Pascal,
Umeanza kwa kunishutumu kuwa nina chuki na Wamishionari.
Unanisingizia.
Lau kama una ushahidi wa chuki hizo tafadhali ulete hapa uonekane.
Kwa kuwa umeleta hili la chuki sina budi nami kukupa ushahidi wa kuaminika
wa chuki za hao wenye chuki katika nyoyo zao:
Wanamajlis, someni paragraph ya mwisho hapo juu kutoka kitabu cha
Padri
John Sivalon.
Mara kadhaa nimemuonya
Paschal kuwa afanye utafiti wa kutosha kabla ya
kuandika.
Kwanza kaweka picha ambazo nyingine ni za vita vya Maji Maji havina uhusiano
wowote na utumwa.
Hao hapo juu ni wapiganaji dhidi ya Wajerumani katika Vita Vya Maji Maji wakiwa
wamekamatwa.
Picha nyingine hazina, ''source,'' kwa hiyo msomaji hawezi kujua wapi zilikotoka.
Muhimu kwa
Paschal ajifunze na ajue historia ya utumwa ilikuwaje.
Utumwa uliofurtu ada ni ule wa Transatlantic Slave Trade na wa Wabelgiji Congo.
Akipenda anaweza kuingia hapa:
The Butcher of Congo
Paschal hawezi kujua lakini hiyo, ''report'' ya
Mackenzie si ngeni kwangu naijua siku
nyingi sana.
Mwaka wa 1991 nilikuwa Blantyre nje kidogo ya Glasgow hiki ni kijiji alichozaliwa
David Livingstone na kimenfanywa makumbusho yake kijiji kizima na nilifanya kipindi
na BBC Glasgow kuhusu
David Livingstone na Afrika.
''Report,'' mfano wa hii ya
Mackenzie zipo nyingi sana ila hakuna hata moja utaipitia
ukute Zanzibar watumwa wakinyongwa au kucharazwa viboko au kukatwa mikono
kama Marekani na Congo.
Si kama kama nasema kuna utumwa mwema la hasha ila hapa nia ni kueleza ule
ukweli wa hali halisi iliyokuwapo.
''Report,'' hizi nyingi zilizokuwa zikiandikwa na Wamishionari zilijazwa chumvi ili kutafuta
kupewa fedha kwa ajili ya shughuli zao za kiroho moja wapo ikiwa hiyo ya kukomesha
utumwa.
Katika ''report,'' ya
Mackenzie namuomba
Paschal aonyeshe mahali
aliposema kuwa Watumwa Zanzibar walibakwa,
walihasiwa na kuuawa kinyama kwa ushahidi madhubuti.
Bahati mbaya sana
Paschal anaandika kwa lugha ya kejeli na kuchanganya mambo mengi
yasiyokuwa na adabu wala ustaarabu.
Namsoma anapoandika kuhusu Waarabu Zanzibar na mengine ya uchaguzi.
Wanamajlis, nakuwekeeani hapa ujumbe niliopokea unaomuhusu
Paschal:
‘’…mwaka 1995 uchaguzi wa kwanza nchini kushiriki vyama vya upinzani kituo cha DTV
hivi sasa kinaitwa jina la Chanel Ten kilikua kikirusha matangazo mubashara hewani mimi
binafsi yangu na wenzangu tulikua nyumbani tunafatilia matangazo hayo mtangazaji wa
kituo hicho wakati huo alikua anaitwa
Paschal Mayala.
Mayala alikusanya matokeo ya vituo hivyo na kuenesha matokeo halisi ya nani mshindi wa
uchaguzi huo kati ya
Salmin Amour na
Seif Sharif Hamad.
Ally Amer aliihojiwa na
Paschal Mayala na kuoneshwa ushahidi.
Ali Ameir akasema yeye hayatambui matokeo hayo.
Akamwambia
Mayala, ‘’kijana hunitambui mimi?''
''Wewe endelea na hizo habari tu tutaonana.’’
DTV khatimae ikaingia matatani.
Baadae
Ally Ameir Mohamed akachaguliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani.’’
Paschal,
Unaweza kusema kitu kuhusu hayo hayo juu ikiwa utapenda.