‘Udikteta’ wa Magufuli na uhuru wa kujieleza

Vibendera hawataweza kukuelewa
Yaani Watanzania Wakitaka wajute wawape hawa Wapuuzi nchi
hakiyamungu watajuta
wao wenyewe wameshindwa kujiongoza nani watamuongoza
 
Wacha maCCM yaendelee kutawala tu. Maana elites ndio mawazo yao kama haya. Kama hawaoni (ma)tatizo kabisa, ni vipi wanaweza kuisaidia nchi yao kutoka hapa tulipo? Bado nafikiri kina Nyerere na timu yake wakati wa kutafuta uhuru....pamoja na elimu ndogo ya watu wengi...lakini wametuzidi pakubwa sana!

I can bet, ingalikuwa leo bado tunatawaliwa na uingereza kwa akili hizi za elites wetu, uhuru tungeusikia kwa wenzetu tu!
 
Kwa matakwa ya kipindi kile haukuwa udikteta . Na tulishavuka hizo nyakati so hatutakiwi kurudi huko.

Ila huyu ndugu yenu anataka kuturudisha nyuma.

Sent using Jamii Forums mobile app

Mataka ya nani?

Maana tulikuwa na vyama vingi, vikafutwa!

Vilipofutwa tukaingia mfumo mmoja!

Utawala wa mtu mmoja kwa zaidi ya miaka 20 si udikteta huo?
 
Wiki iliyopita serikali mpya ya Zimbabwe iliamua kufunga upatikanaji wa intaneti nchini humo kama malipizo ya maandamano ya watu kupinga upandaji wa bei ya mafuta.

Hapa Tanzania kuwekuwepo na kila aina ya lawama kwa utawala wa Rais Magufuli.

Rais Magufuli keshaitwa kila aina ya majina. Jina ambalo limekuwa likijirudia rudia ni ‘dikteta’.

Nikiri kuwa hata mimi mwanzoni mwanzoni mwa utawala wake kuna mambo sikuyapenda na niliutumia huo utambulisho wa ‘dikteta’ kuelezea kutopendezwa kwangu na baadhi ya mambo .

Lakini kwa kadri siku zinavyokwenda, yajiriyo hapa nchini na nje ya nchi, yananifanya nianze kujiuliza kama ni jambo sahihi kumwita Rais Magufuli dikteta.

Kuna watu humu mitandaoni wanapenda kulalamika kuwa eti Tanzania sasa hivi hakuna uhuru wa kutoa maoni na uhuru wa kujieleza.

Mara nyingi watu hawa hutoa malalamiko yao kupitia mitandao ya kijamii.

Sasa kilichotokea huko Zimbabwe wiki iliyopita kimenfanya nijiulize upya kuhusu huu udikteta wa Rais Magufuli.

Hivi ni lini hapa Tanzania tumewahi kufungiwa kabisa huduma ya intaneti kutokana na maandamano au sababu ingine yoyote ile?

Kilicho ironic ni kwamba hao wakosoaji wa Magufuli kuhusu uminywaji wa haki za kidemokrasia za kutoa maoni na kujieleza, hutumia intaneti kutoa maoni yao wakiwa hapa hapa nchini.

Huyu Magufuli ni dikteta gani anayeruhusu watu wamkosoe, kumpinga, na hata kumtukana huko kwenye mitandao ya kijamii lakini hachukui hatua kali za kuifungilia mbali intaneti kama alivyofanya Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe ambaye kaingia madarakani majuzi tu hapa?

Watanzania wakati mwingine huwa tunabweteka sana na uhuru tulionao!
Nashukuru mkuu kwa kuelewa hilo mapema
 
Achana na conspiracy theories.

Conspiracy theory?
1. Ben Saanane yuko wapi?
2. Kanguye yuko wapi?
3. Lissu je?
4. Zitto ana kesi ngapi
5. Lema alifungwa bila dhamana miezi minne kwa kauli wanasema ya uchochezi
6. Sugu alipigwa nyundo ya miezi mitano kwa kauli ya "uchochezi"
7. Kesi kibao za makosa ya mtandao
8. Bloggers wamewekewa fee ya kumiliki blog interms of millions
9. Ukiwa na Channel youtube lazima uisajili
10. Kuna sheria ya takwimu, imeharamisha kila takwimu isipokuwa zao
11. JF yenyewe hapa tulishapigwa pini almost miezi miwili tukakimbilia ukimbizini huko Kenya
12. Kuna sheria ya habari inang'ata kinyama
13. Sasa kuna muswada wa sheria ya vyama vya siasa unaokwenda kuvifanya vyama kuwa "client parties"
14. Harrasment ya magazeti, Katika utawala huu wameshafungia almost kila gazeti lililo vocal against matendo ya serikali hii!

Sasa katika mazingira kama hayo unataka mpaka Wakwambie kuwa hawataki "UWASEMESEME NA UKIWASEMASEMA WANATAFUTA NAMNA YA KUKUSHUGHULIKIA?"

Angalia mazingira wanayoyaweka ya kuminya uhuru wa habari/maoni ndo utajua kuwa situation ya kwetu ni mbaya kuliko Zimbabwe katika ishu hii ya freefom of speech, Sisi tunainstitutionalize uminywaji huu kwenye sheria, wakati Wazimbabwe wamefanya sporadically tu baada ya Maandamano makubwa ya kupinga hike ya bei ya mafuta
 
Wiki iliyopita serikali mpya ya Zimbabwe iliamua kufunga upatikanaji wa intaneti nchini humo kama malipizo ya maandamano ya watu kupinga upandaji wa bei ya mafuta.

Hapa Tanzania kuwekuwepo na kila aina ya lawama kwa utawala wa Rais Magufuli.

Rais Magufuli keshaitwa kila aina ya majina. Jina ambalo limekuwa likijirudia rudia ni ‘dikteta’.

Nikiri kuwa hata mimi mwanzoni mwanzoni mwa utawala wake kuna mambo sikuyapenda na niliutumia huo utambulisho wa ‘dikteta’ kuelezea kutopendezwa kwangu na baadhi ya mambo .

Lakini kwa kadri siku zinavyokwenda, yajiriyo hapa nchini na nje ya nchi, yananifanya nianze kujiuliza kama ni jambo sahihi kumwita Rais Magufuli dikteta.

Kuna watu humu mitandaoni wanapenda kulalamika kuwa eti Tanzania sasa hivi hakuna uhuru wa kutoa maoni na uhuru wa kujieleza.

Mara nyingi watu hawa hutoa malalamiko yao kupitia mitandao ya kijamii.

Sasa kilichotokea huko Zimbabwe wiki iliyopita kimenfanya nijiulize upya kuhusu huu udikteta wa Rais Magufuli.

Hivi ni lini hapa Tanzania tumewahi kufungiwa kabisa huduma ya intaneti kutokana na maandamano au sababu ingine yoyote ile?

Kilicho ironic ni kwamba hao wakosoaji wa Magufuli kuhusu uminywaji wa haki za kidemokrasia za kutoa maoni na kujieleza, hutumia intaneti kutoa maoni yao wakiwa hapa hapa nchini.

Huyu Magufuli ni dikteta gani anayeruhusu watu wamkosoe, kumpinga, na hata kumtukana huko kwenye mitandao ya kijamii lakini hachukui hatua kali za kuifungilia mbali intaneti kama alivyofanya Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe ambaye kaingia madarakani majuzi tu hapa?

Watanzania wakati mwingine huwa tunabweteka sana na uhuru tulionao!
Kwa maoni yako mtu mpaka akiifungia intaneti ndio awe dikteta!!?kuitwa kwake dikteta kunatia ndani mambo mengi tu sema kwasababu zako binafsi au kwa maslahi ya waliokutuma unajifanya una-challenge!ukiua watu kwa tuhuma za kisiasa,ukitamani mitandao ifungwe,ukibadilisha sheria ya takwimu na kuifanya serikali ndo mtoa takwimu,ukikosolewa tu hadharan ushamkamata mtu au pengine kupotezwa kabiswa!Huyu Melo c alivamiwa aliombwa taarifa za baadhi ya watu humu!!?na tungekuwa wote ni wakosoaji humu ndani JF ingeshafungiwa lakin kwasababu kuna watu wanashabikia watu humu kwa maslah yao kwasababu ni kanda ya ziwa mwenzao,ndio maana ina exist JF!!Kwahiyo we Nyani unaruhusiwa kumuona mzuri kwasababu hajafungia intanet!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hisani ya Michuzi Blog

MMILIKI WA JF AACHIWA HURU NA MAHAKAMA

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru Mkurugenzi Mtendaji wa mtandao wa Jamii Forums, Maxence Melo na Mwanahisa wa mtandao wa Jamii Forums, Micke William baada ya kuonekana hawana kesi ya kujibu.

Max na Micke wameachiwa huru leo mahakamani hapo na Hakimu Mkazi Godfrey Mwambapa baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi sita wa upande wa mashtaka na kuona kuwa ushahidi uĺiotolewa na mashahidi hao dhidi ya washtakiwa umeshindwa kuthibitisha mashtaka pasipo kuacha na kuongeza kuwa hauna mashiko.

Katika kesi hiyo namba 457 ya mwaka 2017 washtakiwa wanatuhumiwa kuwazuia Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi.

Kabla ya uamuzi huuo kutolewa leo, awali washtakiwa hao walisomewa maelezo ya awali na Wakili wa Serikali Mutalemwa Kishenyi ambae alidai Melo na William ni wamiliki na waanzilishi wa mtandao wa Jamii Media Co Ltd ambao umesajiliwa Brela Julai 2 mwaka 2008 na kupewa namba ya usajili 66333

Alidai baada ya usajili, hupatiwa taarifa za siri ambazo huwezesha mtu kuingia katika mtandao huo husika hivyo washtakiwa hao walikuwa na uwezo wa kuona taarifa kwenye mfumo wao.

Aidha katika maelezo hayo, Kishenyi alidai Mei 10 mwaka 2016, ZCO aliwaandika barua washtakiwa akiwafahamisha ofisi yake inafanya upelelezi kuhusu taarifa ya uongo dhidi ya Cusna Investment na Ocean Link iliyochapishwa na mwanachama wao Kwayu JF senior Expert member na Amrishipuri. ZCO pia aliwafahamisha kwa kifupi taarifa ambayo anaihitaji kutoka kwao na maelezo binafsi ya mtu aliyechapisha ili aweze kufanya upelelezi.

Alibainisha kuwa Mei 11mwaka 2016 mfanyakazi wa Jamii Media, Chrispin Mganyizi aliipokea na kuiwasilisha kwa washtakiwa lakini walikwamisha polisi kufanya upelelezi kwa kuficha taarifa za wanachama wao Kwayu JF senior Expert member na Amrishipuri.

Kishenyi alidai kuwa kufuatia jitihada hizo za ZCO za kuwataka washtakiwa kutoa taarifa muhimu na wao kukataa walikamatwa na kufikishwa mahakamani.
 
Wiki iliyopita serikali mpya ya Zimbabwe iliamua kufunga upatikanaji wa intaneti nchini humo kama malipizo ya maandamano ya watu kupinga upandaji wa bei ya mafuta.

Hapa Tanzania kuwekuwepo na kila aina ya lawama kwa utawala wa Rais Magufuli.

Rais Magufuli keshaitwa kila aina ya majina. Jina ambalo limekuwa likijirudia rudia ni ‘dikteta’.

Nikiri kuwa hata mimi mwanzoni mwanzoni mwa utawala wake kuna mambo sikuyapenda na niliutumia huo utambulisho wa ‘dikteta’ kuelezea kutopendezwa kwangu na baadhi ya mambo .

Lakini kwa kadri siku zinavyokwenda, yajiriyo hapa nchini na nje ya nchi, yananifanya nianze kujiuliza kama ni jambo sahihi kumwita Rais Magufuli dikteta.

Kuna watu humu mitandaoni wanapenda kulalamika kuwa eti Tanzania sasa hivi hakuna uhuru wa kutoa maoni na uhuru wa kujieleza.

Mara nyingi watu hawa hutoa malalamiko yao kupitia mitandao ya kijamii.

Sasa kilichotokea huko Zimbabwe wiki iliyopita kimenfanya nijiulize upya kuhusu huu udikteta wa Rais Magufuli.

Hivi ni lini hapa Tanzania tumewahi kufungiwa kabisa huduma ya intaneti kutokana na maandamano au sababu ingine yoyote ile?

Kilicho ironic ni kwamba hao wakosoaji wa Magufuli kuhusu uminywaji wa haki za kidemokrasia za kutoa maoni na kujieleza, hutumia intaneti kutoa maoni yao wakiwa hapa hapa nchini.

Huyu Magufuli ni dikteta gani anayeruhusu watu wamkosoe, kumpinga, na hata kumtukana huko kwenye mitandao ya kijamii lakini hachukui hatua kali za kuifungilia mbali intaneti kama alivyofanya Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe ambaye kaingia madarakani majuzi tu hapa?

Watanzania wakati mwingine huwa tunabweteka sana na uhuru tulionao!
1) Askofu NiweMugizi anatiliwa shaka uraia wake na amenyang'anywa Pasipoti yake karibu nusu mwaka sasa kwa kushiriki Kutamka kwamba "Tunahitaji katiba tena katiba nzuri".

2) Bwana Aidan Eyakuze wa TWAWEZA, baada ya kutoa takwimu zinazoonesha kushuka kwa umaarufu wa Magufuli, naye ametiliwa shaka uraia wake. Naye kanyang'anywa Pasipoti yake. Serikali inasema kwamba haijui lini itakamilisha "mchakato" wa kuverify uraia wa hao jamaa, maana uchunguzi unafanyika mpaka "nje ya nchi".

3) Azory Gwanda wa gazeti la Mwananchi "alipotezwa" baada ya kuwa anafanya uchunguzi kuhusu miili iliyokuwa inaonekana bichi.

4) Ben Saanane "alipotezwa" baada ya kuhoji PhD ya Magufuli.

5) Rais Magfuli amewahi kutoa kauli kwamba msemo wa "vyuma vimebana" ni jinai, anayesema hivyo anapingana na takwimu zinazoonesha uchumi unakua. Hivyo anayesema hivyo akamatwe kwa mujibu wa sheria ya takwimu.

6) Yeyote anayempinga Magufuli hadharani anashughulikiwa. wengi wamefunguliwa mashitaka na kufungwa kwa kutumia sheria ya mtandao, kwa kutoa kauli zisizompendeza Magufuli kwenye makundi ya WhatsApp.

7) Vyombo mbalimbali vya habari vimepigwa faini na kufungiwa, magazeti mengine yamefutwa kabisa sababu ya kuchapisha habari zinazomkosoa Rais Magufuli, mfano Channel Ten, Magic FM, STarTV, ITV nk. na magazeti kama MAWIO, MWANAHALISI, RAIA MWEMA, MWANANCHI, nk. magazeti yameisoma namba, na yanajaribu ku"balansi" kati ya kusifia na kukosoa kidoooogo sana. Pia magazeti hayapewi tena matangazo kutoka serikalini, hasa yale ambayo ni "kidomodomo".

8) Kuna mkazo mkubwa sana wa chini kwa chini unaowaandama wote wanaomkosoa Rais Magufuli. Unapomsifia unazawadiwa, unapomkosoa unaandamwa. Mwangalie Askofu Kakobe. aliwahi kutoa kauli kali sana dhidi ya Magufuli " Yeye ni nani? hata Mungu hawashughulikii wanaomkosoa au kumsema vibaya, na Mungu ana majeshi yenye nguvu kuliko mwanadamu yeyote" Kilichofuatia TRA walikwenda kufanya msako nyumbani kwake na kutoa taarifa za siri hadharani, na hata kudiriki kuchomekea kwamba Askofu Kakobe ameandika barua ya kuomba radhi kwa Magufuli, jambo ambalo Kakobe alilikanusha. Askofu Kakobe naye anachunguzwa uraia wake na Pasipoti yake imezuiliwa. Lakini sasa tunamwona Kakobe Mpya, ambaye sasa anaonekana akimwombea Magufuli katika hafla mbalimbali na kutoa maneno ya kuwakejeli "wanaomkosoa". Kakobe huyu "aliyeokoka upya" anadiriki kutamka yafuatayo:
"sio Vizuri kupinga kila kitu kana kwamba hakuna kilichofanyika. Kuna watu wakisikia Rais Magufuli anasifiwa masikio yao yanawasha... Tumemuita rais kwamba ni shujaa kwa sababu miaka mingi watu wamekuwa wanaimba nchi masikini.. Lakini Magufuli kasema nchi yetu ni tajiri na inaweza kugawa misaada. Naomba rais uendelee kuimba hivyo ili kila mtu aimbe nchi yetu ni tajiri....Katika maombi ninayokwenda kuomba namkabidhi rais katika mikono ya bwana na kufanya nchi hii iweze kuneemeka".

9)Rais Magufuli anapambana hata na Taasisi zilizopo kisheria ili kuisimamia Serikali. Upinzani - wamepewa likizo ya lazima wasifanye kazi hadi 2020, wana kesi kila mahali nchini. Wabunge wa Upinzani wanabanwa nje na ndani ya bunge. CAG, hapewi bajeti ya kutosha, na anadhalilishwa na kudhoofishwa asitimize majukumu yake vizuri. anatakiwa naye kujiunga na akina kakobe aanze kumsifia Mfalme ili mambo yaende vizuri. Tume ya Haki za Binadamu na utawala bora, ambayo ilipokuwa chini ya Jaji Amiri Manento iliwahi kuikosoa serikali na jeshi la Polisi kwa mauaji ya Daudi Mwangosi, inashindwa kufanya kazi zake vizuri kwa sababu kwa muda mrefu sasa haina viongozi wenye uwezo wa kufanya maamuzi. Waliostaafu hakuna walioteuliwa kuchukua nafasi zao. Hakuna Mwenyekiti Mtendaji, Hakuna Makamu Mwenyekiti, Hakuna Makamishna wa Tume, Hakuna Makamishna wasaidizi wa Tume, Hakuna Katibu Mtendaji. Tume hiyo haina uongozi toka Januari 2018, na mpaka sasa Rais Magufi haonekani kama ana hamu yoyote ya "kuiwasha" Tume hiyo. Soma hapa kwa waraka kutoka kwa Mtandao wa watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), uliosainiwa na Mratibu Onesmo Olengurumwa. Wameeleza kwamba kwa mujibu wa Katiba, Tume hiyo inasemwa kwamba ipo kisheria kama wakiwapo hao viongozi wa juu. kwa maana hiyo japo wapo watendaji wanaendelea na ajira zao, Tume haipo kisheria kwa sababu viongozi wote wa juu hawapo.

10) Kama Madikteta wote, Magufuli anapenda 100% kwenye kila kitu. Kama hauko tayari kumsifia, basi mpe nafasi ajisifie mwenyewe. Pale Nkrumah kwenye kongamano la kutathmini miaka mitatu ya uongozi wake, alitumia Saa nzima kujisifia mwenyewe. uenyekiti wa CCM alipata kura 100%, jambo ambalo siyo kawaida katika chaguzi za CCM. chaguzi zote ndogo, ukiacha tukio la kule Tunduma ambapo nafasi chache zilikwenda CHADEMA, na mkuu wa mkoa wa Mbeya aliomba radhi kwa "udhaifu" huo, chaguzi zote CCM inashinda 100%.

11) Hilo la Internet kutofungiwa na Magufuli, alitaka sana, maana aliwahi kutamka "Natamani malaika aifunge mitandao angalau kwa miaka mitatu tu". Kuna mahali tu kakwama, au washauri wake wamemdhibiti, au pengine atafungia kesho, huwezi jua. lakini anataka sana kuifunguia.

Nimejaribu kuorodhesha hayo, ni machache, yako mengi sana, ili kukubaliana na wale ambao wanasema HOJA YAKO NI MYOPIC. Maana yake hukutazama mbali.
 
1) Askofu NiweMugizi anatiliwa shaka uraia wake na amenyang'anywa Pasipoti yake karibu nusu mwaka sasa kwa kushiriki Kutamka kwamba "Tunahitaji katiba tena katiba nzuri".

2) Bwana Aidan Eyakuze wa TWAWEZA, baada ya kutoa takwimu zinazoonesha kushuka kwa umaarufu wa Magufuli, naye ametiliwa shaka uraia wake. Naye kanyang'anywa Pasipoti yake. Serikali inasema kwamba haijui lini itakamilisha "mchakato" wa kuverify uraia wa hao jamaa, maana uchunguzi unafanyika mpaka "nje ya nchi".

3) Azory Gwanda wa gazeti la Mwananchi "alipotezwa" baada ya kuwa anafanya uchunguzi kuhusu miili iliyokuwa inaonekana bichi.

4) Ben Saanane "alipotezwa" baada ya kuhoji PhD ya Magufuli.

5) Rais Magfuli amewahi kutoa kauli kwamba msemo wa "vyuma vimebana" ni jinai, anayesema hivyo anapingana na takwimu zinazoonesha uchumi unakua. Hivyo anayesema hivyo akamatwe kwa mujibu wa sheria ya takwimu.

6) Yeyote anayempinga Magufuli hadharani anashughulikiwa. wengi wamefunguliwa mashitaka na kufungwa kwa kutumia sheria ya mtandao, kwa kutoa kauli zisizompendeza Magufuli kwenye makundi ya WhatsApp.

7) Vyombo mbalimbali vya habari vimepigwa faini na kufungiwa, magazeti mengine yamefutwa kabisa sababu ya kuchapisha habari zinazomkosoa Rais Magufuli, mfano Channel Ten, Magic FM, STarTV, ITV nk. na magazeti kama MAWIO, MWANAHALISI, RAIA MWEMA, MWANANCHI, nk. magazeti yameisoma namba, na yanajaribu ku"balansi" kati ya kusifia na kukosoa kidoooogo sana. Pia magazeti hayapewi tena matangazo kutoka serikalini, hasa yale ambayo ni "kidomodomo".

8) Kuna mkazo mkubwa sana wa chini kwa chini unaowaandama wote wanaomkosoa Rais Magufuli. Unapomsifia unazawadiwa, unapomkosoa unaandamwa. Mwangalie Askofu Kakobe. aliwahi kutoa kauli kali sana dhidi ya Magufuli " Yeye ni nani? hata Mungu hawashughulikii wanaomkosoa au kumsema vibaya, na Mungu ana majeshi yenye nguvu kuliko mwanadamu yeyote" Kilichofuatia TRA walikwenda kufanya msako nyumbani kwake na kutoa taarifa za siri hadharani, na hata kudiriki kuchomekea kwamba Askofu Kakobe ameandika barua ya kuomba radhi kwa Magufuli, jambo ambalo Kakobe alilikanusha. Askofu Kakobe naye anachunguzwa uraia wake na Pasipoti yake imezuiliwa. Lakini sasa tunamwona Kakobe Mpya, ambaye sasa anaonekana akimwombea Magufuli katika hafla mbalimbali na kutoa maneno ya kuwakejeli "wanaomkosoa". Kakobe huyu "aliyeokoka upya" anadiriki kutamka yafuatayo:
"sio Vizuri kupinga kila kitu kana kwamba hakuna kilichofanyika. Kuna watu wakisikia Rais Magufuli anasifiwa masikio yao yanawasha... Tumemuita rais kwamba ni shujaa kwa sababu miaka mingi watu wamekuwa wanaimba nchi masikini.. Lakini Magufuli kasema nchi yetu ni tajiri na inaweza kugawa misaada. Naomba rais uendelee kuimba hivyo ili kila mtu aimbe nchi yetu ni tajiri....Katika maombi ninayokwenda kuomba namkabidhi rais katika mikono ya bwana na kufanya nchi hii iweze kuneemeka".

9)Rais Magufuli anapambana hata na Taasisi zilizopo kisheria ili kuisimamia Serikali. Upinzani - wamepewa likizo ya lazima wasifanye kazi hadi 2020, wana kesi kila mahali nchini. Wabunge wa Upinzani wanabanwa nje na ndani ya bunge. CAG, hapewi bajeti ya kutosha, na anadhalilishwa na kudhoofishwa asitimize majukumu yake vizuri. anatakiwa naye kujiunga na akina kakobe aanze kumsifia Mfalme ili mambo yaende vizuri. Tume ya Haki za Binadamu na utawala bora, ambayo ilipokuwa chini ya Jaji Amiri Manento iliwahi kuikosoa serikali na jeshi la Polisi kwa mauaji ya Daudi Mwangosi, inashindwa kufanya kazi zake vizuri kwa sababu kwa muda mrefu sasa haina viongozi wenye uwezo wa kufanya maamuzi. hiyo ni mbinu ya kuifanya ofisi hiyo ikose meno.

Hayo yote ndo mara yake ya kwanza kutokea hapa nchini chini ya utawala wa Magufuli?
 
Conspiracy theory?
1. Ben Saanane yuko wapi?
2. Kanguye yuko wapi?
3. Lissu je?
4. Zitto ana kesi ngapi
5. Lema alifungwa bila dhamana miezi minne kwa kauli wanasema ya uchochezi
6. Sugu alipigwa nyundo ya miezi mitano kwa kauli ya "uchochezi"
7. Kesi kibao za makosa ya mtandao
8. Bloggers wamewekewa fee ya kumiliki blog interms of millions
9. Ukiwa na Channel youtube lazima uisajili
10. Kuna sheria ya takwimu, imeharamisha kila takwimu isipokuwa zao
11. JF yenyewe hapa tulishapigwa pini almost miezi miwili tukakimbilia ukimbizini huko Kenya
12. Kuna sheria ya habari inang'ata kinyama
13. Sasa kuna muswada wa sheria ya vyama vya siasa unaokwenda kuvifanya vyama kuwa "client parties"
14. Harrasment ya magazeti, Katika utawala huu wameshafungia almost kila gazeti lililo vocal against matendo ya serikali hii!

Sasa katika mazingira kama hayo unataka mpaka Wakwambie kuwa hawataki "UWASEMESEME NA UKIWASEMASEMA WANATAFUTA NAMNA YA KUKUSHUGHULIKIA?"

Angalia mazingira wanayoyaweka ya kuminya uhuru wa habari/maoni ndo utajua kuwa situation ya kwetu ni mbaya kuliko Zimbabwe katika ishu hii ya freefom of speech, Sisi tunainstitutionalize uminywaji juu keenye sheria, wakati Wazimbabwe wamefanya sporadically tu baada ya Maandamano makubwa ya kupinga hike ya bei ya mafuta

Kwa hiyo hayo ndo yanamfanya Magufuli awe dikteta?
 
1) Askofu NiweMugizi anatiliwa shaka uraia wake na amenyang'anywa Pasipoti yake karibu nusu mwaka sasa kwa kushiriki Kutamka kwamba "Tunahitaji katiba tena katiba nzuri".

2) Bwana Aidan Eyakuze wa TWAWEZA, baada ya kutoa takwimu zinazoonesha kushuka kwa umaarufu wa Magufuli, naye ametiliwa shaka uraia wake. Naye kanyang'anywa Pasipoti yake. Serikali inasema kwamba haijui lini itakamilisha "mchakato" wa kuverify uraia wa hao jamaa, maana uchunguzi unafanyika mpaka "nje ya nchi".

3) Azory Gwanda wa gazeti la Mwananchi "alipotezwa" baada ya kuwa anafanya uchunguzi kuhusu miili iliyokuwa inaonekana bichi.

4) Ben Saanane "alipotezwa" baada ya kuhoji PhD ya Magufuli.

5) Rais Magfuli amewahi kutoa kauli kwamba msemo wa "vyuma vimebana" ni jinai, anayesema hivyo anapingana na takwimu zinazoonesha uchumi unakua. Hivyo anayesema hivyo akamatwe kwa mujibu wa sheria ya takwimu.

6) Yeyote anayempinga Magufuli hadharani anashughulikiwa. wengi wamefunguliwa mashitaka na kufungwa kwa kutumia sheria ya mtandao, kwa kutoa kauli zisizompendeza Magufuli kwenye makundi ya WhatsApp.

7) Vyombo mbalimbali vya habari vimepigwa faini na kufungiwa, magazeti mengine yamefutwa kabisa sababu ya kuchapisha habari zinazomkosoa Rais Magufuli, mfano Channel Ten, Magic FM, STarTV, ITV nk. na magazeti kama MAWIO, MWANAHALISI, RAIA MWEMA, MWANANCHI, nk. magazeti yameisoma namba, na yanajaribu ku"balansi" kati ya kusifia na kukosoa kidoooogo sana. Pia magazeti hayapewi tena matangazo kutoka serikalini, hasa yale ambayo ni "kidomodomo".

8) Kuna mkazo mkubwa sana wa chini kwa chini unaowaandama wote wanaomkosoa Rais Magufuli. Unapomsifia unazawadiwa, unapomkosoa unaandamwa. Mwangalie Askofu Kakobe. aliwahi kutoa kauli kali sana dhidi ya Magufuli " Yeye ni nani? hata Mungu hawashughulikii wanaomkosoa au kumsema vibaya, na Mungu ana majeshi yenye nguvu kuliko mwanadamu yeyote" Kilichofuatia TRA walikwenda kufanya msako nyumbani kwake na kutoa taarifa za siri hadharani, na hata kudiriki kuchomekea kwamba Askofu Kakobe ameandika barua ya kuomba radhi kwa Magufuli, jambo ambalo Kakobe alilikanusha. Askofu Kakobe naye anachunguzwa uraia wake na Pasipoti yake imezuiliwa. Lakini sasa tunamwona Kakobe Mpya, ambaye sasa anaonekana akimwombea Magufuli katika hafla mbalimbali na kutoa maneno ya kuwakejeli "wanaomkosoa". Kakobe huyu "aliyeokoka upya" anadiriki kutamka yafuatayo:
"sio Vizuri kupinga kila kitu kana kwamba hakuna kilichofanyika. Kuna watu wakisikia Rais Magufuli anasifiwa masikio yao yanawasha... Tumemuita rais kwamba ni shujaa kwa sababu miaka mingi watu wamekuwa wanaimba nchi masikini.. Lakini Magufuli kasema nchi yetu ni tajiri na inaweza kugawa misaada. Naomba rais uendelee kuimba hivyo ili kila mtu aimbe nchi yetu ni tajiri....Katika maombi ninayokwenda kuomba namkabidhi rais katika mikono ya bwana na kufanya nchi hii iweze kuneemeka".

9)Rais Magufuli anapambana hata na Taasisi zilizopo kisheria ili kuisimamia Serikali. Upinzani - wamepewa likizo ya lazima wasifanye kazi hadi 2020, wana kesi kila mahali nchini. Wabunge wa Upinzani wanabanwa nje na ndani ya bunge. CAG, hapewi bajeti ya kutosha, na anadhalilishwa na kudhoofishwa asitimize majukumu yake vizuri. anatakiwa naye kujiunga na akina kakobe aanze kumsifia Mfalme ili mambo yaende vizuri. Tume ya Haki za Binadamu na utawala bora, ambayo ilipokuwa chini ya Jaji Amiri Manento iliwahi kuikosoa serikali na jeshi la Polisi kwa mauaji ya Daudi Mwangosi, inashindwa kufanya kazi zake vizuri kwa sababu kwa muda mrefu sasa haina viongozi wenye uwezo wa kufanya maamuzi. hiyo ni mbinu ya kuifanya ofisi hiyo ikose meno.

10) Kama Madikteta wote, Magufuli anapenda 100% kwenye kila kitu. Kama hauko tayari kumsifia, basi mpe nafasi ajisifie mwenyewe. Pale Nkrumah kwenye kongamano la kutathmini miaka mitatu ya uongozi wake, alitumia Saa nzima kujisifia mwenyewe. uenyekiti wa CCM alipata kura 100%, jambo ambalo siyo kawaida katika chaguzi za CCM. chaguzi zote ndogo, ukiacha tukio la kule Tunduma ambapo nafasi chache zilikwenda CHADEMA, na mkuu wa mkoa wa Mbeya aliomba radhi kwa "udhaifu" huo, chaguzi zote CCM inashinda 100%.

11) Hilo la Internet kutofungiwa na Magufuli, alitaka sana, maana aliwahi kutamka "Natamani malaika aifunge mitandao angalau kwa miaka mitatu tu". Kuna mahali tu kakwama, au washauri wake wamemdhibiti, au pengine atafungia kesho, huwezi jua. lakini anataka sana kuifunguia.

Nimejaribu kuorodhesha hayo, ni machache, yako mengi sana, ili kukubaliana na wale ambao wanasema HOJA YAKO NI MYOPIC. Maana yake hukutazama mbali.

Dah!, Mkuu Umemaliza kila kitu, kwa jinsi ulivyoanalyze hii issue sidhani kama ataleta mada nyingine inayosukumwa na "hisia" zaidi kuliko "uhalisia" kama hii!!
 
Back
Top Bottom