania uhuru wa
Zanzibar wenye damu mchanganyiko.

Yakuzungumzwa ikiwa tunatafuta hizo shida ni jela za mateso
zilizokujaanzishwa baada ya mapinduzi.

Kitu hiki kilikuwa hakijulikani kabla.
Jela hizi zilitesa na kuua watu wengi.

Sidhani kama katika karne hii propaganda ya utumwa inaweza
kufua dafu.

Hapo chini ni msaada mkubwa kwa wale wasiojua historia ya
Zanzibar:
1873 Treaty concerning Closure slave market Zanzibar and the slavetrade. Dhow chasing in Zanzibar waters by Sulivan Suppression of slavery in East Africa, Oman and Zanzibar.Slave ships. House of parliament.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…