Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yeah nashangaa VAR haijaona ila alimsukumaHili goli kwangu naona kabisa Gundogan kamsukuma huyu beki. Refa alipaswa kulikataa. Hungary wanaonewa.
Portugal ya 2008-2017 ilikuwa na wachezaji wa kawaida?Ni dhairi kabisa hujanipata kwa usahihi mantiki yangu, umenisosoma kwa juu juu tu kisha ukaona unijibu tena kwa comment iliyojaa mahaba yaliyopitiliza.
Kwanza nikukosoe Ronaldo tangu aanze kushiriki hii michuano ya Euro mwaka huu ni mara ya tano, na katika mara zote 5 amekuwa top scorer wa michuano mara moja tu ambapo ni mwaka 2020/21.
Na pia nikujuze tu Ronaldo katika international career yake ameshiriki hizi major tournaments yaani EURO,WORLD CUP,FIFA CONFEDERATION CUP pamoja na UEFA NATIONS LEAGUE zote kwa pamoja mara 12, sasa katika mara 12 zote alizoshiriki ameibuka kama top scorer mara 2 tu, je unajua sababu???? Ni kwanini kwenye international career ana golden boot chache hivyo na wakati kwenye clubs huwa haipiti misimu miwili anaibuka mfunga bora?
Endapo kama ungekuwa umenielewa mantiki yangu hata usingeona kuna shida kwenye comment yangu.
Yaani hizo goals ambazo wewe unaona amefunga na zinakuridhisha ni ndogo sana kulinganisha na zile ambazo angeweza kufunga endapo kama angecheza na teammates wazuri tangu kipindi yuko kwenye prime(2008-2017) na hata world cup angeweza kuwa nayo leo hii kama hiki kizazi cha akina Bernado Silva,Diaz,Fernandez,Joao Felix angekuwa na anacheza nacha tangu 2010 huko..... nafikiri kwa huu ufafanuzi utakuwa umenielewa sasa.