UEFA EURO 2024: Special Thread | Final: FT: Spain 2-1 England (Spain aibuka bingwa)

UEFA EURO 2024: Special Thread | Final: FT: Spain 2-1 England (Spain aibuka bingwa)

Leo sijaingia kijiwe nongwa cha euro nilikuwa nasoma majibu ya mpina kwa sipika kuhusu Ufisadi wizara ya kilimo na kashfa ya sukari hadi nguvu za kufurahia mpira zimeisha

TANGANYIKA yetu hii basi tu
 
Portugal ya 2008-2017 ilikuwa na wachezaji wa kawaida?

Huu ni uongo mkubwa, kwa miaka hiyo ukiacha Spain hakuna timu ilikua na wachezaji wazuri kama Portugal
Ricardo, Rui Patricio, Jose bosingwa, Pepe, Paulo Ferreira, Ricardo carvalho, maniche, costinha, Deco, bruno alves, postiga, Tiago, Simao, Quaresma, Nuno gomes, raul meireles, Mendes, Luis Nani, Mourinho, Hugo almeida, Fabio contreao, William carvalho,
Hao wote bawakua wazuri?
Wewe jamaa unachokataa sasa hapo ni nini? Halafu umetaja wachezaji waliotokea kwenye generations tofauti tofauti kwa ujumla na wakati mimi point yangu inalenga kuwa na wachezaji wazuri waliotokea kwenye kizazi moja kama ilivyo hivi sasa, hapo ndio tunashidwa kuelewana.

Labda nikuulize ile squad ya akina Rui Patricia,Bruno Alves,Miguel,Roland,Ruben Amorim,Duda,Pedro Mendez,Raul Mereles na Silvio ambayo ilienda kushiriki world Cup ya 2010 unaweza ukalingisha na hii ya sasa hivi ya akina Bernado silva??

Ile squad iliyoshiriki iliyoenda kushiriki Euro 2012 iliyokuwa imejaza wazee kibao akina Helder Postiga, Nuno Gomez,Carlos Martin,Ricardo Carvalho, Ricard Costa unaweza ukailinganisha na hii ya sasa hivi ya akina Raphael Leao??

Squad ambayo ilishiriki World cup 2014 kule brazil yenye midfield mbovu kabisa ya akina Miguel Veloso na Silvestee Velera ambapo walitoka hatua ya makundi unaweza ukailinganishan na hii sasa hivi ya Bruno Fernandez?

Yaani ni kwamba wewe unachotaka kusema hiki kizazi chao cha kisasa ubora wao hauna tofauti na vizazi vilivyopita au?

Halafu unasema eti ukitoa Spain hauna timu nyingine iliyokuwa na wachezaji wazuri kweli? Ronaldo angekuawa anacheza na wachezaji wazuri kama unavyosema angekosa goli hata moja kwenye knock out stage ya world cup tournaments licha ya kushiriki michuano hiyo mara tano???

Kwamba hawa wachezaji wa sasa hivi tunaowaona wakivaa uzi wa Portugal hawana tofauti na hao wa huko nyuma uliowataja au? Kwa hiyo wewe unabishana na Luis Figo ambaye anasema hiki kizazi cha sasa ndio kizazi bora zaidi kuwahi kutokea kwenye historia ya taifa lao?
 
Back
Top Bottom