Udini: Mwalimu Mkuu na wanafunzi wa Kikristo wakimbia shule Bagamoyo kuhofia maisha

Status
Not open for further replies.


“Kama kweli Mkuu wa Shule amekimbia shuleni atakuwa amefanya vizuri kwa sababu alikuwa hatakiwi na wanafunzi,” alisema Mbaga ambaye hata hivyo, hakutaka kufafanua zaidi chanzo cha mgogoro huo.

Dah!! Huyo ndiyo kamanda wa Polisi anayeongea hayo!!!
 
Nchi inaelekea kubaya sana, vita hii ya kidini sasa itaanza kupiganwa kimya kimya ndani ya nyumba mlizopanga, ndani ya mashule, masokoni nk, huko sio Polisi wala JWTZ watakaoweza kupiga mabomu, JK and CCM hamkwepi laana hii.
 
huku tunakokwenda sasa naona itakua wanafunzi wa kikristo wana shule zao na waislam wana shule zao itakua vigumu kuwaweka shule moja...kazi ipo...
 
Mkuu kile chumba Bado Kipo pale kama msikiti....Juhudi kubwa zimefanywa na baadhi ya walimu Kuwanyang'nya waislamu Kile chumba.....
Mimi mwenyewe nilimla mitama Ticha mmoja aliengia na viatu katika kile chumba...
Mzee Kwayu alikuwa Mtu mzuri sana alikuwa hana matatizo yoyote ila kuna Vidampa vina chukiza ajabu sana
 
Kweli kabisa mkuu, leo ndiyo tunasituka juu ya mambo haya.

Tunaanza kusituka kutokana na kukosa siasa bora za kuongoza nchi kama wamoja.
Mshikamano hakuna tena au ndio unazidi kutetereka.

Nimepita hapo Bagamoyo mara nyingi, na najua huo msikiti upo siku nyingi sana, we took ourselves for gtranted.
Leo vijana/walimu wanafarakana kutokana na udini.
Walimu/wanafunzi wanafikia hatua ya kukimbia academic campuses kutokana na mifarakano ya kidini.

Sasa ndo tunatatambua kuwa ile amani tuliyodhani tunayo kumbe sisi wenyewe ndio kuni za moto unaokuja.

Msikiti au Kanisa NDANI ya serikali ilikuwa kitu positive kwa miaka mingi,lakini leo ni source of conflict.

Inabidi tusali sana, kama hatujajua ni wapi tumepotoka.
La sivyo laana ya makosa tuliyofanya itatuhukumu kwa maka mingi ijayo.
 


Nimesoma Tosamaganga Sekondary, kuna Kanisa zuri sana katikati ya Shule na wala halijawahi kuwa tatizo. Nachojua ni kuwa ikiwa shule ilitaifishwa kutoka ktk taasisi ya kidini basi wasingetaifisha hadi imani za waliokuwepo kwa maana kubadili kanisa au msikiti kuwa darasa au ukumbi wa mikutan au starehe. Ikiwa tunaaimini kuwa lengo la Dini ni Amani na utulivu basi hapo shida hamna. Labda kama Kanisa hilo au msikiti umejengwa na Serikali wakati wa ujenzi wa shule au baada. Na huo msikiti unaonekana ni mkongwe sana. Hivyo ulikuwepo toka kitambo.
 
Liko wapi tatizo la Msikiti ndani ya Shule ya Bagamoyo? Nani asiyejua kwamba PUGU SEKONDARI kuna kanisa kubwa la Roma? Mbona MARA Sekondari kuna Kanisa Kubwa la ROMA lakini hakuna Msikiti? Je umeshawahi kusikia mgogoro toka katika Shule hizi za Serikali.
MISIKITI na MAKANISA kwenye Shule za Sekondari wala si tatizo...Tatizo ni sisi tunaotumia muda wetu vibaya kwa kuzungumzia juu ya vitu hivyo bila ya kufanya tafiti za kutosha na kujiridhisha juu ya kile tunachokizungumza.
TAFAKARI.
 
wanaoandika habari kuhusu udini wawe makini sana. hata sisi tuaochangia humu tuwe makini ama sivyo tunaweza kuwa tunachochea moto katika tanuru la udini. madhara yake yatakuwa kwetu sote waliomo na wasiokuwepo.
 
Masyopakindi wa Magamba anaendelea kuchochea udini JF!
 
Mnanikumbusha kisanga cha shule ya sekondari ya Ndanda kule Mtwara!
 
ni vizuri majengo ya ibada yajengwe karibu na shule...kwa dunia hii ya leo wanafunzi wetu wanahitaji sana kumjua Mungu iwe ni dini yoyote ile
 

Huo ndio ujinga wa Waislamu wengi, wanaamini wao wanaujua Ukristo kuliko Wakristo wenyewe lakini papo hapo wanamkashifu huyo Yesu anayeaminiwa na Wakristo. Chakushangaza, Mkristo au mwingine akizungumzia Uislamu au Muhammad kinyume na wanavyoamini basi ni vita na vurugu na kuharibu mali za Wakristo.

Najiuliza; kama Wakristo wangekuwa na tabia kama Waislamu hali ingekuwaje?
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…