UDSM: Tunaomba msaada wenu JF!

UDSM: Tunaomba msaada wenu JF!

wewe sisi watu wa UD tuko active sana humu JF.
sema tu shida hatujiandiki kuwa ni watu wa ud

Angalia post zetu wote ni wapya, mmekuja kama mmeelekezwa kuwa JF watamaliza matatizo yenu, jitahidini kufuta sheria hata kama ni haki yenu, itachelewa lakini mtaipata, mwaka wa mwisho wanagoma ili iweje wamebakiza nearly two weeks kumaliza shule then wakipigwa mwaka mwingine inakuwaje. Je walikamatwa na bangi nao mnawatetea, wanaofanya ufusika mbele ya macho ya watu nao wanatetewa, tunajenga jamii gani ya wasomi wasio heshimu utamaduni wa mtanzania, hawa ndo wanaanza kujifunza ufisadi hukuhuku maana wanakua wanajua kuwa msomi anafanya anachotaka.
 
Ninapenda kupitia hapa niweze kuzungumzia mtafaruku uliopo Chuo kikuu cha DSM. Mkuu wa chuo Prof Mkandara aliwasimamisha wanafunzi 25 hapo chuo akiwemwo waziri mkuu na mpaka sasa wanafunzi wote wapo kimya na hakuna kinachoendelea kudai kurudishwa kwa wanafunzi wenzao... NINI SASA sio kwamba wanafunzi wako kimya bali ni hila na jinsi mkuu alivyoamua kutumia UBABE NA NDIKTETA kuzuia any movement ambayo inaweza kuwarudisha pale chuo.

Ikumbukwe kwamba mkuu huyo yupo pale kisiasa na siyo kivingine na anapoaana matakwa ya chama chake hayafanikiwi anatumia njia mbadala za kuumiza umma wa chuo.

KWANINI NATUMIA JF: nia makusudi yangu kwamba tukitoa sauti ya nguvu kuwasaidia wanafunzi waliosimamishwa chuo eti kwa kuhatarisha amani ya chuo wanaweza kurudi.

Wanafunzi hapa leo walitaka kuanzia mgomo lakini kuna kina hali yawao kushindwa kwa maana kila mtu anayeonekana kuleta move anaitwa na Mgaya(PRof) anampiga biti na kumtukana tena kumwambia atamfunga.

Inaniuma sana pia nikifikiria Uongozi wa chuo unahaonga hata waandishi wahabari ili wasitoe sauti yao

Tupo Chuo kujifunza jinsi ya kutetetea maisha ya watanzania ambao wengi ni masikini tunaomba mtuunge mkono kwani bila msaada wenu hatutaweza...

Mwnakijiji, Invisible na wote wale nyie ni wanaharakati na mnajua nini maana ya haya yote tupeni sapoti ili tuweza kukikomboa chuo chetu then kiweze kuitetea nchi.

Tunamkumbuka Chachage ambaye alikuwa mtetezi wa wanafunzi Siyo hawa kina SHIVJi wanaomuenzi Nyerere bila kufuata yale yote aliyoyataka.
REVOLUTION FOR CHANGES

Usilitumie vibaya jina la Mwanamapinduzi na kamanda Chachage kwa upeo wenu mdogo wa kutafakari mambo! Kabla hujamhukumu Mzee Shivji ebu pitia historia yake enzi zake miaka ya 60 na 70 hata kipindi chote cha ujana wake hapo Chuoni utaipata vyema unataka aungane na upuuzi mlioufanya wa kutawaliwa na emotions badala ya rationality? mnaaibisha sana. Hata hivyo ni kweli kwamba chuoni kuna matatizo makubwa sana na sheria na kanuni zifuatwe kwa pande zote,wale wanaozembea na kusababisha matatizo kwa upande wa utawala nao wawajibishwe. Kwa wale tuliopita hapo tunafahamu vyema maana yake nini maji yanapokosekana Chuoni na hilo linaweza kutatuliwa bila hata ya VC kufahamu kama watendaji ngazi ya chini wanawajibika ipasavyo,
Kuhusu bangi na madawa Mabibo hakuna uongo hapo,nimeishi miaka mitatu mabibo kule uwanjani usiku ni bangi tupu kiasi kwamba wengi wetu tukijiuliza hawa mameneja na madaktari na wanasheria aina gani watatoka kama sio mafisadi na kituo cha polisi kipo jirani tu na walinzi wanaolandalanda. Ebu tumieni busara katika namna mnavyowasilisha madai yenu. Huyo bwana mdogo wa Uganda nae ana matatizo kama alifahamu kwamba kugombea nafasi kama Upresida wa UDSM huwa kuna zengwe kwanini hakujiandaa asiwapatie mwanya wa kumkamata!arudie kumsoma Machiavel asipoteze muda na ma law reports kama hamu yake ni siasa ona sasa kapoteza muda wa wafuasi wake watiifu!Hata kama lengo ilikuwa kumfanya asigombee lazima ufahamu mapungufu ya adui yako ili umumalize ebu waulizeni ndugu zenu wa Political science ama wote siku hizi mnasoma madesa hakuna wachambuzi tena?
Haki hupiganiwa kwa busara na hekima hapa si maanishi kwamba ili kuandamana kwa amani kwamba musubilie mpaka afande Tiba aseme yes kama SHY anavyoshauri maana huyu naye ana matatizo yake,bali nina maanisha kuhakikisha kwamba watawala hawapati kisingizio cha kushusha hadhi yenu machoni pa jamii,kwasasa mnaonekana kama wahuni kwa vitendo mlivyofanya! Jisafisheni ombeni radhi kwa jamii kisha leteni hayo madai yenu yachambuliwe!
ALUTA CONTINUA
 
Once again wanafunzi wamegoma kuingia madarasani na kuna uvumi kuwa kuna mwanafunzi mmoja ambaye alikuwa mjamzito amefariki dunia.

Note:-
Ni uvumi uliotapakaa miongoni mwa wanafunzi ambapo habari hizi bado hazijathibitishwa na UTAWALA, ila baadhi ya wanafunzi wameandamana wakiimba MBINGUNI KUNA MAKAO MAZURI SANA.
Tungojee tusikie kama ni kweli haya wanayoyasema.
 
Kwa hakika hakuna anayejua haswa Tatizo kuu ni nini haswa lakini kuanzia saa 4 asubuhi yaleo wakati wanafunzi hawa walipoanza tena maandamano yao kutokea UDASA wakapitia Yombo na kwenda utawala wameonekana wanabeba mabango ya kumtaka Mkuu wa Chuo ajiuzuri ndio bango la mbele kabisa lilikuwa linasema hivyo .

Upande mwingine ni kuhusu kile kilichotokea jana ambapo inasemekana bomu la machozi lilirushwa katika Mgahawa wa chakula kukatokea kifo cha mwanamama mmoja aliyekuwa mjazito pamoja na mtoto wake tumboni , pia kuna mwanafunzi mwingine naye alifariki katika vurugu hizo hiyo jana .

Kwahiyo leo asubuhi watu wameamka na mengine haswa kuhusu vifo vya watu hao , ila idadi kubwa ya wanafunzi haitoi ushirikiano kwa kikundi hicho cha wanafunzi wanaoendesha huo mgomo katika maeneo kadhaa nilipopita wanafunzi wengi wanaoongea na vyombo vya habari nao wanawashangaa wenzao tazama Channel Ten leo usiku utaona maoni ya wanafunzi waliohojiwa pale Hall 5 .

Wengine wanasema hawataka kuingiliwa uchaguzi wao , kama unajua uongozi wa chuo umemsimamisha mmoja wa wanafunzi aliyekuwa mgombea tokea nchini uganda , huyu mwanafunzi anapendwa sana hapa chuoni na yeye alitoa upinzani mkubwa sana kwa wanafunzi wengine wanaogombea sasa hapo kuja jambo

Mwisho kabisa mmoja wa wagombea uraisi hawa kwa jina nahifadhi yeye anaishi Msewe , huyu ni ndugu wa mmoja wa maprof hapa chuoni , sasa sijui yeye pia anahusika nini na kuingiliwa uchaguzi huu wa chuo .

Naishia hapa lakini wanafunzi wana mashaka kweli kweli haswa hawa wa mwaka wa mwisho wengine wanafikiria kuhusu maisha yao ya baadaye kwanini wasiachiwe wamalize mambo yao wakaendelee na maisha yao ?

MCHANA MWEMA
 
Ahsante sana Shy, lakini ujatwambia hilo bomu lilorushwa cafteria kulikuwa na fujo hau waliamua kulirusha tu, maana inawezekana wakawa wanawachokoza wenyewe ili wapate nafasi ya kuwafukuza chuo.
Mgomo umeisha au unaendelea saa hizi, fate wa wale ambao hawataki kugoma inakuwaje?
 
Du Aisee naona umeamua kuweka kambi Chuo kabis! lete hizo data basi. Hao wameuwawa jana ama leo? na hilolilikuwa bomu la machozi ama guruneti?maana naona vyombo vya habari jana havikugusia hilo zaidi ya polisi waliovunjwa miguu na kupigwa chupa!
 
Kwa hakika hakuna anayejua haswa Tatizo kuu ni nini haswa lakini kuanzia saa 4 asubuhi yaleo wakati wanafunzi hawa walipoanza tena maandamano yao kutokea UDASA wakapitia Yombo na kwenda utawala wameonekana wanabeba mabango ya kumtaka Mkuu wa Chuo ajiuzuri ndio bango la mbele kabisa lilikuwa linasema hivyo .

Upande mwingine ni kuhusu kile kilichotokea jana ambapo inasemekana bomu la machozi lilirushwa katika Mgahawa wa chakula kukatokea kifo cha mwanamama mmoja aliyekuwa mjazito pamoja na mtoto wake tumboni , pia kuna mwanafunzi mwingine naye alifariki katika vurugu hizo hiyo jana .

Kwahiyo leo asubuhi watu wameamka na mengine haswa kuhusu vifo vya watu hao , ila idadi kubwa ya wanafunzi haitoi ushirikiano kwa kikundi hicho cha wanafunzi wanaoendesha huo mgomo katika maeneo kadhaa nilipopita wanafunzi wengi wanaoongea na vyombo vya habari nao wanawashangaa wenzao tazama Channel Ten leo usiku utaona maoni ya wanafunzi waliohojiwa pale Hall 5 .

Wengine wanasema hawataka kuingiliwa uchaguzi wao , kama unajua uongozi wa chuo umemsimamisha mmoja wa wanafunzi aliyekuwa mgombea tokea nchini uganda , huyu mwanafunzi anapendwa sana hapa chuoni na yeye alitoa upinzani mkubwa sana kwa wanafunzi wengine wanaogombea sasa hapo kuja jambo

Mwisho kabisa mmoja wa wagombea uraisi hawa kwa jina nahifadhi yeye anaishi Msewe , huyu ni ndugu wa mmoja wa maprof hapa chuoni , sasa sijui yeye pia anahusika nini na kuingiliwa uchaguzi huu wa chuo .

Naishia hapa lakini wanafunzi wana mashaka kweli kweli haswa hawa wa mwaka wa mwisho wengine wanafikiria kuhusu maisha yao ya baadaye kwanini wasiachiwe wamalize mambo yao wakaendelee na maisha yao ?

MCHANA MWEMA

Tatizo ni wao Mkandara Ajiuzuru?kwa sababu gani ajiuzuru??mie nakwambia hakuna haja ya kuwasaidia hawa watoto waache wanende nyumbani then watarudi tena hapo tena kwa kuomba kurudi.

wanawatesa wenzao ambao hawana ndugu hapa Dar es salaam...
 
Parapanda Litalia parapanda - Hii ndio nyimbo iliyokuwa inaimbwa na wanafunzi waliokuwa wanaandamana kutokea UDASA wakapita Hall 6 mpaka kuelekea utawala , watu waliokuwa upande wa hall 6 na 7 walikuwa wanasikia vilio vya watu tu huko juu utawala , baadhi ya wanafunzi walikuwa nyumbani mwao wengine katika korido , wengine njiani wakiwashangaa wenzao , wale waliokuwa wanaandamana wengine walishika matawi ya mili , wengine vitambaa na hata wengine walibeba maji maji haya ni ya kujiandaa kama polisi wakivurumusha mabomu ya machozi tena waweze kujiosha nyuso zao .

Mbele kabisa kulikuwa na wanafunzi kama 6 hivi wote walikuwa wamebeba bango moja lilioandikwa kwa mkaa inaonyesha wanafunzi hawa hawakujiandaa ndio maana wanakuwa na bango ambali halisomeki vizuri wala nini , pamoja na wanafunzi kuandamana hivi sikuona vyombo vyovyote vya habari pembeni yao au nyuma yao kuweza kuhoji au kudadisi ni nini haswa wanafunzi wanachotaka .

Pia wapiga picha za televisheni hawakuwa pamoja na wanafunzi hawa waandishi wengi walikaa upande wa askari wa kuzuia fujo upande ule wa utawala , wengine walikuwa hall 7 wakihoji wanafunzi ambao hawajaandamana , sijaelewa kwanini haswa waaandishi hawataka kuwahoji wale wanaoandamana nao waongee chao , tatizo lengine ni kwamba hawa wanaoandamana hawana msemaji wao kwahiyo inakuwa ngumu sana kuweza kufuatilia au kukaa meza moja na uongozi wa chuo

Binafsi nilijaribu kumtoa mwanafunzi mmoja niongee nae kujua nini kinaendelea yeye akabaki kusema tu hatumataki mkandara , ukiuliza kwanini hajui jibu kwa nini , lakini pia kuna tatizo lingine kubwa baadhi ya wanafunzi wanasema wengi wanaoandamana wamekuwa na matatizo na chuo kwa muda mrefu wengi wao hawajamaliza kulipa adda zao wanazodaiwa na chuo kwahiyo nao wanajiingiza katika mgogoro huu .

Mpaka namaliza kuandika ukurasa huu hali ya chuo kwa sasa imetulia wanafunzi wanangoja kusikia chochote kutoka kwa uongozi wa chuo watasema nini waende nyumbani au wafanye nini , kuhusu mauaji yaliyotokea jana hapa chuoni , ni kwamba bomu hilo lilikuwa ni la machozi na lilipigwa katika mghahawa wakati wanafunzi wanapata mlo na kufanya mambo mengine ya kiafya

Hakuna upande wowote unaosema kwanini polisi waliamua kurusha bomu la machozi ndani ya kafteria au mule ndani kulikuwa na nini haswa lakini bomu hilo lilianguka karibu na mama mja mzito huyu mama akakosa kupumua vizuri na ndipo mauti yake yalipomkuta , maajabu ilikuwa hata watu wa msaada wa kwanza hawakuwa pale wanafunzi wachache walijaribu kumuokoa ikashindikana kweli kazi ipo humu ndani .

Na mwisho kabisa , maandamano haya yanayoendelea katika eneo la chuo ni batili hayajarihusiwa na mtu wowote yule , na hata kama yangeruhusiwa kuna sehemu zake za kupitia katika maandamano yoyote ili kuepusha fujo au uvunjaji wa amani kwa njia yoyote ile lakini maandamano ya wanafunzi haya ni tofauti kabisa wanapita katika mabweni ya wanafunzi wenzao ambao hawajagoma , wanatishia kupiga baadhi ya watu na wamesababisha hasara kwa baadhi ya biashara ndani ya eneo la chuo hayo ni makosa je watakuwa tayari kulipa hasara hii siku wakitakiwa kufanya hivyo ?

Hii nyingine sijui ni tatizo la mawasiliano au ni hujuma tu inayoendelea kutokana na maandamano haya huduma za mawasiliano ndani ya chuo zimekuwa za taratibu au hazipatikani kabisa mfano wale wanaouza kadi za simu hawauzi ingawa wako katika biashara zao huduma ya internet iko slow sana au kuna kipindi ilikatwa kabisa watu walishindwa kuwasiliana na ndugu na jamaa zao ndio maana usishangae kwanini habari hizi ziko kimya sana watu hawachangii katika blogu na forum zingine ni kuhusu uslow down wa huduma hii
 
jamani wakuu, tatizo ni kwamba hawa vijana siku hizi ujuaji mwingi, boom linawasumbua na kwa kuwa wengi ni familia zetu, matokeo huwa ni kununua televisheni na music systems, na aghalabu computer ambazo matumizi makubwa huishia kwenye music na pichachafu...semester ikienda mwisho lazima watafute sababu ili chuo kifungwe...mbona hawajagoma barabara ya Sam Nujoma ikamilike? au hatuwasikii hata wakitoa press release kukemea maovu mbalimbali ya serikali? msaada wangu kwao; wajitambue, kisha wawe reasonable, si kila kitu mgomo..after all, wenzao wamesimamishwa na hawajafukuzwa! tunakubali serikali na menejimenti ni vimeo, lakini wasomi onyesheni busara na upeo!!!

Haya ya kununua television na music system hayahusiani kabisa na kinachoongelewa hapa.
 
Hawa vijana inabidi wapate ujumbe kamili na waambiwe ukweli hata kama utakuwa mchungu kama Kwinini. Mimi sioni kama ni dawa kuwa tunatetea kila kitu eti tu kwa sababu wanavutana na viongozi wa serikali ambayo hatuipendi. Hawa vijana wa sasa wameshindwa kujiwekea mazingira ya kuheshimika.Siku zote ukijiwekea mazingira ya kuheshimika, misimamo isiyoyumba,ukawa na hoja zenye nguvu zinazosimama zenyewe, kutamfanya mtu yeyeote afikirie mara mbili kabla ya ku-interfare mambo yako. Kama hatutawaambia sasa na kubaki kuwatetea tu,hawatojirekebisha.Ni vizuri wakaelewa pia kuwa UDSM sio form V au VI

Kinachotetewa hapa ni demokrasia na haki sio uanafunzi. Kama huwezi kukemewa swala la wanafunzi wa chuo kikuu kuingiliwa na utawala wa chuo na kushinikizwa na kupandikiziwa viongozi, basi sidhani kama una sababu yoyote ya kulialia pale ccm wanavyopandikiza viongozi wao Zanzibar
 
Habari nilizobnazo,ni kwamba kama khali hii ikiendela mpaka leo saa sita ya mchana basi Makamau mkuu wa chuo atafunga chuo hicho,Jana jioni nilitembelea udasa kuongea na walimu ambao ni rafiki zangu na wako pale Mlimani,

wanashangaa jambo ambalo hawa vijana wanalogomea,wangomea bila kuwa na sababu,watu wamefanya kosa ambalo linapingana na student bylaws,eti wanataka waache kisa wao wanataka,

tunajenga taifa gani lisilofuata shera??lazima watu wajue uhuru wao unaishia wapi na sheria ziwe zinafuatwa tangu wakiwa vijana wadogo.

Nawashauri wadogo zangu,ngudu zangu vijana wa Chuo Cha Mlimani ,Mdogo wangu Daudi Deo..hakikisheni mnalinda Heshima yenu na pia muwe na nidhamu kwa kufuata sheria za Chuo,na ninavyomfahamu mkandara(prof.) ni mtu muungwa na mpenda haki toka yuko pale FASS.

Hakuna sheria ya chuo au ya nchi inayoruhusu chuo kikuu na uongozi wake chini ya dikiteta na fisadi mkandara kuingilia suala la uchaguzi wa wanafunzi na kisha kuwafukuza shule wale wanaotetea demokrasia kabla ya kuwapiga kwa mabomu na virungu
 
kama ulipata opportunity kusoma Mlimani utaelewa dhahiri kwamba elimu yetu ya juu ni zaidi ya duni. Yaani is somewhere between hell and devel deepsea. Haina chochote zaidi ya mchakato wa kukram na kusolve maswali magumu. Walimu ni wazee wasio taka kurefresh their idea with new world.

Try developed country and you will see the difference.

Hii na dharau isiyo na msingi wowote ule, wengine pia tumesoma hizo developed world lakini bado tunathamini elimu ya vijana wetu wa chuo kikuu. Chuo kilichotupatia vijana shupavu kama Zitto na Kitila Mkumbo.
 
wewe sisi watu wa UD tuko active sana humu JF.
sema tu shida hatujiandiki kuwa ni watu wa ud

Kweli thinkpad,

vijana wa UD mpo na mnawakilisha nchi yetu vizuri sana, Hao wengine ni chuki zao tu na dharau ila baadhi yetu tuko very proud of you guys kwa vile mnasomea kwenye mazingira magumu lakini mnapata elimu ya nguvu hapo mlimani.
 
What was the aim ya kugoma? Nini kilikuwa kiini? Let not look at the top, let focus on each corner.

Kama hawakuwa na kibali cha kuandamana then kwa nini waliandamana? Na kwa nini walikwenda kutoa wanafunzi walio madarasani? Mnapochaguliwa mlimani kila mtu anapata jina lake kwa wakati wake, sasa kwa nini mtu asiyetaka kugoma afanyiwe fujo?

Hawa watoto are out of touch, far away from reality.

Nani alikuambia kuwa bila kibali cha kuandamana hakuna kuandamana kama haki haitendeki? Watu kama nyie mngekuwa wapigania uhuru basi nchi hii na nyingine nyingi za Afrika zingekuwa bado chini ya ukoloni.
 
sasa kama hamjiandiki tutafahamu vipi??
anyway ni bora mmekuja hapa leo?hii inaonesha ni kwamba mko tayari kujadili masuala yenu binafsi na kuacha kujadili mambo yanayohusu taifa hapa katika JF,na nadhani mijadara kama ile iliyokuwa inaandaliwa na DUPSA itakuwa haipo coz tabia hizi mnazozionesha ni kwamba mmekosa ustaraabu na chuo kwa sasa kimejaa wanafunzi msio na subira na wenye jazba zaidi ya yote msiopenda majadiliano

siku zote kama unataka kmaliza jambo lazima kuwe na majadiliano yaliyo mauzri ili kuleta mafanikio hapo mbeleni,Jana mlipewa ushauri wa Bure nendeni kwa Mwenyekiti wa CCM wa mkoa akwasiaidie.

,endeleeni kujiandikisha tutakate ushi,embu tuambie nini kinachowafanya wagome??na leo nasikia mnandelea tena,

Wanafunzi wa UD ambao wako wengi sana hapa tena wengine wakiwa membaz machachari hapa JF hawana sababu ya kujitambulisha kama vile wewe na wenzako hamjajitambulisha kuwa ni nani na mnafanya nini huko ccm.

Katika hili la kwenda kwa mwenyekiti wa mkoa wa ccm linaoenyesha jinsi gani wewe na dikiteta na fisadi mkandara mnavyoweka siasa kwenye hii issue.
 
wanafunzi wa UDSM hawana hoja yoyote ya msingi hadi kufikia kuomba msaada hapa JF. wanachokihitaji ni kufanya vurugu na kuharibu mali na kuhatarisha maisha ya watu kwa kurusha mawe. sidhani kama suluhu ya 'matatizo yao' wanayodai itafikia kwa kufanya hivyo.
 
Kweli thinkpad,

vijana wa UD mpo na mnawakilisha nchi yetu vizuri sana, Hao wengine ni chuki zao tu na dharau ila baadhi yetu tuko very proud of you guys kwa vile mnasomea kwenye mazingira magumu lakini mnapata elimu ya nguvu hapo mlimani.


mwafrica wa kike why are you misleadind our young brothers? umepandikizwa kufanya hivyo? please please i have started doubting.

kwa nini hupendi vijana wetu kutulia na kufikia lengo lao?

ninaomba unijibu maswali haya.
1. je wewe ulimaliza UD mwaka gani?
2. je kwenye kipindi chako kulitokea mgomo?
3. ulishiriki kiasi gani? au ulikuwa kama remot control ukitumia internet wakati wenzako wanapigwa mabom.
4. kama huko Ud sasa hivi je unashiriki kiasi gani? au huko tu kwako unatumia propaganda za internet?

nimekudoubt sana. sababu unaongelea democracy lakini huongelei uvunjaji wa democracy ya wale waliotolewa maktaba na madarasani bila kuzingatia kama wao ni postgraduates or the opposite.
 
Wanafunzi wa UD ambao wako wengi sana hapa tena wengine wakiwa membaz machachari hapa JF hawana sababu ya kujitambulisha kama vile wewe na wenzako hamjajitambulisha kuwa ni nani na mnafanya nini huko ccm.

Katika hili la kwenda kwa mwenyekiti wa mkoa wa ccm linaoenyesha jinsi gani wewe na dikiteta na fisadi mkandara mnavyoweka siasa kwenye hii issue.

kama ni wengi na hawawezi kujibu hoja za msingi basi kizazi hiki ni cha vilaza vitupu. kitu gani kimeharibu UD ninayoifahamu?

ni makala ngapi hawajajibu.

msomi anapoomba msaada huwa anasema yeye kafikia wapi kimaandalizi, ila kwa hili tumewaomba hoja walizonazo ili tuwasaidie kuedit na wameshindwa kufanya vile. kinachofanyika ni kulia lia, hoo mkandala ni bata aliyeacha vifaranga nyuma etc.


wameshindwa kuturidhisha wale vijana waliofukuzwa kama sio wavuta bangi, au sio wote wavuta bangi, au wote ni wavuta bangi.

wameshindwa kuturidhisha kuwa yule mganda hakuonewa, maana kama hakuja na certificate ya form six, muda uliotolewa unatosha kuwa ametumiwa cheti chake halali. tangu february mpaka leo, jamani ems is a reasonable period for a serious person to have submitted his documents concerned.

tunasema hivi kulingana na hoja zinazoweza kutolewa kuwakandamiza wanafunzi pindi kunapotokea chuo kikafail a suit to the court of law.

wameshindwa kuconvince the majority of the population pale chuoni mpaka kutumia fimbo na fujo.

WAMESHINDWA WAMESHINDWA WAMESHIMDWA...
 
wanafunzi wa UDSM hawana hoja yoyote ya msingi hadi kufikia kuomba msaada hapa JF. wanachokihitaji ni kufanya vurugu na kuharibu mali na kuhatarisha maisha ya watu kwa kurusha mawe. sidhani kama suluhu ya 'matatizo yao' wanayodai itafikia kwa kufanya hivyo.

Hizi ni bangi tupu hapa na wanafunzi wa chuo wana akili na uwezo mkubwa wa kuona huu upuuzi unaotolewa na huyu anayejiita Lawyer
 
Ni kweli pale uongozi mbaya lakini hiyo sio ticket ya kuharibu mali na kufanya vurungu kilio chao kinaweza kusikilizwa kwa njia za amani. Hii ni sawasawa na sisi tuamue siku moja tukutane sehemu tuanze kuandamana bila kibali ni kwamba hata kama tutakuwa na hoja ya msingi hatutasikilizwa zaidi ni kuwa tutapigwa virungu na kuumizwa.
MWK, unajua kuwa kuna wavuta bangi na wanaotumia madawa ya kulevya wanatetewa na hawa wanafunzi sijui hili unalionaje, wanaruhusiwa kuwatetea wanaotumia madawa ya kulevya?
 
Back
Top Bottom