Ni kawaida mwamba ngozi kuvutia kwake. Ni kanuni ya maumbile. Sishangai huyu anayetoka povu kutetea magonjwa ya mlipuko kwa chuo ali/anachosoma yeye.
Ukiongea na wahitimu wa UDOM wasio biased utasikia mambo ya ajabu. Moja, kozi nyingi hazina walimu wenye sifa. TA's wanashika kozi nyingi na GPA zao hazikidhi kiwango cha angalau 3.8 tunayoijua wote. Nina mfano wa mmoja mwenye GPA ndogo na anapiga mzigo kama kawa Department of Chemistry.
Pili, Shahada za Uzamili ni kama majaribio fulani yanaendelea wakati wakisubiri masomo. Ikama haina dalili ya kutimia kwa siku za karibuni kwa hiyo kozi nyingi zinafundishwa na watu ambao nao inabidi wasome kujua wanapaswa kufundisha nini. Walichosoma wao sicho wanachofundisha. Mifano mingi. Au ndio maana ada ni sawa na ya sekondari? PhD inasomwa kwa 500,000 kwa mwaka! Ingia kwenye web ya chuo ushindwe kucheka
http://udom.ac.tz nenda postgraduate
Tatu, course za sayansi asilia /natural sciences zinafundishwa bila maabara na hivyo uhalali wa transcripts husika kuwa mashakani. Utasomaje sayansi bila practicals? Mmekuwa shule za kata zisizo na walimu wala maabara? Are you chuo cha kata?
Nne, crash programs (wao huziita extremes) ambapo part timer anapolazimika kuja, hufundisha kozi ya semester nzima ndani ya wiki moja mfululizo hii ikiwa ni pamoja na test, assignment na kutunga Final exam. Unategemea nini hapo? Wanasema matokeo yake mtihani wa mwisho UE hulegezwa ili kuwapa ahueni watahiniwa.
Tano, wahitimu wengi ambao hawakutokea makazini kukosa pa kwenda mfano wale wa BSc. Mathematics wasiojulikana wana utaalamu upi hasa. Kozi nyingi zina objectives zilizosimama lakini practically ni hewa tupu.
Na sita, udini. Hapo nisiitwe mchochezi lakini kwa wahitimu wengi wa UDOM walio wakweli hili halina ubishi.
Mnaobisha bisheni maana tunajua kisaikolojia hiyo ndiyo available option kujiliwaza.
Heko JK. Heko Kikula.