Ufafanuzi kuhusu shambulio la gari la watumishi wa TRA eneo la Tegeta, Dar es Salaam

Mwambieni aache kuteka wàtu ona sasa anaumiza wasiohusika!
 
Valid point aione mkuu wa TRA
 
Gari namba DH si ni miaka karibu nane ipo nchini au? Yaani kwa usajili huo inaonesha iliingia nchini mwaka 2016. Sasa kweli tangu kipindi hicho ndyo ije idaiwe hizo kodi kwa kuzingirwa tena usiku? Halafu bila polisi?
Sikia,
Ipo gari Ingine iliyoingia hiyo miaka 8 iliyopita lakin sio hiyo BMW. Sasa hiyo gari Ingine labda ilipata ajali ikawa "Written -Off" ndio number plate zake (plate number) zikahamishiwa kwenye hiyo BMW iliyoingia juzi tu kimagendo.

Angalia hapa chini usajili wa bima hizo number unasoma ni gari ya aina gani
 
Shida ni kwamba mmekuja kama watekaji lazima mpigwe mawe tu adios
Wananchi wanahaki ya kutetea maisha yao kwa mtu asiyejitambbulisha rasmi kwa kufuata mujibu wa sheria.

Huu ukamataji haramu na utekaji, haya ndiyo madhara yake.
Wananchi hawana makosa na mimi binafsi safari hii nawapongeza.
Serikali ijisahihishe kiutendaji maana wananchi siyo nguruwe ambao unaweza kuwafanyia upendavyo.
 
sio vigilant tu ni tumekuwa masenari..
 
Wanasiasa bana, sijui wanawachukuliaje wananchi?

Basi, asubuhi Waziri Mwigulu Nchemba akaibuka Instagram na kulaani.

Wananchi nao wamemtolea uvivu (hakuna cha siasa).

Nawarahisishia TRA kupata snapshot ya public reaction kwa Waziri wenu na jinsi wananchi walivyochoka.

Iwe funzo pia kwa Serikali na Mamlaka zake huko tunakoelekea. Hofu HAKUNA TENA


 
TRA mnafanya mambo kama vile shule hamjapitia kabisa.

Yaani kipindi hiki cha utekaji halafu mnawatuma watu wawakamate mtu usiku kwa gari hizo hizo(Land cruiser)?

Pia nina mashaka kama kweli walikuwa wanafatilia gari ambalo halijalipiwa kodi usiku maana kama wangefanikiwa kuteka tungeambiwa ni watu wasiojulikana.

Siku nyingine mkifanya hivyo mnawahatarishia maisha wafanyakazi wenu; tumieni japo akili kidogo ingawa najua hakuna kitu mnajua zaidi ya kutumia nguvu bila hata chembe ya akili..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…