Udom, udom, udom. Hivi hii ni kweli?

Udom, udom, udom. Hivi hii ni kweli?

UDOM ni mojawapo ya VYUO vya HOVYO kabisa kutokea TANZANIA, kwa postgraduate degrees hali ni mbaya zaidi maana wanafundishwa na walimu wengi wenye degree moja, kwa undergraduate kozi nyingi hata mazoezi kwa vitendo hawaendi, TUMEONGEZA IDADI YA WAHITIMU KWA CHUO HIKI CHA KATA BILA KUZINGATIA UBORA WA ELIMU.

naunga mkono hoja kaka yangu yupo hapo udom second year ananiambia walimu wao ni matutorial assistant ,hiki chuo cha udom kimekuja kuharibu elimu sijui madaktar watatibu vip wakat hawafundishwi hata na mtu mwenye pHD na maengineer watajenga majengo chini ya kiwango
 
tatizo sio kuwa na part time lecturers,ila kutegemea tu part time lecturers bila kuwa na mtaalam wa kozi husika kwenye school,uwe muelewa.

mi naona we ndio kam sio muelewa kutegemea part time lecturers sio tatizo ata kama hakuna mtaalamu husika kwenye school.

cha muhimu hao malecturers wawe na sifa zinazoitajika, kumbuka udom ni chuo kipya bado wataalamu wake wengi wapo wasomoni ili baadae wawe malecturers.

kumbuka inaweza kuchukua si chini ya miaka 10 kwa chuo kipya kujitosheleza kwa asilimia kubwa kwa malectures iliyowasomesha kwa kozi mbalimbali.
 
hiki chuo cha udom kitakuja kuleta ubovu mkubwa kwenye elimuu , sipati picha lawyerz wanaotoka udom itakuwajee , nahisi school of law wataiona ni moto kwao, wahasibu je kutoka udom? nahisi c.p.a wanaweza wakafanya hata mara mia
 
Hii sasa kali tena,, IRDP development and planning ndo major wengi wameanza cheti ,diploma then degree hapo hapo sasa why wasiwe wazuri sana kwa fani hiyo!!!! THOUGH WE NEED DATA ili kuendelea na huu mjadala wako ila uzoefu unaonesha hivyo so far!!!

Challenge; Wanaosoma mipango cheti na diploma degree za fani zao huwa wanasomea vyuo gani mkuu??!!!

Hako katoto kacheti tu, mpk kakimaliza certificate yake kameenda field mara mbili, vijijini kuapply planning tool, na maofisini kujifunza hizo "planning technique" wakati anayesoma degree hapo UDOM hajui hata Field nini. Sio kwamba tunaponda, huo ndo ukweli unaopaswa tuuseme ili wahusika wasikae na wafanye mabadiliko, na si kupotosha ukwel ambao mwishowe wanaoathirika ni sisi vijana.
 
mi naona we ndio kam sio muelewa kutegemea part time lecturers sio tatizo ata kama hakuna mtaalamu husika kwenye school.

cha muhimu hao malecturers wawe na sifa zinazoitajika, kumbuka udom ni chuo kipya bado wataalamu wake wengi wapo wasomoni ili baadae wawe malecturers.

kumbuka inaweza kuchukua si chini ya miaka 10 kwa chuo kipya kujitosheleza kwa asilimia kubwa kwa malectures iliyowasomesha kwa kozi mbalimbali.

hivi mkuu, ina maana mtaani hakuna wasomi wenye sifa hitajika wangeweza kuajiriwa hapo Udom, au tatizo limetokana na nini?
 
Ni kawaida mwamba ngozi kuvutia kwake. Ni kanuni ya maumbile. Sishangai huyu anayetoka povu kutetea magonjwa ya mlipuko kwa chuo ali/anachosoma yeye.

Ukiongea na wahitimu wa UDOM wasio biased utasikia mambo ya ajabu. Moja, kozi nyingi hazina walimu wenye sifa. TA's wanashika kozi nyingi na GPA zao hazikidhi kiwango cha angalau 3.8 tunayoijua wote. Nina mfano wa mmoja mwenye GPA ndogo na anapiga mzigo kama kawa Department of Chemistry.

Pili, Shahada za Uzamili ni kama majaribio fulani yanaendelea wakati wakisubiri masomo. Ikama haina dalili ya kutimia kwa siku za karibuni kwa hiyo kozi nyingi zinafundishwa na watu ambao nao inabidi wasome kujua wanapaswa kufundisha nini. Walichosoma wao sicho wanachofundisha. Mifano mingi. Au ndio maana ada ni sawa na ya sekondari? PhD inasomwa kwa 500,000 kwa mwaka! Ingia kwenye web ya chuo ushindwe kucheka http://udom.ac.tz nenda postgraduate

Tatu, course za sayansi asilia /natural sciences zinafundishwa bila maabara na hivyo uhalali wa transcripts husika kuwa mashakani. Utasomaje sayansi bila practicals? Mmekuwa shule za kata zisizo na walimu wala maabara? Are you chuo cha kata?

Nne, crash programs (wao huziita extremes) ambapo part timer anapolazimika kuja, hufundisha kozi ya semester nzima ndani ya wiki moja mfululizo hii ikiwa ni pamoja na test, assignment na kutunga Final exam. Unategemea nini hapo? Wanasema matokeo yake mtihani wa mwisho UE hulegezwa ili kuwapa ahueni watahiniwa.

Tano, wahitimu wengi ambao hawakutokea makazini kukosa pa kwenda mfano wale wa BSc. Mathematics wasiojulikana wana utaalamu upi hasa. Kozi nyingi zina objectives zilizosimama lakini practically ni hewa tupu.

Na sita, udini. Hapo nisiitwe mchochezi lakini kwa wahitimu wengi wa UDOM walio wakweli hili halina ubishi.

Mnaobisha bisheni maana tunajua kisaikolojia hiyo ndiyo available option kujiliwaza.

Heko JK. Heko Kikula.
 
Ndibalema. Anaweza toa maelezo kuhusu hizo stori zako ambazo zinaonekana ni za kutunga.
 
Last edited by a moderator:
hiki chuo cha udom kitakuja kuleta ubovu mkubwa kwenye elimuu , sipati picha lawyerz wanaotoka udom itakuwajee , nahisi school of law wataiona ni moto kwao, wahasibu je kutoka udom? nahisi c.p.a wanaweza wakafanya hata mara mia

Usishangae ya UDOM. Kuna kimoja kinaitwa MUCCOBS zamani Chuo cha Ushirika Moshi kiko opposite na CCP. Ya huko tuyaache kwanza.
 
mkuu chromium UMENENAAA NI KWELI KABISAAA ETI MTU ANAFUNDISHWA NA LECTURER WIKIMOJA ,ANATUNGIWA TEST,ASSIGNMENT NA UE HUMOHUMO ALAFU LECTURER ANAONDOKA AKIRUDI ANAANZA KUSAHISHA UE ,JAMANI UDOM NI JANGA LA KITAIFA
 
hivi mkuu, ina maana mtaani hakuna wasomi wenye sifa hitajika wangeweza kuajiriwa hapo Udom, au tatizo limetokana na nini?

kumbuka watu wanaoitajika kufundisha chuo kikuu ni academician wenye kuanzia degree mbili.
1 wasomi hao bado ni wachache sana tz
2 si kila msomi ana interest ya kufundisha,ndio maana vyuo vikuu vina utaratibu kubakiza baadhi ya wanafunzi na kuwaajiri kama tutorial assistant(TA) ili baade wasome wawe malecturers.
kwa hiyo njia pekee na nzuri kuepuka na tatizo hili ni chuo chenyewe kuwa na sera za kusomesha TA kila mwaka

3 udom in kozi nyingi sana kuna kozi ambazo wataalamu wake kuwapata sio rahisi, na kuwaandaa pia inachukua mda(medicine,engineering)

nikupe mfano.wakati udom imechukua wanafunzi wa mwaka wa kwanza in medicine ilitumia walimu wa party time toka muhas na bugando, kwa kozi za mwaka 1&2, na wakati huo huo ilishapeleka vijana kusomea master medicine kwa ajili ya kufundisha kozi za mwaka 4&5(clinical medicine)
tayari wakufunzi hao wameitimu na ni waajiriwa wa udom as full time hawapungui 6, na wengine bado wapo vyuo mbalimbali wakisomea master.

nb kwa chuo kipya sio rahisi kuweza kujitosheleza kwa mda mfupi,inaitaji mda. na kamwe hauwezi kuanzisha chuo kikuu ukawa na waalimu wa kozi zote wanaotosheleza.

ata chuo kikuu cha dsm wakati kimeanzishwa miaka ya 63--65,kilitegemea kwa sana visiting lecturers toka makerere na ulaya.
 
Bw. Mwakalonge, uliyosema yote ni sahihi kwa asilimia 100!! TCU inashughulika na vyuo binafsi tu. Kibaya zaidi haya uliyosema yanatendeka pia kwenye programmes za Chuo cha Afya (College of Health Sciences) cha UDOM
 
kumbuka watu wanaoitajika kufundisha chuo kikuu ni academician wenye kuanzia degree mbili.
1 wasomi hao bado ni wachache sana tz
2 si kila msomi ana interest ya kufundisha,ndio maana vyuo vikuu vina utaratibu kubakiza baadhi ya wanafunzi na kuwaajiri kama tutorial assistant(ta) ili baade wasome wawe malecturers.
Kwa hiyo njia pekee na nzuri kuepuka na tatizo hili ni chuo chenyewe kuwa na sera za kusomesha ta kila mwaka

3 udom in kozi nyingi sana kuna kozi ambazo wataalamu wake kuwapata sio rahisi, na kuwaandaa pia inachukua mda(medicine,engineering)

nikupe mfano.wakati udom imechukua wanafunzi wa mwaka wa kwanza in medicine ilitumia walimu wa party time toka muhas na bugando, kwa kozi za mwaka 1&2, na wakati huo huo ilishapeleka vijana kusomea master medicine kwa ajili ya kufundisha kozi za mwaka 4&5(clinical medicine)
tayari wakufunzi hao wameitimu na ni waajiriwa wa udom as full time hawapungui 6, na wengine bado wapo vyuo mbalimbali wakisomea master.

Nb kwa chuo kipya sio rahisi kuweza kujitosheleza kwa mda mfupi,inaitaji mda. Na kamwe hauwezi kuanzisha chuo kikuu ukawa na waalimu wa kozi zote wanaotosheleza.

Ata chuo kikuu cha dsm wakati kimeanzishwa miaka ya 63--65,kilitegemea kwa sana visiting lecturers toka makerere na ulaya.

mkuu naona wewe una ufaham fulani juu yya udom.naomba unipe profile ya waalimu wanaofundisha nursing udom.nilitaka kuapply kufanya diploma this year,lakini nasikia hakuna mwalim aliyespecialize nursing hata mmoja ambaye yupo hapo school of nursing.na nasikia kuanzia mkuu wa kitengo mpaka mahead wa department hawajui nesi anatakiwa kusoma nini.
 
mi naona we ndio kam sio muelewa kutegemea part time lecturers sio tatizo ata kama hakuna mtaalamu husika kwenye school.

Cha muhimu hao malecturers wawe na sifa zinazoitajika, kumbuka udom ni chuo kipya bado wataalamu wake wengi wapo wasomoni ili baadae wawe malecturers.

Kumbuka inaweza kuchukua si chini ya miaka 10 kwa chuo kipya kujitosheleza kwa asilimia kubwa kwa malectures iliyowasomesha kwa kozi mbalimbali.

du,kumbe hata mimi naweza kuanzishachuo hata kama sina wataalam hata moja,nikitegemea washkaji waliospecialize hiyo fani?inaruhusiwa kisheria?
 
Kumbe ndio maana wamepunguza sifa za kujiunga pale maana wanachukua 2.5 cut off points.
 
Kumbe ndio maana wamepunguza sifa za kujiunga pale maana wanachukua cut off points kuanzia 2.5.
 
Endelea na remorse zako mkuu watu wanakosa dawa, wanawake wanazalia chini we unashangaa mtu kukosa placement!!!

Nimejaribu kukupa picha halisi wewe umekamatana na story ya mtaani hiyo case yangu ni kiwa ujue vyuo vingi havipati nafasi kwa wanachuo wote wahitaji so kwa wanaokosa inabidi wajitafutie na sababu nimekupa kuwa ofisi nying zinachukulia kama trainees ni mzigo or something kwa hiyo wanachukua watu wachache sana. Sasa hapo chuo kinafanyaje kwa mfano!!!

Udom ni buzz word kwa sasa kwa hiyo sikushangai wala na vyuo si viko vingi pia wanaoona.pale.sio ni kupeleka kwingine tu dont bother.It is a new UNi a milestone ya chuo kikubwa sio kama ofisi binafsi kwa hiyo kipindi ambacho we are in shumbles UDOM is not exceptiona case


Hutaki unaacha
sijui kwanini unakua mbishi kwa vitu ambavyo viko wazi, au unataka tufiche uhozo wadogo zetu waendelee kupotoka kwa kupata elimu duni!...,

Tofautisha Chuo kuwa na mkakati mahususi wa kuwatafutia Wanafunzi Field Placement lakini kwa bahati mbaya nafasi zikawa finyu kwenye Taasisi husika na ile ya kutoonyesha hali ya kutokua na mkakati huo kwa maana kwamba issue ya Field Practical kutokua kwenye mipango ya Chuo.....kwa maelezo niliyoyatoa awali nimesema hivi ndugu yangu anasoma Development Studies(Degree), swala la field kwao hakuna kabisa wanafunzi wanaangika kutafuta wao kama wao na wanaopata hawapatiwi supervision yoyote kutoka Chuo, na pia Field Report hawaandiki.

Tuwe makini jamani tunapokua tunachangia, sifa za kijinga za kuwa mimi nimesoma sijui UDSM sijui wapi hivyo najua kila kitu tuache. kuogopa kukosolewa ni hatari, mimi nitaendelea kusema, ili mhitimu wa Elimu ya Juu aonekane kweli ameiva kabla haja-graduate ni sharti afanye mazoezi ya vitendo(practical) kwa yale aliyoyasoma darasani kama theories. Hakuna umuhimu wowote Chuo kuanzisha program ambayo haina sehemu ya kufanyia Practical.
 
Back
Top Bottom