Mkuu kwanza jifundishe kujibu hoja bila matusi kwani waswahili wansema ukimuona mtu ananza kujibu hoja kwa matusi ujue huyo kashindwa hoja,maana yake IQ ndogo..
Watu weusi wamezagaa kuanzia Arabuni,Iran,Uturuki,Pakistan,Palestina ..huweizi kuwaona kasababu media za nchi hizo haziwapi muonekano,watu wa weusi wanabaguliwa lakini wapo wengi tu..
Mfano Pakistani watu weusi walipelekwa kama watumwa wanaitwa
Sidi,hawa watu wengi wao wanapatikana Baluchistan,Oman kuna sehemu inaitwa
Salalla hii ni sehemu ya watu weusi waliopelekwa huko kama watumwa,Iran ukienda sehemu inaitwa Hormozagan utakuta watu weusi wengi walipelekwa huko kama watumwa,..
Kitu cha kushangaza hawa watu wenye asili ya Kiafrika walioko Iran,Pakistan wao moja kwa moja wanasema kuwa wao ni Wazanzibari,hawa wa Uturuki wao wanakwenda nyuma katika himaya ya Othman wa Uturuki "Othman Empire", wao wanasema walikuwa kama wanajeshi wa jeshi la Othmann...
View attachment 744872
watoto wairani wenye asili ya kiafrika
View attachment 744875
View attachment 744876
Waomani wenye asili ya Kiafrika
View attachment 744877
Wapakstani wenye asili ya kiafrika
View attachment 744878
wapalestinia wenye asili ya Kiafrika
View attachment 744880
Waturuki wenye asili ya watu wa afrika
Mkuu kabla hujaadika matusi,fanya utafiti kwanza...usizikubali sana propaganda za wazungu,nyengine ni uongo,..usiku mwema mkuu,ukitaka historia zaidi nitakupatia,kumbuka kuuliza sio ujinga..