UEFA EURO 2024: Special Thread | Final: FT: Spain 2-1 England (Spain aibuka bingwa)

Nimemiss chambuzi za Dr Ricky
Ungesikia hawa denmark sio wa kubeza na kwa faida ya watazamaji hii ndio nchi inayo ongoza kwa watu wake kula nyama duniani 😄🔥🔥🔥🔥

Nimemiss chambuzi za Dr Ricky
Ungesikia hawa denmark sio wa kubeza na kwa faida ya watazamaji hii ndio nchi inayo ongoza kwa watu wake kula nyama duniani 😄🔥🔥🔥🔥
Mzee alikuwa bonge la mshereheshaji

Naskia chanzo cha kifo chake ni kamari alikuwa anacheza sana kamari kwenye
 
Kwanza nachokataa ulivyosema Portugal haikuwa na wachezaji wazuri 2008-2017
Huu ni uongo

Wachezaji wazuri waliotokea kizazi kimoja na Ronaldo wapo na nimekutajia mfano ndio hao kina Ricardo carvalho, pepe, Luis nani, n.k na wengine ni hao walikuja mara moja ba kupotea

Squad ya sasa ya kina bernaldo ni bora kuliko ya 2010? Hii haina sana ukweli labda kama unaangalia kwamacho. 2010 Portugal walikuwa nafasi ya 7 kwa ubora, mwaka huu 2024 wapo nafasi ya 6. Kwa utofauti hapo huwezi kuona, hivyo tunasema Portugal ya 2010 na hii ya 2024 zote viwango sawa

Squad ya 2012 iliyoshiriki euro huwezi linganisba na hii ya Sasa? Huu nao ni uongo, kwa mujibu wa wapima ubora FIFA rankings Portugal 2012 walikua nafasi ya 3 kwa ubora nyuma ya Spain na Germany. Ww ubora unaupimaje? Maana katika hata hiyo euro Portugal ndio alitoa changamoto kubwa kwa spain iliiyokua bora kabisa duniani, bila mikwaju ya penalty spain alikua anatolewa

Squad ya 2014 iliyoenda kushiriki world cup nayo umeibeza? Kwa taarifa tu kabla ya world cup portugal bado ilikua nafasi ya 3 kwa ubora duniani nyuma ya Spain na germany

Unasema Ronaldo kukosa goli kwenye knockout stage ndio sababu ya we kuona Portugal haikua na timu nzuri? Hiyo kukosa goli ni la Ronaldo mwenyewe binafsi, maana katika timu hiyo hiyo ya Portugal wapo waliofunga goli kwenye hatua hiyo.

Mchezaji kufunga au kutofunga goli hatua flani haina uhusiano na uzuri au ubovu wa timu. Fernandez mchezaji wa kawaida tu kutoka timu ya kawaida kabisa ya Australia kwenye world cup iliyopita alifunga goli hatua ya knockout. Hii euro tunayoangalia sasa, ile iliyopita top scorer alikua Ronaldo pamoja Schik kutoka Czech, Czech ni timu ya kawaida kabisa lakini Schick ameweza kuibuka top scorer. Hivyo Ronaldo kushindwa kufunga goli knockout stage huo ni uzembe wake wala hauhusiani na uzuri wa wachezaji. Hata huu uzembe messi amewahi kufanya, 2010 hakufunga goli hata moja. Hapo napo ilibidi ilaumiwe Argentina?

Figo kusifia timu ya sasa sio hoja, ndio hufanya hivyo legends wengi. Hii euro Germany wameshinda 5 dhidi ya Scotland, lakini ulimuuliza kocha wa Germany kuhusu scotland bado ataisifia na kusema wana nafasi kubwa kuchukua ubingwa wa euro
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…