UDOM hao omba omba ndani ya chuo na Watoto wadogo wanaozagaa kwenye cafeteria hatuwaelewi, liangalieni hili

UDOM hao omba omba ndani ya chuo na Watoto wadogo wanaozagaa kwenye cafeteria hatuwaelewi, liangalieni hili

UDOM ni takataka mkuu

Huwezi kufananisha gamba la UDSM na la UDOM hata siku moja kaka
​
Sawa mkuu lkn nafasi ya BCOM ACCOUNTING ya udsm ikitangazwa wote mnaombwa na kukandwa wote wanakandwa udism wana fail pia mimi nazan ni kichwa cha mtu juhudi na kujituma kwenye career yako.
 
Nimeshangaa na mie, eti kila mtu ana access ya kuingia maeneo ya chuo. Lol
Vitani pekee ndio Kila MTU awezi akawa na access ya kuingia.
Vyuo ni huduma ya kijamii tena inabidi iishi vizuri sana na jamii zinazoizunguruka chuo.
Chuo kinapaswa kufanya vitu vya kuinua jamii na si kuwa chanzo cha kunyanyapaa jamii.
Kama wewe ulisoma chuo ambacho akitengamani na jamii umekosa mafundisho mengi sana ya upendo.
Kifupi wewe ulikuwa vitani sio chuoni.
 
Ukisoma comments nyingi za wadau utapata picha kwamba watanzania sisi ni watu wa aina gani
 
Umeongea point kubwa sana japo naamini kuna baadhi ya wengine wenye Akili mgando na mitizamo tofauti hasa kuna wale ninaowachukia sana wenye dhana ya “wewe zaa watoto analea Mungu.” Ndiyo hawatakuelewa kabisa.

Ni aibu kubwa sana ya kitaifa kwasababu UDOM haitoi huduma kwa wazawa tu. Kuna wakati nawaza hata kwa hili pia la Mji Mkuu bado Serikali itahitaji kusaidiwa na wananchi huku wananchi haohao wakitarajia msaada kulihusu kutoka serikalini.
 
Kwa wale waliosoma ama waliowahi kufika Chuo kikuu cha Dodoma, hasa college ya social na Humanities, utaona wamama wengi na wazee wanazagaa kwenye milango cha cafeteria wakiwa na watoto wadogo wakiomba hela kwa wanafunzi. Shida ni wale watoto wanaokuwa nao kwamba hawasomi? maana ni watoto wadogo tena wengi wao ni mabinti pia je, wazazi wao wanataarifa kuwa watoto wao wanakuja kwenye kampasi na wale wamama wanaoomba omba?



Alafu kuna vikundi vya watoto hasa wa kiume [miaka 8 hadi 12] wanazagaa kwenye kamapasi wakiomba hela kwa wanafunzi au kununuliwa chakula. Ukiwasikiliza utawasikia hawana wazazi, mara wazazi wamesafiri, mara nyumbani hawajapika chakula na wengine wanageuka kuwa watumwa wa wanafunzi. Wanawafuatia chakula wanafunzi na kuwapelekea kwenye hosteli zao huku wakiambulia chakula au pesa.



Wale watoto ni wadogo, kwa umri ule wanapaswa kuwa shuleni, na kama ni kweli hawana wazazi uongozi wa chuo umechukua hatua gani?



Soma pia: UDOM ni chuo chenye kozi nyingi za ajabu a
 
Back
Top Bottom