UEFA EURO 2024: Special Thread | Final: FT: Spain 2-1 England (Spain aibuka bingwa)

Ndio maana nikasema tukubaliane kutokubaliana. Hakuna haja ya mmoja kulazimisha kwamba ndie yupo sahihi na tukibishana hatutafika mwisho. Huu mjadala wa takwimu vs uhalisia ni mpana mzee baba jaribu kufuatilia hata uko mbele inaleta mkanganyiko nankusababisha majibu yasiwe na logical based hata kwenye utoaji tuzo ya ballon dor bado haijulikani kipi kinapewa uzito. Kuna mwaka ambao messi alipewa balon dor watu wakahoji inakuaje anyimwe iniesta ambae kabeba world cup ambae aliupiga mwingi sana kwenye yale mashindano na kafunga goli la kuwapa spain ubingwa? tukaambiwa messi anajua ball kuliko iniesta na ukiweka takwimu pembeni ukiangalia uhalisia unaona ni kweli ikabidi tunyamaze, msimu jana kachukua messi tukauliza kivipi anyimwe halaand ambae ana takwimu nzuri zaidi tukaambiwa messi kaupiga mwingi sana kule qatar na kachukua world cup. Kwaiyo bado mjadala wa takwimu vs uhalisia haujafika mwisho. Ndio yale yale kwenye takwimu unaambiwa uchumi unakua lakini ukicheki hali ya maisha mtaani inazidi kuwa mbaya. Takwimu vs uhalisia ni mjadala mrefu ndugu yangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…