Ufafanuzi kuhusu shambulio la gari la watumishi wa TRA eneo la Tegeta, Dar es Salaam

Ufafanuzi kuhusu shambulio la gari la watumishi wa TRA eneo la Tegeta, Dar es Salaam

Kama gari mnaijua na ina usajili kwanini msimuite mwenye nayo atoe nyaraka za gari yake? Inakuwaje mnaanza kufuatilia mtu tena usiku?

Nyie ni polisi?
Je mna mamlaka ya kumfuatilia mtu na kumkamata au kukamata mali yake bila kushirikisha vyombo vya ulinzi na usalama?

Hayo yote mmeyataka kwakuwa hali ya usalama wa raia nchini imedhoofu kiasi kwamba sasa raia ni lazima kuwa vigilant la sivyo ni kutekwa na kuuwawa tu.

Wafanyakazi wenu mnatakiwa muwape barua ya onyo kwa kuwa negligent. Wameshindwa kusoma alama za nyakati.
Nadhani Tuishie Hapa
 
View attachment 3170012

UFAFANUZI KUHUSU SHAMBULIO LA GARI NA WATUMISHI WA TRA KATIKA ENEO LA TEGETA (Kwa Ndevu)

Dar es Salaam, 06 Desemba, 2024:

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inasikitika kuutarifu Umma kwamba gari yake yenye namba za usajili STL 9923, ikiwa na Watumishi watatu katika doria za kawaida za udhibiti na ukamataji wa magendo na magari yaliyoingia nchini kinyume na taratibu za Forodha na kutolipiwa ushuru, imeshambuliwa na watumishi kuumizwa katika eneo la Tegeta kwa Ndevu, tarehe 05 Disemba, 2024, usiku.

Kadhia hii imetokea baada ya watumishi wa TRA kubaini kwamba gari namba T229 DHZ aina ya BMW X6 ilioingizwa nchini kinyemela bila kulipa kodi za serikali stahiki kwa mujibu wa sheria na kuifuatilia kwa lengo la kuikamata ili kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria za kodi.

Wakati Watumishi wa TRA wanatimiza wajibu wao, walihusishwa na kitendo cha utekaji, kilichopelekea wao na gari kushambuliwa.

Mamlaka ya Mapato Tanzania, inawapa pole watumishi wake waliojeruhiwa wakiwa wanatimiza wajibu wao, pamoja na wengine wote waliojeruhiwa katika kadhia hii, na kuwaombea wapone kwa haraka.

Mamlaka ya Mapato Tanzania inauhakikishia umma kuendelea kutimiza wajibu wake kwa mujibu wa sheria.

"Pamoja Tunajenga Taifa Letu"

Imetolewa na;

IDARA YA ELIMU KWA MLIPAKODI NA MAWASILIANO

Pia Soma: Tegeta, Dar: ‘Wasiojulikana’ washambuliwa na wananchi kwa mawe
Hatari, watu wameanza kuhamka kujitetea, hatari kubwa inakuja mbeleni
 
Poleni sana watumishi wa umma
Kazi za ku enforce compliance ya sheria zina madhira yake. Kikubwa ni kuwa na tahadhari wakati wote mnapoteleleza jukumu hilo
 
Unajua watu wengi wanajua TRA ni makadirio tu ya biashara, saa 12 jioni wamefunga ofisi.

Kumbe kuna upande mwingine wana deal hadi na magendo na wanakesha, ila kwa escort ya vyombo vya usalama. Kama hawakuwa na polisi basi wamejitakia, pole yao.
Magendo yapo kibao hapa Nyamisati na mpaka Mkuu wa TRA wa Mkoa na Wilaya nilishawapa taarifa,na hata dii.es.oo anajua hiki,ila hakuna kitu kimefanyika.
 
Flexible and anti smuggling unit hao... FAST

Wana operate kama Askari kamili na wana maeneo yao ya kushikilia watu/vitu. Ni kitengo kipo ndani ya TRA.
 
Tanzania ina tatizo kubwa majeshi mengi - TRA task force, misitu, uvuvi, mapori tengefu, TANAPA, mgambo, polisi shirikishi bila kusahau majeshi ya usalama yaliyo DCEA, Zimamoto, Uhamiaji na Polisi.

Traffic police walikuwa na mashine viganjani kwa ajili ya kutoza faini, kufuatilia faini ambazo hazijalipwa. Pia traffic police wanafuatilia insurance kama zimelipwa n.k

Kwanini TRA wasiripoti taarifa hizo za BMW kwa jeshi la police traffic ili lishughulikiwe kipolisi badala ya TRA kukimbizana mabarabarani na gari shukiwa ambalo linadaiwa halijalipiwa kodi zote ?

TRA inafanye kazi kwa kisasa zaidi na kuhusisha traffic police kukazia sheria za kodi za magari.

Majeshi ya TRA task force, misitu, uvuvi, mapori tengefu, TANAPA, mgambo, polisi shirikishi hayajulikani yanadhibitiwa kwa kanuni gani za kikazi, nidhamu na mamlaka yao yanaishia wapi .
Yaani hawa watu wa serikali are not coordinated.Mi nilijua gari halina usajili ,kumbe linalo tena namba D haya tuseme hiyo namba sio ,je kulikuwa hakuna namna nyingine ya kumkamata huyo mtu au gari mbona Trafic wanatukamata kiulaini tu ,tunabananishwa mataa hapo hufurukuti.Vijana wa watu wanashindwa kutumia busara ingawa sheria inaruhusu TRA kufanya hizo kazi but kwa kushirikiana na vyombo vya usalama.Rais si alisema akuna "task force " ya kodo eee au ninachoona kwa sasa nchi imekosa mwelekea kwenye usalama na soon "investor wataanza kuweka kama risky ya ku invest Tanzania .
 
View attachment 3170012

UFAFANUZI KUHUSU SHAMBULIO LA GARI NA WATUMISHI WA TRA KATIKA ENEO LA TEGETA (Kwa Ndevu)

Dar es Salaam, 06 Desemba, 2024:

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inasikitika kuutarifu Umma kwamba gari yake yenye namba za usajili STL 9923, ikiwa na Watumishi watatu katika doria za kawaida za udhibiti na ukamataji wa magendo na magari yaliyoingia nchini kinyume na taratibu za Forodha na kutolipiwa ushuru, imeshambuliwa na watumishi kuumizwa katika eneo la Tegeta kwa Ndevu, tarehe 05 Disemba, 2024, usiku.

Kadhia hii imetokea baada ya watumishi wa TRA kubaini kwamba gari namba T229 DHZ aina ya BMW X6 ilioingizwa nchini kinyemela bila kulipa kodi za serikali stahiki kwa mujibu wa sheria na kuifuatilia kwa lengo la kuikamata ili kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria za kodi.

Wakati Watumishi wa TRA wanatimiza wajibu wao, walihusishwa na kitendo cha utekaji, kilichopelekea wao na gari kushambuliwa.

Mamlaka ya Mapato Tanzania, inawapa pole watumishi wake waliojeruhiwa wakiwa wanatimiza wajibu wao, pamoja na wengine wote waliojeruhiwa katika kadhia hii, na kuwaombea wapone kwa haraka.

Mamlaka ya Mapato Tanzania inauhakikishia umma kuendelea kutimiza wajibu wake kwa mujibu wa sheria.

"Pamoja Tunajenga Taifa Letu"

Imetolewa na;

IDARA YA ELIMU KWA MLIPAKODI NA MAWASILIANO

Pia Soma: Tegeta, Dar: ‘Wasiojulikana’ washambuliwa na wananchi kwa mawe
Pole Sana Kwa ndugu zetu
 
Back
Top Bottom