Huo ni mfano halisi tu ila nchi kama nchi kusema kweli kabisa tuna shida sana.
Nikuhakikishie tatizo la kweli la nchi yetu wala sio hayo ya mgao sijui V8 siju ila ni mindset za watu. Kubali kataa bado tunasafari ndefu sana ili kufanana na binadamu wengine. Nitakupa mifano michache sana hapa chini
1. Polisi na wanajeshi ndio wasimamizi wakuu wa sheria lakini
a. Hawalipi nauli hata kama wanaenda mizunguko yao binafsi
b. Hawasimami kwenye foleni au kwenye traffic lights hata kama hawana emergency yoyote anatoka kazini au anaenda kazini
c. Polisi na usalama wa Taifa badala wasimamie sheria kwa haki wakati wa uchaguzi wanakuwa washirika namba moja kuiba kura na kukibakiza madarakani chama fulani hata kwa gharama za kuuwa watu
2. Tazama uendeshaji wa boda boda au daladala. Haijalishi kuna nini yeye lazima anataka kuwa mbele kabisa. Kwenye taa nyekundu hawasimami hata kama traffic yuko hapo au ndio anaongoza magari.
3. Utakuta mtu ana li V8 asubuhi anaenda kazini kavaa tai na suti ila barabarani anatanua hataki kukaa foleni hata kama hana emergency yoyote na huyu eiza ni mfanyabiashara au ofisa wa serekali ila kachelewa kutoka kwake sasa anapita barabarani kwa kutanua hataki kufata foleni
4. Wabunge, mawaziri na Rais hawalipi kadi kwenye mishahara yao na kila siku wako majukwaani wanaongelea umuhimu wa kadi na wanatunga sheria kukamata raia wasiolipa kadi
Ni mind set zetu tu tukiweza kuziweka sawa nchi hii maendeleo ndani ya miezi 6 tu mbona tunapata