UDSM mnakosa hata Solar power karne hii?

  • Kumbe UD inaachwa mbali na baadhi ya shule za kanisa; baadhi ya shule zinazalisha umeme wake.
  • Aliyesema ni Extended High School amewaheshimisha sana.
  • Parking ina thamani karibia trillion hivi

"EXTENDED HIGH SCHOOL" hapa ndipo ninapomwamkia Jenerali Ulimwengu SHIKAMOO!
 
Mna vitivo vya Uhandisi, sayansi, ICT sheria ila mpaka zama hizi mnakosa Solar power project kusaidia wakati wa mgao? Mbona mnanunua V8/VX kila uchwao?

Mnakwama wapi?
**Kipi ninajivunia miaka 60 ya kuanzishwa kwenu?
REDET ni genge la wahuni
 
Unataka kutuambia jambo gani labda
Nataka kusema
1. Mkurugenzi anatembelea V8 lakini shuleni hakuna madawati
2. Prof. Janabi anatembelea V8 lakini muhimbili hakuna dawa.
3. Mbunge anapewa V8 kila baada ya miaka 5 lakini jimboni kwake hakuna kitu.
4. Niendelee kwa mawaziri hadi juu?
V8 ni matakwa ya serikali kwa nafasi zote za Presidential Appointee sio tu V8, kuna dereva, vocha, housing e.t.c
 
V8 ni matakwa ya serikali kuna vyeo lazima upewe usafiri na dereva
Hiyo V8 ndio kipaumbele cha viongozi wa Ccm na wateule wao.

Wanatenga mabilioni ya walipa kodi masikini kununua na kuyahudumia hayo MaV8 kila mwaka, huku miradi inayogusa maisha ya raia wao ikikwama kwa ukosefu wa fedha.

Watunga sera wa aina hii ni hasara tu kwa nchi.
 
Mambo ya serikali ndivyo yalivyo, inasikitisha sana...
 
5. Wavunjaji wakuu wa sheria za usalama barabarani ni madereva wa viongozi
6. Walaji wa rushwa wakuu ni watu wa serikali
7. Taasisi zinazotoa huduma za hovyo ni za serikali.
 
Taasisi inayozalisha wasomi ilitakiwa kuwa na mbadala wa umeme wa uhakika ili hata wasomi wake wakitoka hapo waone kuwa ni aibu nchi kuwa gizani waweze kutatua.
Kama ma professor na ma Dr waliotoka hapo wanapaita jalalani unategemea nin mkuu
 
5. Wavunjaji wakuu wa sheria za usalama barabarani ni madereva wa viongozi
6. Walaji wa rushwa wakuu ni watu wa serikali
7. Taasisi zinazotoa huduma za hovyo ni za serikali.
Hakuna sehemu inaongoza kwa rushwa kama mahakamani na polisi halafu unaambiwa eti ndio vyombo ya kusimamia haki za raia
 
Mna vitivo vya Uhandisi, sayansi, ICT sheria ila mpaka zama hizi mnakosa Solar power project kusaidia wakati wa mgao? Mbona mnanunua V8/VX kila uchwao?

Mnakwama wapi?
**Kipi ninajivunia miaka 60 ya kuanzishwa kwenu?
VYuo vya uhandisi tanzania ni vitatu pekee "ATC ,DIT na MUST" sawa sawa na vya afya " MUHAS , BUGANDO na KCMC" .UDSM Watu wakasome ualimu na sheria basi .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…