...we unafikiri hiyo Field Placement ambayo mwanafunzi mwenyewe anaenda kutafuta kwa kubuni itakua na ufanisi kweli hiyo!!!, wewe kama ulifanya Field Bungeni kwa kujitafutia mwenyewe shukuru Mungu ulibaatisha; na ata hivyo nina mashaka na ulichosoma darasani as Theory kama ndicho ulienda kufanyia Practical sana sana na we ulienda tu huko ili nawe uonekane uko Field:
sifa za kijinga tuache, Kitu cha msingi ambacho unatakiwa ukijue na kinachoongelewa hapa ni Juu ya ubora wa elimu inayotolewa UDOM hasa kwa baadhi ya Course, uwezi kuniambia nikakuelewa kwamba Mwanafunzi apewe INTRO LETTER aende mwenyewe kuangaika kutafuta Field Placement kusikojulikana bila Supervison yoyote ile alafu at the end of the day uniambie eti huyo mwanafunzi amejifunza kwa vitendo..
Of coz uhozo huu siyo UDOM peke yake bali ata Vyuo vingine upo ila unatofautiana lakini atuwezi kusema ni kawaida tuache hivyohivyo. Imagine mtu anamaliza Degree ya kwamba ukiangalia Transcript yake unakuta amesoma Research Methodology na ameandika Dissertation/research paper na vyote amefaulu sana tu-ukimuuliza Statement of the Problem ameipataje anajikanyaga tu.
Tuache sifa, tupende kukosolewa na kushauriwa na pia kuishauri Serikali panapowezekana kuongeza umakini, vinginevyo Elimu ya Juu tunaizika.