UEFA champions league : Coincidence au ni kweli dunia inaendeshwa na binadamu..

UEFA champions league : Coincidence au ni kweli dunia inaendeshwa na binadamu..

Kufuatilia haya mambo ni kazi kubwa
Unaweza kuogopa kila mzungu unaemuona
 
Ngoja tusubiri hiyo 26. Ninacho amini mambo huwa hayatokei kwa bahati mbaya tu.
 
Habari zenu wakuu..

Mimi ni mmoja kati ya watu wanaoamini kuna watu wanatupangia matukio kwenye sekta tofauti(uchumi, siasa, michezo)kila mwaka kwa namna watakavyo hapa duniani kwa faida wanazozijua wenyewe..

Leo nakuja na uchambuzi huu kuhusu matukio mbalimbali kwenye mashindano ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE mwaka huu..

Natumaini sote twajua 26/5/2018 kuna mechi ya fainali kati ya REAL MADRID na LIVERPOOL..

Mashabiki na wafuatiliaji wengi wa mpira imani yao ni kwamba REAL MADRID watachukua ubingwa mapema bila taabu yeyote ,lakini ni tofauti kwa mashabiki wa LIVERPOOL ambao tangu timu yao iingie hatua robo Fainali, wanaamini ubingwa ni wao..

UNAJUA KWANINI MASHABIKI WA LIVERPOOL WANAAMINI WATAIFUNGA REAL MADRID NA KUTWAA UBINGWA WA ULAYA.?

FUATILIA MATUKIO HAYA HAPA..


MAAJABU YA KWANZA.

1978
*Liverpool walichukua ubingwa kwa kuifunga Club Bruge 1-0..

*Royal wedding(Prince Michael of Kent alifunga ndoa na Baroness Von Reibnitz)..

*Papa John Paul 2 alichaguliwa kuliongoza kanisa katoriki duniani.


1981
*Liverpool walitwaa ubingwa kwa kuipiga Real madrid 1-0..

*Royal wedding (Charles,Prince of wales alifunga ndoa na Diana)..

*Papa John Paul 2 wa kanisa katoriki alipigwa risasi lengo likiwa kumuua(ingawaje alipona)..


2005
*Liverpool walichukua ubingwa kwa kupiga Ac millan KIMAAJABU kwa mikwaju ya penalti katika fainali inayotajwa kuwa bora kuliko zote UCL..

*Royal wedding (Charles prince of wales alifunga ndoa na Camilla parker)..

*Papa John Paul 2 alifariki dunia,(kumbuka ndiyo huyu aliyepigwa risasi 4 na kupona mwaka 1981 wakati liverpool wanachukua ubingwa)..


2018
*Liverpool wameingia fainali ya UCL kitu ambacho hakuna aliyetegemea kabisa(ingawaje tangu hatua ya robo fainali mashabiki wa liverpool uingereza walianza kuamini kombe ni lao kwa kuunganisha matukio haya)..

*Royal wedding(Jana Prince Harry alimuoa Meghan Markle)..

*Hakuna taarifa zozote mbaya kuhusu Papa (ingawaje mwaka haujaisha)..


MAAJABU YA PILI

2005
*Mechi ya ligi kuu uingereza iliyochezwa kwenye uwanja wa old trafford kati ya mahasimu LIVERPOOL na MAN UTD msimu huu wa 2005 ambao Liverpool waliibuka mabingwa wa UCL iliisha kama ifuatavyo.
-Man utd walishinda 2-1..
-Magori yote mawili ya Man utd yalifungwa na mchezaji mmoja(Mikael Silvestre)..
-Gori Liverpool lilipatikana baada ya beki wa Man utd(O'shea) kujifunga..

2018
*Mechi ya Ligi kuu uingereza kati ya mahasimu Liverpool na Man utd iliyochezwa old trafford msimu huu ambao Liverpool wameingia fainali ya UCL iliisha kama ifuatavyo..
-Man utd walishinda 2-1..
-Magori yote mawili ya Man utd yalifungwa na mchezaji mmoja(Marcus Rashford)..
-Gori Liverpool lilipatikana baada ya beki wa Man utd(Eric Bailly) kujifunga..


MAAJABU YA TATU

1981
*TUN MAHATHIR alichaguliwa kuwa Waziri mkuu wa Malyasia..

*Liverpool walichukua ubingwa kwa kuifunga Real Madrid 1-0 (27/05/2018)..

2018
*TUN MAHATHIR amechaguliwa kuwa Waziri mkuu wa Malyasia tena huku akiwa mzee sana.

*Liverpool wameingia fainali ya UCL ambayo itachezwa tarehe (26/05/2018) na watakutana na timu ileile(Madrid) waliyokutana nayo 1981 wakati MAHATHIR anachaguliwa kuwa waziri mkuu wa Malyasia.
View attachment 781794


MAAJABU YA NNE

1958 Real Madrid bingwa UCL..
1968 miaka 10 baadae Man united Bingwa Ucl..
1978 miaka 10 baadae Liverpool bingwa Ucl..
....
1998.Real Madrid bingwa UCl..
2008 miaka 10 baadae Man united bingwa Ucl..
2018 miaka 10 baadae,Liverpool wapo fainali..


ACHANA NA HAYO YA JUU, MAAJBU KAMILI HAYA HAPA SASA..

*MOJA.
Siku kadhaa kabla ya droo ya nusu fainali kufanyika zikiwa zimebaki timu 4, kwa 'bahati mbaya' timu ya AS ROMA ilituma email za offer kwa mashabiki wake kuhusu tiketi za mechi yao ya nusu fainali na Liverpool(kumbuka hapa droo ilikuwa bado).

View attachment 781812
Cha ajabu zaidi waliandika mpaka tarehe ya mechi hiyo,wakati zinakuwa zimepangwa tarehe mbili mbili tofauti na kinachoamua ni nani atacheza tarehe ngapi na nani ni droo tu kitu kinachoonesha haikuwa bahati mbaya..

Baadae Roma wakaomba msamaha na kusema ni 'technical issue' lakini droo iliyofanyika jijini Nyon ikaleta matokeo yaleyale katika tarehe ileile.


*MBILI..
Kwenye website ya UEFA huwa kuna sehemu wanaweka mabingwa wa UCL kwa mwaka huo na statistics zote sasa cha ajabu ni kwamba kabla fainali haijachezwa, 'kimakosa' waliwaweka Liverpool kama mabingwa wa Msimu 17/18(2018) ..
View attachment 781819
View attachment 781823
Baadae waliondoa na kuomba radhi kuwa ni 'technical issue'..


Mungu katupa maarifa ili tuyatumie vizuri kuchambua mambo, naamini kila mmoja wetu hapa ana akili na maarifa yatakayomfanya aelewe jambo hili kwa namna aelewavyo..


Msafwa,
Uporoto, Mbeya..
Hapa Kuna Kitu.. Ila Ukiweka ushabiki pembeni kuna Asilimia fulani Matokeo hupangwa kabisa kwa maslahi ya kibiashara maana Sasa Hivi watu hawachezi kujifurahisha tu ila wanaangalia Pesa ipo wapi...

So if Liverpool wakishinda then Utabiri wako utakuwa sawa ila wakichukia real madrid itakuwa false
 
Liverpool akishinda papa ajiandae....
Usisahau kuna papa wawili walio hai. Mmoja anaitwa Emeritus pope (Benedict xvi) aliyejiuzuru mwaka 2013. Na pope Fransis aliye madarakani sasa. Hivyo kama historia juu ya papa itajirudia baada ya Liverpool kuchukua ubingwa, nadhani papa atakayefuata mlolongo wa historia atakuwa Benedict xvi.
 
Ngoja tusubiri
 

Attachments

  • FB_IMG_1527023691727.jpg
    FB_IMG_1527023691727.jpg
    85.2 KB · Views: 46
Dah! Kwa utabiri wangu wacha nkaweke bet ya 1M kwa Liverpool
 
kivovote itakavokua. Fainal ya 2005 ya Liverpool na Ac Milan uhakika ilikua ya kimazingara. Liverpool hawakuwa nauwezo kabisa ya kuwafunga Milan si kwa kikosi na hata uwanjani. Mechi ilikua upande mmoja dakika zote 120 ukiotoa dakika sita.

Lazima palaikua na mchezo mchafu pale.
 
Hii Match itaisha kwa suluhu ya bila kufungana ila Real atashinda kwenye mikwaju ya penalti.

Nimeota hiki kitu mara mbili.
 
Liver akishinda tutaamini alipangwa cha muhimu washinde tu Madrid iwe salama yao na vielelezo vyote hivyo kuna watu watafungwa
 
us against the world.
kwa shabiki wa Man u kumpa kombe Liverpool ni sawa na kumkabidhi mkeo mwanaume mwenzio ampe vyombo mbele yako.
heri Madrid alichukue hata Mara mia kuliko Liverpool
 
Back
Top Bottom