DOKEZO Responded UDSM wamepigapigaje hapa kwa Tarimba Abbas, aliwezaje kusoma degree na masters ndani ya miaka miwili tu?

DOKEZO Responded UDSM wamepigapigaje hapa kwa Tarimba Abbas, aliwezaje kusoma degree na masters ndani ya miaka miwili tu?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
Wakuu

Wasifu wa mbunge wa Kinondoni Tarimba Gulam Abbas katika tovuti ya bunge unaonesha alitumia miaka miwili tu, 2010 na 2011 kupata degree pamoja na master's ya sheria kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam.

Hii inawezekanaje, wakati kwa kawaida tunafamu degree peke yake si chini ya miaka mitatu? Hapo Tarimba amepiga miaka miaka miwili na masters juu, Hii ni fedheha kwa chuo kikongwe kama UDSM.

Ukiachana na chuo lakini hata ngazi zingine zote amesoma mwaka mmoja mmoja, jambo linalotia shaka juu ya safari yake kwenye elimu na taaluma kwa ujumla.

Pia soma: Kwahiyo Bunge mnatuambia Tarimba alisomba Cheti, Diploma na Degree kwa wakati mmoja? Ile Masters imeenda wapi?

1748696282275.png
 
UDSM wamepigapigaje hapa kwa Tarimba Abbas, aliwezaje kusoma degree na masters ndani ya miaka miwili tu?
Nadhani UDSM utawaonea bure, huyo Tarimba atakuwa kajiandikia uongo mwenyewe tu, ila kwa kuwa ni mbunge hakuna wa kumuuliza wala kumwajibisha.

Kwa yale maelezo yake alipokuwa akimkosoa Gwajima, hawezi kuwa na kiwango hicho cha elimu, ni kilaza pro
 
Back
Top Bottom