Ufafanuzi kuhusu shambulio la gari la watumishi wa TRA eneo la Tegeta, Dar es Salaam

Ufafanuzi kuhusu shambulio la gari la watumishi wa TRA eneo la Tegeta, Dar es Salaam

Sikukuu hizi kuna wanaolazimisha mapato kwa janja janja wakisema wanatimiza wajibu kazini. Kama hilo gari lina shida, kwanini wasingelikamata kwa kufuata sheria na taratibu.

Kuzuia gari katikati ya barabara inaogopesha maana kesho tutaambiwa ni watu wasiojulikana. Nidhamu ya kazi za umma lazima iheshimiwe.

Hatuna wafanyakazi wa umma wanaofanya kazi kama magenge ya wahalifu. Ndio maana watu wanapokamatwa na kuchukuliwa kwa staili za namna hiyo, tunasikia ni watu wasiojulikana.

Tunavuna yale tunayoyapanda
 
nadhani ndugu huajelewa. Kwa taarifa iliyotolewa walikuwa wapo katika kudhibiti magendo na ndipo walikutana na gari ambalo walihsii kabisa ni moja ya gari zilizoingia kinyemela na inaonekana nia yao ni kutaka kuthibitisha ndipo walipofikiriwa vingine. Haya magari unaweza kuta hata namba siyo zake na wanabadili ili kutojulikana kama ni gari zilizoingia kinyemela na pengine walitumia mitambo yao na kuona usajili haukuwa sawa wa gari ndipo walipoamua kulifata.Sheria nimesoma wanayo ya kukamata kwa makosa kama hayo
Okay. Sawa mkuu.
 
Niauliza tu. Inakuwaje TRA watumie no za STL za serikali. Hao watumishi pia siyo waaminifu. Wanatakiwa wapewe onyo kali sana. Hapa walikuwa wanatafuta michuzi yao ndiyo maana wakaamua kufuatilia gari usiku wakati wangetumia vyombo vya sheria wangmpata mtuhumiwa kirahisi tu.
 
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inasikitika kuutarifu Umma kwamba gari yake yenye namba za usajili STL 9923, ikiwa na Watumishi watatu katika doria za kawaida za udhibiti na ukamataji wa magendo na magari yaliyoingia nchini kinyume na taratibu za Forodha na kutolipiwa ushuru, imeshambuliwa na watumishi kuumizwa katika eneo la Tegeta kwa Ndevu, tarehe 05 Disemba, 2024, usiku.

Kadhia hii imetokea baada ya watumishi wa TRA kubaini kwamba gari namba T229 DHZ aina ya BMW X6 ilioingizwa nchini kinyemela bila kulipa kodi za serikali stahiki kwa mujibu wa sheria na kuifuatilia kwa lengo la kuikamata ili kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria za kodi.

Wakati Watumishi wa TRA wanatimiza wajibu wao, walihusishwa na kitendo cha utekaji, kilichopelekea wao na gari kushambuliwa.

Mamlaka ya Mapato Tanzania, inawapa pole watumishi wake waliojeruhiwa wakiwa wanatimiza wajibu wao, pamoja na wengine wote waliojeruhiwa katika kadhia hii, na kuwaombea wapone kwa haraka.

Mamlaka ya Mapato Tanzania inauhakikishia umma kuendelea kutimiza wajibu wake kwa mujibu wa sheria.

"Pamoja Tunajenga Taifa Letu"

Imetolewa na;

IDARA YA ELIMU KWA MLIPAKODI NA MAWASILIANO

Pia Soma: Tegeta, Dar: ‘Wasiojulikana’ washambuliwa na wananchi kwa mawe
walitakiwa wawaue maaneener zao hao wanaojiita kikosi kazi wanajikuta sana TRA ni mila rushwa mikubwa sasa kama gari i;liingia kinyemela na wao ndio wanaosajili hayo magari nani wa kulaumiwa? hii ndio inatakiwa kuwa spirit kwa wananchi maana nchi imekua ya kifala sana.
 
Kwanini msingepa wito aende ofisini?

Mmepata mnachokitafuta , gari imeharibika na sasa mnaenda kulitengeneza kwa kodi za wananchi.

Mwisho wa siku hao wahuni wenu wameumizwa na mliyekuwa mnamtaka hamjampata.
 
Unajua watu wengi wanajua TRA ni makadirio tu ya biashara, saa 12 jioni wamefunga ofisi.

Kumbe kuna upande mwingine wana deal hadi na magendo na wanakesha, ila kwa escort ya vyombo vya usalama. Kama hawakuwa na polisi basi wamejitakia, pole yao.
Kwa mzee Ali kimbao walisema trafic akaenda kuuwawa Leo nani hata amini ni kweli ni tra. Wakibanagwa watatoa kila Aina ya vitambulisho
 
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inasikitika kuutarifu Umma kwamba gari yake yenye namba za usajili STL 9923, ikiwa na Watumishi watatu katika doria za kawaida za udhibiti na ukamataji wa magendo na magari yaliyoingia nchini kinyume na taratibu za Forodha na kutolipiwa ushuru, imeshambuliwa na watumishi kuumizwa katika eneo la Tegeta kwa Ndevu, tarehe 05 Disemba, 2024, usiku.

Kadhia hii imetokea baada ya watumishi wa TRA kubaini kwamba gari namba T229 DHZ aina ya BMW X6 ilioingizwa nchini kinyemela bila kulipa kodi za serikali stahiki kwa mujibu wa sheria na kuifuatilia kwa lengo la kuikamata ili kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria za kodi.

Wakati Watumishi wa TRA wanatimiza wajibu wao, walihusishwa na kitendo cha utekaji, kilichopelekea wao na gari kushambuliwa.

Mamlaka ya Mapato Tanzania, inawapa pole watumishi wake waliojeruhiwa wakiwa wanatimiza wajibu wao, pamoja na wengine wote waliojeruhiwa katika kadhia hii, na kuwaombea wapone kwa haraka.

Mamlaka ya Mapato Tanzania inauhakikishia umma kuendelea kutimiza wajibu wake kwa mujibu wa sheria.

"Pamoja Tunajenga Taifa Letu"

Imetolewa na;

IDARA YA ELIMU KWA MLIPAKODI NA MAWASILIANO

Pia Soma: Tegeta, Dar: ‘Wasiojulikana’ washambuliwa na wananchi kwa mawe
Nyakati zimebadilika,haya mambo ya kukamatakamata watu kwa njia zinazonekana kihuhalifu hazifai,sahv watu wanatekwa ovyo ovyo watu hawaaminiani
Kamateni watu kwa kufata utaratibu
Haya je kama huyo mwenye BMW angekuwa na bunduki angejihami sahv si mngekuwa mnazungumza mengine

Operation zenu nyingi mnafanya kiholela holela tu mnaonekana hata nyie wahalifu kumbe mko kwenye majukumu yenu

Ova
 
Inawezekana wao wanaona wanatimiza wajibu. Kukamata kuwe kwa utaratibu na kwa kutimiza vigezo vyote vinavyotakiwa.
Jamii yetu ina taharuki na hawa wanaosemekana ni watu wasiojulikana. Wanachukua watu na so far ni kama vile wameshinda maana hawakamatiki
Kwahiyo, pale raia wanapowaona wasiojulikana wameingia 18 zao, si wanawarahisishia kazi wenye wajibu wa kukamata?
Imani imepotea kabisa kwenye usalama wa raia sababu watu wengi waliopotea hakuna anayejua wameenda wapi. Kwahiyo ikitokea kuna mwanya wa kuzuia kupotezwa kwa raia wengine na watu wasiojulikana, raia wakiweza kudhibiti sina shaka wataendelea kufanya hivyo.
Necessity is the mother of all invetions.
 
Nasema hivi wananchi fanyeni hivyohivyo tena chunguzeni vizuri mkibaini ni watekaji kamateni piga mawe choma moto.

Yanatuumiza sn ya ndugu zetu kutekwa na kuuliwa.
 
Sikia,
Ipo gari Ingine iliyoingia hiyo miaka 8 iliyopita lakin sio hiyo BMW. Sasa hiyo gari Ingine labda ilipata ajali ikawa "Written -Off" ndio number plate zake (plate number) zikahamishiwa kwenye hiyo BMW iliyoingia juzi tu kimagendo.

Angalia hapa chini usajili wa bima hizo number unasoma ni gari ya aina gani
View attachment 3170139
Nakubaliana na wewe maana ilimkuta mtu wangu yeye sasa gari yake ilikamatwa na kuja fatilia kumbe kuna gari kama yake ilikuwa na namba zake ikadakwa nayo yeye akaachiwa sababu alikuwa na nyaraka halali akaendelea. Watu wanatengeneza namba bandia na kuvisha kwenye magari yao
 
Back
Top Bottom