‘Udikteta’ wa Magufuli na uhuru wa kujieleza

History huandikwa na mshindi ... anaweza kuipaka rangi ili iweze kumfanya atukuzwe .. halafu akatoa maagizo ipitishwe katika mitaala ya elimu nchini ,,.kisha ikafanikiwa kuwa brainwashed vijana wote wa taifa husika ambao ndio taifa la kesho .... hicho ndio alicho kifanya mchonga .... kisikuzubaishe sana akili yako
Sasa kama Nyerere alikuwa dikteta mbona yuko revered sana, ndani na nje ya Tanzania?

Hata wapinzani wa Tanzania kwa heshima humwita Baba wa Taifa!

Dikteta gani huyo anayeheshimika kihivyo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bora azime internet kuliko kupiga watu risasi ,kuteka,kuua n.k
Sio lazima afanye unavyotaka eti azime data yeye ameona ubabe wa live ndio dawa.
 
Naona leo umeshiba maharage ya iringa
Hakuna hoja hapo ni ujinga, wewe kufanananisha matumizi ya mitandao na Uhuru wa kutoa maoni. Hivi unajua kuna uhuru wa kukutana? Sasa kwenye mitandao wanakutana? Wanafanya mikutano au? Acha kujipumbuza na ujinga wako. Huna hoja, hata kwenye orodha wa great thinker wewe hautakuja kuwamo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wiki iliyopita serikali mpya ya Zimbabwe iliamua kufunga upatikanaji wa intaneti nchini humo kama malipizo ya maandamano ya watu kupinga upandaji wa bei ya mafuta.

Hapa Tanzania kuwekuwepo na kila aina ya lawama kwa utawala wa Rais Magufuli.

Rais Magufuli keshaitwa kila aina ya majina. Jina ambalo limekuwa likijirudia rudia ni ‘dikteta’.

Nikiri kuwa hata mimi mwanzoni mwanzoni mwa utawala wake kuna mambo sikuyapenda na niliutumia huo utambulisho wa ‘dikteta’ kuelezea kutopendezwa kwangu na baadhi ya mambo .

Lakini kwa kadri siku zinavyokwenda, yajiriyo hapa nchini na nje ya nchi, yananifanya nianze kujiuliza kama ni jambo sahihi kumwita Rais Magufuli dikteta.

Kuna watu humu mitandaoni wanapenda kulalamika kuwa eti Tanzania sasa hivi hakuna uhuru wa kutoa maoni na uhuru wa kujieleza.

Mara nyingi watu hawa hutoa malalamiko yao kupitia mitandao ya kijamii.

Sasa kilichotokea huko Zimbabwe wiki iliyopita kimenfanya nijiulize upya kuhusu huu udikteta wa Rais Magufuli.

Hivi ni lini hapa Tanzania tumewahi kufungiwa kabisa huduma ya intaneti kutokana na maandamano au sababu ingine yoyote ile?

Kilicho ironic ni kwamba hao wakosoaji wa Magufuli kuhusu uminywaji wa haki za kidemokrasia za kutoa maoni na kujieleza, hutumia intaneti kutoa maoni yao wakiwa hapa hapa nchini.

Huyu Magufuli ni dikteta gani anayeruhusu watu wamkosoe, kumpinga, na hata kumtukana huko kwenye mitandao ya kijamii lakini hachukui hatua kali za kuifungilia mbali intaneti kama alivyofanya Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe ambaye kaingia madarakani majuzi tu hapa?

Watanzania wakati mwingine huwa tunabweteka sana na uhuru tulionao!
mkuu

@maxencemelo kila siku wanamsumbua..kesi kibao wanataka atoe utambulisho wetu..juzi tuu huko songwe jamaa wa chadema kadakwa na kaletwa dsm kimya kimya kisa page ya kwinyara....na mengine mengi

unataka mifano zaidi???????
 
Usome vizuri huo mswaada then uone kama ana nia njema ya kukuza demokrasia nchini kisha tuambie ni sheria ipi inazuia shughuli za kisiasa nchini?
 
Wiki iliyopita serikali mpya ya Zimbabwe iliamua kufunga upatikanaji wa intaneti nchini humo kama malipizo ya maandamano ya watu kupinga upandaji wa bei ya mafuta.

Hapa Tanzania kuwekuwepo na kila aina ya lawama kwa utawala wa Rais Magufuli.

Rais Magufuli keshaitwa kila aina ya majina. Jina ambalo limekuwa likijirudia rudia ni ‘dikteta’.

Nikiri kuwa hata mimi mwanzoni mwanzoni mwa utawala wake kuna mambo sikuyapenda na niliutumia huo utambulisho wa ‘dikteta’ kuelezea kutopendezwa kwangu na baadhi ya mambo .

Lakini kwa kadri siku zinavyokwenda, yajiriyo hapa nchini na nje ya nchi, yananifanya nianze kujiuliza kama ni jambo sahihi kumwita Rais Magufuli dikteta.

Kuna watu humu mitandaoni wanapenda kulalamika kuwa eti Tanzania sasa hivi hakuna uhuru wa kutoa maoni na uhuru wa kujieleza.

Mara nyingi watu hawa hutoa malalamiko yao kupitia mitandao ya kijamii.

Sasa kilichotokea huko Zimbabwe wiki iliyopita kimenfanya nijiulize upya kuhusu huu udikteta wa Rais Magufuli.

Hivi ni lini hapa Tanzania tumewahi kufungiwa kabisa huduma ya intaneti kutokana na maandamano au sababu ingine yoyote ile?

Kilicho ironic ni kwamba hao wakosoaji wa Magufuli kuhusu uminywaji wa haki za kidemokrasia za kutoa maoni na kujieleza, hutumia intaneti kutoa maoni yao wakiwa hapa hapa nchini.

Huyu Magufuli ni dikteta gani anayeruhusu watu wamkosoe, kumpinga, na hata kumtukana huko kwenye mitandao ya kijamii lakini hachukui hatua kali za kuifungilia mbali intaneti kama alivyofanya Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe ambaye kaingia madarakani majuzi tu hapa?

Watanzania wakati mwingine huwa tunabweteka sana na uhuru tulionao!
japo sijasoma mpaka mwisho nilishia pale uliposema eti.... kwa taarifa tu ni kwamba uhuru wa kutoa maoni haupo... hata wewe jina unalotunia sio lako yapo wapi magazeti haya ''' MWAIO NA MWANAHALISI?
 
Kwa hiyo wewe ndugu, endapo utafungiwa "intaneti" tu, ndipo utathibitisha huyu bwana ni dikteta??????

aseee!!!
 
Sidhani kama watanzania wanoatumia mitandao kisawasawa wanafikia milioni. Huku Jf idadi inakaribia tu laki tano na wengi hawaingii. watanzania wako milioni 50+. mtu akifikiri anaweza asione sababu ya kuzuia mitandao akazuia maandamano na mikutano!
 
japo sijasoma mpaka mwisho nilishia pale uliposema eti.... kwa taarifa tu ni kwamba uhuru wa kutoa maoni haupo... hata wewe jina unalotunia sio lako yapo wapi magazeti haya ''' MWAIO NA MWANAHALISI?

Jina ninalotumia hapa nimelichagua mwenyewe.

Nina hiyari ya kutumia jina langu la serikali pia.

So what’s your point?
 
Back
Top Bottom