UEFA champions league : Coincidence au ni kweli dunia inaendeshwa na binadamu..

UEFA champions league : Coincidence au ni kweli dunia inaendeshwa na binadamu..

Hii mechi LIVERPOOL ANASHINDA KABISA BILA MATATIZO... ILISHAPANGWA IMEPANGIKA... BADO UTEKELEZAJI TU...
 
Usifanye watu wakauza nyumba walale nje wakaweke betting
[emoji23] [emoji23] [emoji23] lakini ndio ukweli huo... Ila kwenye betting mtu asiweke direct win... Maana wanaweza wakatoka draw kwa 90 na LIVERPOOL akashinda kwa extra time ama penalties... Ila mimi naamini LIVERPOOL anashinda ndani ya Dk 90
 
Habari zenu wakuu..

Mimi ni mmoja kati ya watu wanaoamini kuna watu wanatupangia matukio kwenye sekta tofauti(uchumi, siasa, michezo)kila mwaka kwa namna watakavyo hapa duniani kwa faida wanazozijua wenyewe..

Leo nakuja na uchambuzi huu kuhusu matukio mbalimbali kwenye mashindano ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE mwaka huu..

Natumaini sote twajua 26/5/2018 kuna mechi ya fainali kati ya REAL MADRID na LIVERPOOL..

Mashabiki na wafuatiliaji wengi wa mpira imani yao ni kwamba REAL MADRID watachukua ubingwa mapema bila taabu yeyote ,lakini ni tofauti kwa mashabiki wa LIVERPOOL ambao tangu timu yao iingie hatua robo Fainali, wanaamini ubingwa ni wao..

UNAJUA KWANINI MASHABIKI WA LIVERPOOL WANAAMINI WATAIFUNGA REAL MADRID NA KUTWAA UBINGWA WA ULAYA.?

FUATILIA MATUKIO HAYA HAPA..


MAAJABU YA KWANZA.

1978
*Liverpool walichukua ubingwa kwa kuifunga Club Bruge 1-0..

*Royal wedding(Prince Michael of Kent alifunga ndoa na Baroness Von Reibnitz)..

*Papa John Paul 2 alichaguliwa kuliongoza kanisa katoriki duniani.


1981
*Liverpool walitwaa ubingwa kwa kuipiga Real madrid 1-0..

*Royal wedding (Charles,Prince of wales alifunga ndoa na Diana)..

*Papa John Paul 2 wa kanisa katoriki alipigwa risasi lengo likiwa kumuua(ingawaje alipona)..


2005
*Liverpool walichukua ubingwa kwa kupiga Ac millan KIMAAJABU kwa mikwaju ya penalti katika fainali inayotajwa kuwa bora kuliko zote UCL..

*Royal wedding (Charles prince of wales alifunga ndoa na Camilla parker)..

*Papa John Paul 2 alifariki dunia,(kumbuka ndiyo huyu aliyepigwa risasi 4 na kupona mwaka 1981 wakati liverpool wanachukua ubingwa)..


2018
*Liverpool wameingia fainali ya UCL kitu ambacho hakuna aliyetegemea kabisa(ingawaje tangu hatua ya robo fainali mashabiki wa liverpool uingereza walianza kuamini kombe ni lao kwa kuunganisha matukio haya)..

*Royal wedding(Jana Prince Harry alimuoa Meghan Markle)..

*Hakuna taarifa zozote mbaya kuhusu Papa (ingawaje mwaka haujaisha)..


MAAJABU YA PILI

2005
*Mechi ya ligi kuu uingereza iliyochezwa kwenye uwanja wa old trafford kati ya mahasimu LIVERPOOL na MAN UTD msimu huu wa 2005 ambao Liverpool waliibuka mabingwa wa UCL iliisha kama ifuatavyo.
-Man utd walishinda 2-1..
-Magori yote mawili ya Man utd yalifungwa na mchezaji mmoja(Mikael Silvestre)..
-Gori Liverpool lilipatikana baada ya beki wa Man utd(O'shea) kujifunga..

2018
*Mechi ya Ligi kuu uingereza kati ya mahasimu Liverpool na Man utd iliyochezwa old trafford msimu huu ambao Liverpool wameingia fainali ya UCL iliisha kama ifuatavyo..
-Man utd walishinda 2-1..
-Magori yote mawili ya Man utd yalifungwa na mchezaji mmoja(Marcus Rashford)..
-Gori Liverpool lilipatikana baada ya beki wa Man utd(Eric Bailly) kujifunga..


MAAJABU YA TATU

1981
*TUN MAHATHIR alichaguliwa kuwa Waziri mkuu wa Malyasia..

*Liverpool walichukua ubingwa kwa kuifunga Real Madrid 1-0 (27/05/2018)..

2018
*TUN MAHATHIR amechaguliwa kuwa Waziri mkuu wa Malyasia tena huku akiwa mzee sana.

*Liverpool wameingia fainali ya UCL ambayo itachezwa tarehe (26/05/2018) na watakutana na timu ileile(Madrid) waliyokutana nayo 1981 wakati MAHATHIR anachaguliwa kuwa waziri mkuu wa Malyasia.
View attachment 781794


MAAJABU YA NNE

1958 Real Madrid bingwa UCL..
1968 miaka 10 baadae Man united Bingwa Ucl..
1978 miaka 10 baadae Liverpool bingwa Ucl..
....
1998.Real Madrid bingwa UCl..
2008 miaka 10 baadae Man united bingwa Ucl..
2018 miaka 10 baadae,Liverpool wapo fainali..


ACHANA NA HAYO YA JUU, MAAJBU KAMILI HAYA HAPA SASA..
..

Mimi natofautiana na wewe kidogo, matukio ni kitu cha kawaida Duniani na ndiyo ambayo yanatengeneza historia. Hata wewe kwa ulichokiandika hapa ukifuatilia matukio mbali mbali yaliyotokea Duniani kwa leo na ukayakusanya, basi na wewe utatengeneza historia.

Ila nilichogundua wewe ni Madrid. Usitoe visingizio viiiingi. Mtapigwa kipigo cha mbwa koko. Ndoo ni ya Liverpool.

Salaaaaaah...waya
 
Ni vyepesi kufuata upepo kuliko kuukumbata tusubiri tuone 6days to go sio nyingi tutarudia huu uzi
 
Mimi ni mmoja kati ya watu ambao hawaamini Liverpool kuwa mabingwa wa UCL msimu huu
 
Mkuu sijasema Liverpool atakuwa bingwa(hakuna sehemu niliyoandika hivyo)..

Na vipi kuhusu Roma kujua ratiba kabla droo haijachezwa ,nalo ni suala la mwaka 47 ?
KUNA watu ni vigumu kuelewa huu uchambuzi.kuna watu wanafikir kila wanachokiona ndivyo kilivyo. Na ndio maana giza likiingia lazima umulike ili uone. Kuna mamb ya gizan na ya nuruni. KTK DUNIA YA LEO KM WW HUSOMI HUFWATILII. KILA KITU UTAKICHUKULIA KWA AKILI NYEPESI.
 
Mkuu mm sina neno nasubiri tar 26/05/2108
 
Mimi mkuu sipingani na wewe kabisa... Hii dunia kuna vitu hata mimi sivielewi kabisa kuna watu wanaiendesha dunia... Nilikuwa naingia deep web.. Mambo niliyoyakuta kule nimeamua kuacha kuingia aisee... Dunia ina siri kubwa sana...hizi vita vita hazitokei bahati mbaya... Matukio makubwa pia hayatokei kibahati
Mkuu "deep web" ndo wapi n mim nijaribu kuingia?
 
Mkuu mm sina neno nasubiri tar 26/05/2108
NA YA MWISHO NI HII
UKIACHA KIWA 1981 UKIIGEUZA INAKIWA 18...AKA 2018
BASI JUA KIWA 1981 HUKO GERMANY EITRANCH FRANKFURT WALIKUWA MABINGWA WA DFP CUP (KOMBE LA UJERUMANI)
.
.2018 HUKO UJERUMANI EINTRANCH FRANKFURT NDIO MABINGWA WA DFP (KOMBE LA UJERUMANI)[emoji5][emoji5][emoji5][emoji5][emoji5][emoji5][emoji5]
 
NA YA MWISHO NI HII
UKIACHA KIWA 1981 UKIIGEUZA INAKIWA 18...AKA 2018
BASI JUA KIWA 1981 HUKO GERMANY EITRANCH FRANKFURT WALIKUWA MABINGWA WA DFP CUP (KOMBE LA UJERUMANI)
.
.2018 HUKO UJERUMANI EINTRANCH FRANKFURT NDIO MABINGWA WA DFP (KOMBE LA UJERUMANI)[emoji5][emoji5][emoji5][emoji5][emoji5][emoji5][emoji5]
Noma sana
 
Mkuu, weka nyumba kabisa,; liverpool anabeba ndoo mapema sana m, tena kwa goli 1-0.
Duh! Mkuu hebu tuweke ushabiki pembeni, huwezi sema liver anachukua ndoo kwa kumfunga madrid 1-0 mapema, utakua huijui madrid vizuri wewe[emoji848].
 
Hapo ndo freemason wanachezaga na hesabu na namba na kila kitu kinaenda sawa.Lazima ujue kuwa Queen Elizabeth ni 'matron of frremason' na mjukuu wake ambae ndo mrithi wa kiti cha ufalme ameoa juzi.Hivyo piga ua lazima liverpool ashinde.
 
Back
Top Bottom