Ufafanuzi kuhusu shambulio la gari la watumishi wa TRA eneo la Tegeta, Dar es Salaam

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inasikitika kuutarifu Umma kwamba gari yake yenye namba za usajili STL 9923, ikiwa na Watumishi watatu katika doria za kawaida za udhibiti na ukamataji wa magendo na magari yaliyoingia nchini kinyume na taratibu za Forodha na kutolipiwa ushuru, imeshambuliwa na watumishi kuumizwa katika eneo la Tegeta kwa Ndevu, tarehe 05 Disemba, 2024, usiku.

Kadhia hii imetokea baada ya watumishi wa TRA kubaini kwamba gari namba T229 DHZ aina ya BMW X6 ilioingizwa nchini kinyemela bila kulipa kodi za serikali stahiki kwa mujibu wa sheria na kuifuatilia kwa lengo la kuikamata ili kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria za kodi.

Wakati Watumishi wa TRA wanatimiza wajibu wao, walihusishwa na kitendo cha utekaji, kilichopelekea wao na gari kushambuliwa.

Mamlaka ya Mapato Tanzania, inawapa pole watumishi wake waliojeruhiwa wakiwa wanatimiza wajibu wao, pamoja na wengine wote waliojeruhiwa katika kadhia hii, na kuwaombea wapone kwa haraka.

Mamlaka ya Mapato Tanzania inauhakikishia umma kuendelea kutimiza wajibu wake kwa mujibu wa sheria.

"Pamoja Tunajenga Taifa Letu"

Imetolewa na;

IDARA YA ELIMU KWA MLIPAKODI NA MAWASILIANO

Pia Soma: Tegeta, Dar: ‘Wasiojulikana’ washambuliwa na wananchi kwa mawe
ACHENI UPUMBAVU,YAANI KWA HALI ILIYOPO TANZANIA NYIE MNAKWENDA KUMKAMATA MTU KWA STAILI ILE?
HIVI NYIE NDIO MNGEKUWA MWENYE GARI MSINGEONA MKO HATARINI?

BASI MNAONGOZA KWA UJINGA!
mnatukosea watanzania.
 
Yalitokea hapo bandarini tuu sio mbali kivile
Magendo Bandari ya Mbweni yalianza tangu Mbweni kukiwa ni mashamba ya mpunga

Mali Kutoka Zanzibar hasa Mafuta ya Kula na Betri ndio bidhaa kuu

Pwani ya Ununio wamejikita kwenye Ngada na yule rais wao Dallas

Kunduchi ni Mafuta ya Kula na baiskeli za Mitumba Kutoka Unguja

Pale Kunduchi kuna Boti ya Patrol ikiwabeba Usalama, TRA, Polisi na Uhamiaji Lakini naiona imefungwa kamba tu pale Pwani

Wasalimie hapo Kilingeni Msata 😀
 
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inasikitika kuutarifu Umma kwamba gari yake yenye namba za usajili STL 9923, ikiwa na Watumishi watatu katika doria za kawaida za udhibiti na ukamataji wa magendo na magari yaliyoingia nchini kinyume na taratibu za Forodha na kutolipiwa ushuru, imeshambuliwa na watumishi kuumizwa katika eneo la Tegeta kwa Ndevu, tarehe 05 Disemba, 2024, usiku.

Kadhia hii imetokea baada ya watumishi wa TRA kubaini kwamba gari namba T229 DHZ aina ya BMW X6 ilioingizwa nchini kinyemela bila kulipa kodi za serikali stahiki kwa mujibu wa sheria na kuifuatilia kwa lengo la kuikamata ili kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria za kodi.

Wakati Watumishi wa TRA wanatimiza wajibu wao, walihusishwa na kitendo cha utekaji, kilichopelekea wao na gari kushambuliwa.

Mamlaka ya Mapato Tanzania, inawapa pole watumishi wake waliojeruhiwa wakiwa wanatimiza wajibu wao, pamoja na wengine wote waliojeruhiwa katika kadhia hii, na kuwaombea wapone kwa haraka.

Mamlaka ya Mapato Tanzania inauhakikishia umma kuendelea kutimiza wajibu wake kwa mujibu wa sheria.

"Pamoja Tunajenga Taifa Letu"

Imetolewa na;

IDARA YA ELIMU KWA MLIPAKODI NA MAWASILIANO

Pia Soma: Tegeta, Dar: ‘Wasiojulikana’ washambuliwa na wananchi kwa mawe
Something is completely wrong,Kwa muda ule walitakiwa kuambatana na askari and sio kienyeji vile,this is completely wrong,completely wrong time.nimeongea Kwa lugha ya kigeni ili kusisitiza
 
Hao WALIO shambuliwa walikuwa wanakimbiza magendo yaliyotokea wapi mpaka yafike Tegeta?tegeta Kuna namdari?
Wale ni watekaji sio MAAFISA wa Tra

Bahati mbaya TRA wanasai walitaka kukamata hiyo gari kwa kutokulipiwa ushuru sahihi wakati inaingizwa nchini hivyo swala la magendo halipo kwenye issue ya leo pale TEGETA
 
Hujuo lolote wewe endelea na uchawa wako ili uweze kuishi. Hayo maeneo nayajua kuliko wewe unavyojua kushabikia wizi wa KURA!
Uzushi upo wapi! Unataka tuwataje hadi wahusika hapa?
sasa ukitaja inasaidia nini badala kuchukua hatua kizalendo?

don't exposed your nonsense gentleman 🐒
 
Magendo Bandari ya Mbweni yalianza tangu Mbweni kukiwa ni mashamba ya mpunga

Mali Kutoka Zanzibar hasa Mafuta ya Kula na Betri ndio bidhaa kuu

Pwani ya Ununio wamejikita kwenye Ngada na yule rais wao Dallas

Kunduchi ni Mafuta ya Kula na baiskeli za Mitumba Kutoka Unguja

Pale Kunduchi kuna Boti ya Patrol ikiwabeba Usalama, TRA, Polisi na Uhamiaji Lakini naiona imefungwa kamba tu pale Pwani

Wasalimie hapo Kilingeni Msata 😀
Na mpaka sahv wanashusha hata hapo kawe beach washashusha sana mizigo
Mchezo huo polisi wa tegeta na kawe wanaujuwa sana na wanakuwaga kwenye payroll zao
Labda kama sahv kdg watulie

Ova
 
sasa ukitaja inasaidia nini badala kuchukua hatua kizalendo?

don't exposed your nonsense gentleman 🐒
Kwani kumtaja mhalifu siyo hatua ya kizalendo? Hata maana ya uzalendo hujui! Unaweweseka tu ukifikiri uzalendo ni kuiba KURA TU.
mara ngapi polisi wanaahidi mpaka pesa kwa kuwafichua wahalifu?
Hatuongelei wizi wa kura hapa so huwezi kuelewa! Ulitaka nichukue hatua zipi za kizalendo labda ? Nikawateke? Au niseme juhudi za raisi zimesababisha maafisa wa TRA Kushambuliwa?
Uzalendo kwako ni UCHAWA WEWE
 
huo ni unafiki tu gentleman, ambao ni wa kupuuzwa,

mindset yako ina mawenge ya kuibiwa usichokua nacho.

nadhan unaelekea pabaya saikolojikali 🐒
 
Back
Top Bottom