Je, ni kweli Wanasiasa Wanafanya PhD kama Wengine?
Nataka nishee mawazo yangu kuhusu Doctor Jafo S.S. kujipatia PhD. ndani ya muda. Kabla ya hapo niseme kwanza haya maneno yanayofuata.
Nimekumbuka wanasiasa wachache waliojipatia PhDs wakiwa mawaziri au vyeo vingine serikalini: Dr. Magufuli J.P.J., Dr. Nchemba, M.L., Dr. Biteko, M.D., et al.
Nianze kwa kukumbusha kwamba kusoma PhD ni kugumu sana, nadhani mtakubaliana nami. Kuanza kuandaa proposal, ifikie viwango vya kuridhisha supavaiza, idara na chuo. Aandae study design iliyonyooka ili apate kibali cha utafiti kutoka chuoni.
Siyo tu kibali, bali ukusanyaji data na uchakataji wake ili ulete maana na matokeo tarajiwa au kinyume.
Baada ya hapo kuna zile progress ambazo mara urudi field, mara udizaini upya study, mara ubadilishe objectives, n.k.
Wakati wote huo ukimeinteini constant communications/meeting with supervisors. Huku ukijitahidi kupablishi kwenye predator journals na conferences ili utimize vigezo vya chuo husika.
Hili tunaliona kwa career academicians ni GUMU sana sana wakati hawana kazi nyingine zaidi ya kusoma tu ili wapate hiyo PhD. Wengine hadi wanafikia kushindwa kumaliza PhD na kulazimika kubadilishia kada ya kazi (au kufukuzwa hapo zamani).
Sasa tujiulize, mtu ni waziri, ana majukumu kede kede nchi nzima. Anazunguka na raisi au waziri mkuu au makamu wa raisi. Wakati huo huo anakimbizana na dharura zinazojitokeza wizarani na nchini pote. Je, mtu huyu anapata wapi muda wa kufanya yote ya hapo juu ili apate PhD?
Najiuliza na sidhani kama nitaweza kujijibu NAOMBA mnisaidie. Hawa wanasiasa wanapataje PhD kirahisirahisi wakati career academicians wanashindwa?
Nafikiri jibu likipatikana litasaidia wengine wengi waweza kufanikisha jambo hili.
Nitoe mifano miwili tu midogo. Nina wanafunzi wa MSc. Eng. wawili. Wanafanya kazi. Imekuwa taabu sana kupata progress ninayoitegemea kwao kutokana na majukumu ya kazini. Kumbuka hawa wanafanya kazi kitengo kimoja tu na siyo nchi nzima. Ninaye mwingine wa PhD., yeye hata proposal bado hajaweza kuikamilisha na mwaka unaisha. Kwanini? Ametingwa na majukumu ya kazini.
Iweje leo mtu anazunguka Tanzania nzima, yupo bungeni, anaenda nchi za nje, ana majukumu lukuki ya kitaifa. Anawezaje kumaliza PhD kwa haraka hivyo?
Nijibuni ili niwasaidie wanafunzi wangu jamani wamalize haraka kwa muda. Sababu kama waziri anaweza kwanini wao washindwe?
Ninachofikiria, inawezekana kuna kamchezo kachafu kanakofanywa na wanasiasa. Labda study wanafanyiwa na CONTRACTORS halafu anamwambia mwanafunzi akariri na kuprezenti. Hili yawezekana linafanyika bila supavaiza kujuwa au anajuwa lakini anaona bora liende tu.
Hili yawezekana hata hawa wanafunzi wengine wanafanya lakini kwa kiwango cha chini. Ndiyo maana wanachelewa kumaliza. Hawa wanasiasa wanafanya kiwango cha juu ndiyo maana wanamaliza mapema.
Nimefikiria tu. Nimefikiria nikaona nirushe hapa ili mnichape bakora.
Lakini nitashukuru mkinielekeza wanachofanya wao ili niweze kuwasaidia wanafunzi wangu.
Ikitokea siku nipate wasaa, nitaongea na Dr. Jafo, Dr. Biteko, Dr. Nchemba, et al. Nitawauliza mliwezaje wezaje? Wengine wanashindwa wakati wana vikazi vidogo vidogo tu.
Asalaam.
Aviti T. Mushi
Aliyechelewa kupata PhD, hivyo anawashangaa wanasiasa wanaowahi kuzipata ndani ya muda.