tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,040
Kwa wale waliosoma ama waliowahi kufika Chuo kikuu cha Dodoma, hasa college ya social na Humanities, utaona wamama wengi na wazee wanazagaa kwenye milango cha cafeteria wakiwa na watoto wadogo wakiomba hela kwa wanafunzi. Shida ni wale watoto wanaokuwa nao kwamba hawasomi? maana ni watoto wadogo tena wengi wao ni mabinti pia je, wazazi wao wanataarifa kuwa watoto wao wanakuja kwenye kampasi na wale wamama wanaoomba omba?
Alafu kuna vikundi vya watoto hasa wa kiume [miaka 8 hadi 12] wanazagaa kwenye kamapasi wakiomba hela kwa wanafunzi au kununuliwa chakula. Ukiwasikiliza utawasikia hawana wazazi, mara wazazi wamesafiri, mara nyumbani hawajapika chakula na wengine wanageuka kuwa watumwa wa wanafunzi. Wanawafuatia chakula wanafunzi na kuwapelekea kwenye hosteli zao huku wakiambulia chakula au pesa.
Wale watoto ni wadogo, kwa umri ule wanapaswa kuwa shuleni, na kama ni kweli hawana wazazi uongozi wa chuo umechukua hatua gani?
Soma pia: UDOM ni chuo chenye kozi nyingi za ajabu ajabu na kimetumika kuwaharibia vijana wengi future zao, sasa wameanza kujishtukia!