Ufafanuzi juu ya haki ya mjukuu kurithi mali ya babu/bibi yake

Ufafanuzi juu ya haki ya mjukuu kurithi mali ya babu/bibi yake

zamani1116

Member
Joined
Oct 24, 2017
Posts
28
Reaction score
6
Habari wana jamii,kuna jambo naomba muongozo kidogo wa kisheria kwa mwenye ufahamu nalo.Tuna mali tumerithi toka kwa baba yetu na tuko watatu lakini kwa bahati mbaya mwenzetu mmoja amefariki na kuacha watoto wawili ambao ni wakubwa (above 18).

Baada ya msiba tulikaa kama familia na sehemu ya mali ya marehemu tukaigawa kwa watoto wake(kiukweli baada ya kufuata taratibu zote za mirathi kimahakama tulikabidhiwa mali za marehemu mzee lakini tulikubaliana kutokuuza kwa maana tulikuwa tunaendelea kuzisimamia na kugawana mapato tunayopata kwa usawa).

Lakini ikaja shida kwa mtoto mmoja wa marehemu ndugu yetu anaanza kusumbua anataka apewe pesa kwa maana tuuze tuwape fungu lao wakae pembeni mimi nikawa tayari kwa hilo kwa kuamini kuwa wana haki na sehemu ya mirathi ya mama yao lakini mwenzangu akasema hawapaswi kurthi na wala hawana haki ambapo ilileta tafaruku kubwa sana.S

WALI LANGU SASA, JE, HAWA WATOTO WANA HAKI KWENYE HILI AU LA!?NA MUONGOZO WAKE UKO VIPI!?
 
Ni mali ya Mama/Baba yao wana haki. Fikiria wanao nao waje wafanyiwe hivyo mbeleni

Ila tafuta wataalam wa sheria watakujulisha zaidi
 
Habari wana jamii,kuna jambo naomba muongozo kidogo wa kisheria kwa mwenye ufahamu nalo.Tuna mali tumerithi toka kwa baba yetu na tuko watatu lakini kwa bahati mbaya mwenzetu mmoja amefariki na kuacha watoto wawili ambao ni wakubwa (above 18).Baada ya msiba tulikaa kama familia na sehemu ya mali ya marehemu tukaigawa kwa watoto wake(kiukweli baada ya kufuata taratibu zote za mirathi kimahakama tulikabidhiwa mali za marehemu mzee lakini tulikubaliana kutokuuza kwa maana tulikuwa tunaendelea kuzisimamia na kugawana mapato tunayopata kwa usawa).Lakini ikaja shida kwa mtoto mmoja wa marehemu ndugu yetu anaanza kusumbua anataka apewe pesa kwa maana tuuze tuwape fungu lao wakae pembeni mimi nikawa tayari kwa hilo kwa kuamini kuwa wana haki na sehemu ya mirathi ya mama yao lakini mwenzangu akasema hawapaswi kurthi na wala hawana haki ambapo ilileta tafaruku kubwa sana.SWALI LANGU SASA,JE HAWA WATOTO WANA HAKI KWENYE HILI AU LA!?NA MUONGOZO WAKE UKO VIPI!?
Kisheria MJUKUU harithi mali

Labda kama kabla ya baba yenu kufariki aligawa mali zake na akampa marehemu kaka yako mali.... hapo hizo mali zitakuwa za marehemu na watoto wake wana haki ya kurithi
 
Ni mali ya Mama/Baba yao wana haki. Fikiria wanao nao waje wafanyiwe hivyo mbeleni

Ila tafuta wataalam wa sheria watakujulisha zaidi
Kisheria hizo sio mali zao(wajukuu na mama yao)
Hizo ni mali za watoto wa marehemu
Wajukuu na mama yao sio watoto wa marehemu labda iwapo watoto wote wa marehemu wakiwa hawapo hapo ndio wajukuu watarithi mali za babu yao

Ni ubinadamu na uungwana ndio hupelekea hata wajukuu kupewa urithi kwa mgongo wa “marehemu mtoto wa marehemu”
 
Yaani ni hivi mleta mada waliachiwa mali na Baba yao. Hizo mali wakagawana ila hawakuuza. Sasa kama wamegawana ina maanisha watoto wao pia wanahusika kwenye mali za hao watatu waliogawana. Pale hawarithi mgao wa babu bali wa mama au baba yao aliyefariki

Ninaposema mama au baba namaanisha hao watatu maana mleta mada hajataja jinsia ya marehemu ndugu yake

Mwenye mali akifa kisheria mali zinatakiwa kuhamishwa umiliki na kwenda kwa wahusika ambaoni
Mke wa marehemu
Watoto wa marehemu

Ikiwa mali hazijahamishwa kisheria au kimila/kienyeji na mali zikabaki kiujumla za wahusika hapo mali zitakua bado ni za marehemu
Siku zitakapo amuliwa kugawanywa rasmi kuwa miliki ya kila muhusika hapo wajukuu hawata husika

Inawezekana kuwapa gawio la mali za marehemu kama kodi au kitegeuchumi chochote kile
Lakini wakiingia kwenye kugawana rasmi basi wajukuu haiwahusu

Labda kama mgao ulikwisha fanywa kabla baba yao hajafariki hapo watakua na haki ya kudai mirathi ya baba yao aliyopewa na babu yao kabla hajafariki
 
Hapa ndipo nilipomuelewa mleta mada labda aje aseme vinginevyo
Labda kama mgao ulikwisha fanywa kabla baba yao hajafariki hapo watakua na haki ya kudai mirathi ya baba yao aliyopewa na babu yao kabla hajafariki
 
Wana haki ya kurithi kisheria tunaita per stirpes au urithi wa kizazi. Ikiwa marehemu aliacha watoto watatu, na mmoja wao akafariki kabla ya mgawanyo wa mali, watoto wa huyo aliyefariki (yaani wajukuu) watachukua sehemu ya urithi ambayo mzazi wao angepata.
 
Umesoma thread ya mleta mada? Na jibu lako ni kwa mujibu wa thread hiyo?
 
Umesoma thread ya mleta mada? Na jibu lako ni kwa mujibu wa thread hiyo?
Umesoma thread ya mleta mada? Na jibu lako ni kwa mujibu wa thread hiyo?
Ndio majibu yangu yako sahihi kutokana na mada kwa swali la milki ya mali. Na nimeelezea hapo, kama una kinzana lete majibu, maana unajiita attorney, mimi ni wakili pia, come with something hii ndio jamii forum.
 
Kisheria mjukuu haithi mali ya baba ila kwa kuwa baba yao alikufa, wanarithi mali ya baba yao na siyo babu. Wanasimama badala ya baba yao, ni haki yao.
 
Back
Top Bottom