Leta ushahidi hapa kama unaweza, wewe si mwanafunzi kuna mtu unataka umchafue, hiyo kitu udom hakuna,
Na ushahidi nimekuwekea hapo , ukifaulu umefaulu na ukifeli umefeli.
Dreadnought @
Mtoa mada nahisi sio mwanachuo na ameelezwa hayo mambo na mtu ambaye pengine kadisco hapo UDOM. Anyway, mimi sijasoma hapo ila kwenye suala la Matokeo ya wanafunzi kuna shida kubwa sana. Mfumo wa matokeo hapo ni mbovu sana na unahitaji marekebisho makubwa sana ukilinganisha na ukubwa wa chuo.
Kinachomsukuma huyu jamaa kuzungumza hivo ni kuktokana na
kubadilika sana kwa matokeo ya wanafunzi. Na inashangaza ilikuwaje kwa chuo kutumia
comp. program.system ya mwanafunzi kabla ya kuifanyia tafiti ya kutosha na hiyo ndiyo ambayo ilisababisha wanafunzi hasa wa informatics kufanya lobby kwa mwezao ili awerekebishie matokeo yao.Pengine hiki kitu ndio jamaa anataka kukielezea hapa.
Tofauti na vyuo vingine hapa nchini, mf. UDSM matokeo yalikuwa sio ya kubadilika hovyo namna hiyo. Nakumbuka tulikuwa tunaambiwa kila semister tu-print matokeo yetu, na hata kama baadaye ikitokea shida yoyote unaweza ukasimama na hayo matokeo yako kama ushahidi.
swali ambalo naomba kuwauliza Je, mwanafunzi wa Udom saivi anaweza print matokeo yake akaenda nayo utawala akadai kama amaeonewa au lah? hasa pale ambapo amekuta yameshuka?
Na kwa nini matokeo ya udom yanabadilika hovyo sana kwenye aris yao? Je, wanaudom mmechukua jitihada gani kupambana na hilo? au kwenu sio priority? mnaona ni bie tuu..!
Inawezekanaje, upo likizo unampigia simu Prof. unamuuliza umepata ngapi anakujibu umefaulu ama C au B afu chuo kikifunguliwa ukichek tena aris unakuta una Sapp! How this happens?
Mwisho, kwa hakika Udom inahitaji mabadaliko makubwa kwenye quality hasa ukizingatia ndio chuo kikubwa.