UDSM: Tunaomba msaada wenu JF!

UDSM: Tunaomba msaada wenu JF!

hivi hawa wanafunzi si ndio wale waliitwa diamond na jakaya kisha wakapewa flana na kofia na chakula cha mchana wakatoka wanaimba kwa mbwembwe na mikogo nyimbo za kuisifia CCM?
sasa leo hii kwenye ukweli wanakuja JF kutaka msaada upi? mi nahisi wakienda CCM makao makuu kueleza yaliyowasibu itakuwa vizuri zaidi.
acha sie tushughulike na mafisadi bwana.
 
hivi hawa wanafunzi si ndio wale waliitwa diamond na jakaya kisha wakapewa flana na kofia na chakula cha mchana wakatoka wanaimba kwa mbwembwe na mikogo nyimbo za kuisifia CCM?
sasa leo hii kwenye ukweli wanakuja JF kutaka msaada upi? mi nahisi wakienda CCM makao makuu kueleza yaliyowasibu itakuwa vizuri zaidi.
acha sie tushughulike na mafisadi bwana.

Hapa angekuwa mzee wangu makwaia angesema "...hapo patamu,unasemaje??embu rudia wasikie,kwamba waende CCM.."
 
Mimi kwa upande wangu hawa wanafunzi wa Chuo kikuu wa karne hii ni mabishoo waliojaa ubinafsi. Kuna ishu chungu nzima zinazogusa mustakabali wa nchi hii lakini hukuti hata siku moja wakizichambua na kuzitolea matatamko.

Wao kama wasomi wanaotegemewa na Taifa kuwa viongozi na watendaji, wanawajibu wa kuyachambua mambo muhimu kwa taifa hili kwa niaba ya watanzania wao ambao hawakupata nafasi hiyo. Hivi hawafahamu kuwa wakulima masikini wanawategemea wao kuwasaidia katika kuikosoa serikali kwa mambo mengi ya kijinga inayofanya??

Inanitia kinyaa kuona muda wote wapo kimya na wanapoona masuala yao yameguswa ndio wanaomba msaada kwa watanzania.

yaani hapa ndugu yangu umesema ukweli kabisa, kwenye kesi za kitaifa wao wananyamaza kimyaaa huku wakila raha, sasa shuzi lao limelipuka wanakuja wanahaha wanataka msaada...ni wapuuzi bwana hata kama ndo wasomi
 
wanakumbuka blangeti wakati kumekucha, mbona walivyoitwa diamond na kikwete hawakutaka msaada wetu?
so mi naona kama ni sheria wanazisoma na kuzijua, kama ni ubabe kila mtu kaumbwa nao so ukishindwa plan A tumia plan B.
ila swala la kuja kujikomba komba kwetu mi sioni kama ni la msingi.
 
sidhani kama ni vyema kuwahukumu hawa wanafunzi kwa makosa ya nyuma.

Nafikiri nyote mwafahamu wanafunzi wnegi wa chuo hufuata mkumbo wakifikiria tu kupata chochote cha tumbo.Thinking critically, kutowapa suluhisho kwa kuwa tu walishangilia mbio za CCM pake Diamond hakutakua ni faida zaidi ya kuwaongezea machungu.

Washaurini watoto hawa
 
sidhani kama ni vyema kuwahukumu hawa wanafunzi kwa makosa ya nyuma.

Nafikiri nyote mwafahamu wanafunzi wnegi wa chuo hufuata mkumbo wakifikiria tu kupata chochote cha tumbo.

Kumbe ni wafuata mkumbo? hata mkumbo wa ufisadi wanao akili mwao ili waweze kupata chochote cha tumbo tuu, Sasa hao ndio unadhani watakuja kulinusuru hili taifa hapo baadae au ndio watazidi kulididimiza kwa kufuata kwao mkumbo! Hawa ndio tunaosema kuwa ni taifa la leo.
 
sidhani kama ni vyema kuwahukumu hawa wanafunzi kwa makosa ya nyuma.

Nafikiri nyote mwafahamu wanafunzi wnegi wa chuo hufuata mkumbo wakifikiria tu kupata chochote cha tumbo.Thinking critically, kutowapa suluhisho kwa kuwa tu walishangilia mbio za CCM pake Diamond hakutakua ni faida zaidi ya kuwaongezea machungu.

Washaurini watoto hawa

hata huu mgomo wanaotaka si ni kufuata Mkumbo??Je tuwaache wandelee na tabia yao ya kufuata mkumbo..Je wakifuata mkumbo wa kuwapenda mafisadi,au wao kuwa mafisadi nani atalaumiwa??Samaki Mkunje angali mbichi
 
Kuna watu wa aina nyingi.
Wapo wale wanaoamini katika kutafuta suluhisho kisha wakaja kutafuta mchawi.
Na pia kuna wale wanaopneda kumtafuta mchawi wakamkemea wakimpiga vijembe na kufanya tatizo liendelee kusambaa bila kupata majibu.

Pia wapo wale wapendao kukaa pembeni na kulaumu tu huku wakitoa maneno yaso na daawa.
Kama mwana jambo jiulize waangukia katika kundi gani
 
Tatizo ni kwamba wanataka kuwa Political oriented kabla ya muda wao,si vibaya kuonyesha mapenzi yao zaidi kwa vyama vya siasa vilivyopo, isipokuwa kinachoendelea hapo ni nani CUF nani CCM nani Chadema n.k si uongozi wa chuo tena inawezekana labda ndiyo wanafanya Practical ya wanayojifunza darasani nawashauri wasome watafute hizo CV then waingie UPDP, TPP na kwingineko kujihusisha na siasa kwa muda huu kutawagharimu labda kama watakuwa tayari kufa msalabani kwa ajiri ya wengine japo kumbu kumbu zangu hazinionyeshi kuwa na binadamu aliepo Dunia ya sasa zaidi ya walioandikwa kwenye vitabu vitakatifu. Ushauri wangu vijana wasome, waondoke Chuoni salama then wataamua wenyewe KAMA NI KUWINDA NDEGE PORINI AU LA! na si vibaya wakifahamu kuwa huku Uraiani hali ya maisha si nzuri sana wakichemsha huko kwa sababu ya makundi wataula wa chuya
 
Taarifa za uhakika ambazo nimepata sasa hivi toka chuoni ni kuwa vurugu zimekuwa kubwa zaidi kiasi kwamba mabomu ya machozi yameanza kuporomoshwa.

Wanafunzi wanakimbilia vyumbani na hali inaelekea kuwa tete chuoni hapo.

Kama kutakuwa na zaidi nitakufahamisheni kwakuwa naongea na watu wa ndani zaidi pale.

Invisible
 
Nimepigiwa simu sasa hivi na mwanafunzi wa mwaka wa pili wa IT, wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kwamba, baada ya wanafunzi wa UDSM kuamua kuandamana kupinga kwa wenzao 15 kusimamishwa shule na kukamatwa ili kupelekwa mahakamani, mchana wa leo, hali ya amani hapo chuoni iligeuka baada ya askari polisi kutumwa kwenda kuwakamata wanafunzi wote ambao walionekana wakiandamana. Aidha, polisi waliendesha zoezi hilo kwa kuwakamata hata wale wanafunzi ambao hawakuwa wakiandamana, ili mradi walikuwa katika sehemu mbali mbali za wazi (hadharani), wakijikuta wakipigwa bakora na kuswekwa kwenye TZR za polisi!

Habari zaidi zitapatikana kwenye vyombo rasmi vya habari. Ila, habari hizi ni za kweli. Yeyote mwenye kutaka ufafanuzi zaidi apige simu namba +255-786-019019
 
Jamani, pamoja na mapungufu mengi ya hawa watoto ambayo yamezungumzwa sana, pengine sasa tungekuja na suluhu. Baada ya kunyimwa haki yao ya msingi "kumchagua kiongozi wao" kitendo kilichofuatiwa na vitisho na kesi zisizo na msingi, sasa ktk historia ya chuo, FFU wameingia na wanapiga mabomu, kupiga na kukamata watu ovyo.Huu ni uvunjaji wa haki za binadamu, hatuwezi kuendelea kukaa kimya na tukumbuke hii ndo imekuwa desturi kuwanyamazisha watu na kujenga tabia ya woga katika kutafuta haki"siyo tu UDSM".

Hatuwezi kunyamazia utawala wa aina yoyote unaoleta sumu ya woga, kwa nini wasikae wazungumze. Mkandala, is this the best uliyoiona kwa kipindi hiki? Shame on you Mkandara, shame kwa wanaharakati wote mliopo mlimani, Shamee to the university community!!!
 
Nimepigiwa simu sasa hivi na mwanafunzi wa mwaka wa pili wa IT,

hakuna kozi hiyo pale mlimani,navyojua kuna Bsc. in Computer science pekee,hauna haja ya kutupa namba.siye wenyewe tutajua.

Invisible fuatilia suala hili kwa ukaribu,
 
Mimi nawashangaa sana. Migomo kila inapokaribia mitihani kwa nini? Nyie kama mnasoma kwa mkopo wa sirikali, mjukuu wangu anasoma kwa pesa ya mauzo ya kolosho. Nimeuza mpaka tubuzi twangu kumlipia ada kisha alete upuuzi wa kugoma walahi ntanyonga mtu.

Kuna vijana hawataki kusoma wakiona mitihani visingizio kibao, mara uchaguz, mara nyumba za kulala chafu, mara maji hakuna. Mbona wenzeo akina Mbatia walipokuwa wakigomaga walikuwaga hawangoji mitihani? Haya watueleze kwa Mukandala walifuata nini tena usiku?

Mjukuu wangu Aggy nikisikia umegoma ntakuja nikutandike bakora mbele ya kadamnasi. Nimekupeleka huko kusoma, kama umeshindwa ludi nyumbani tuokote kolosho
 
Niko nje kidogo na UD hapa FFU wamemwagwa naona kwa uharaka magari 3 na lile la maji .Usalama kweli upo ? Naendelea kuangalia na mwisho wake sijui utakuwaje .
 
Nimepigiwa simu sasa hivi na mwanafunzi wa mwaka wa pili wa IT,

hakuna kozi hiyo pale mlimani,navyojua kuna Bsc. in Computer science pekee,hauna haja ya kutupa namba.siye wenyewe tutajua.

Invisible fuatilia suala hili kwa ukaribu,

Gembe naona umemshushua sana mwanahaki, nadhani hakuwa na nia mbaya kutoa taarifa hii, kama alikosea jina la kozi basi na simu pia ni shida??? hii itafanya watu wawewanaogopa kuleta habari hapa, mimi binafsi nilijua kakosea kozi lkn hapa ujumbe ulikuwa ni maandano na maaskari, les try to be realistic hapa jamani
 
Back
Top Bottom