Ufafanuzi: Kuvunjwa Halmashauri ya Jiji la Dar kuipandisha hadhi Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kuwa Jiji

Moja ya manufaa yake ni kulifanya Jiji la Dar es Salaam kuwa na sehemu yake mahsusi ya kiutawala tofauti na ilivyokuwa awali. Awali, jiji la Dar es Salaam ni kama lilikuwa likielea kuhusu eneo hasa la kiutawala.
Basi wafute wakuu wa mikoa Mana wakuu wa wilaya wapo pia. Au unaonaje. Na raisi afutwe pia maana Kuna wakuu wa mikoa Mana Hana kazi zaidi ya kuzurura kila kazi anafanya mkuu wa mkoa kwenye eneo lake. Halafu cheo Cha headmaster kifutwe Mana Kuna academic master, discipline master, n.k.

Baba wa nyumba anyongwe maana Kuna watoto wanweza kujitawala pia hakuna haha ya kuongeza mzigo.

Huo no uamuzi wa kipumbavu
 
Mi kwa ushauri wangu naona wangevunja halmashauri kama tatu hivi; Manispaa ya Ilala, Kinondoni na Ubungo ndo zikatengeneza halmashauri moja ya Dar es salaam. Eneo ni dogo lina maeneo ya kiutawala mengi sana.
 
Kwa hio kuna jiji LA ilala na jiji LA dar es salaam
Au dar es salaam ndiyo eneo lote LA ilala tu?
Jiji la Dar lina manispaa 6 lkn kiutawala ilala ndiyo Makao makuu ya jiji la Dar. Wengine wanabaki kuwa manispaa zinazojitegemea ndani ya jiji. Nilivyoelewa mm.
 
Petro E. Mselewa ,

..mara nyingi maamuzi ya hovyo-hovyo huwa hayaeleweki, na yanahitaji nguvu nyingi za ufafanuzi.

..kuna thread zaidi ya tatu hapa JF kujaribu kufafanua uamuzi uliofanywa na serikali, na hali hiyo hainipi hisia nzuri kuhusu uamuzi huu.
 
I agree with you brother...
 
Mi naona siasa tu, na kutafuatiana ulaji tu kwa wafu fulani, wameona ili kuwe na ulahisi wa kufanya mambo yao ndio wakafanya hayo waliyoyafanya, kama kweli wameona kuna gharama kubwa hakukuwa na haja ya kulundika halmashauri nyingi kwa kamkoa kadogo kama haka ka Dar, wakati mtatizo ya watu wa mbangara ndio hayo hayo ya watu wa bunju, anyway ila unategemea nini cha maana toka ccm aka gambas, garbage in garbage out.
 
Malizia basi kwa kusema kuwa sasa Mkoa wa Dar Salaam uunaundwa na/una:

1.
2.
3.
4.
5.
 
Kwa ufupi huyu mzee ana ubabe wa kijinga! Kwani sheria inamruhusu kuchagua jina la halmashauri ? Kuchagua Meya anaruhusiwa na sheria gani?
 
Ndugu ahsante kwa ufafanuzi
 
umewadanya watu. Sehemu yote ya Mkoa wa Dar es Salaam ni jiji. Ila majukumu ya uratibu yaliyokuwa yanafanywa na halmashauri ya jiji iliyovunjwa sasa yatasimamiwa na ilala. So pale halmashauri ya mpya ya jiji la DSM itasimamia eneo lote la ilala pamoja na kazi za uratibu wa jiji la dsm ambalo linaundwa na halmashauri zote tano
 
Umeelewa vema sana mkuu. Kwamba kwa mfano: Madiwani wa iliyokuwa halmashauri ya jiji la Dar (ambayo ilikuwa eneo lote la mkoa wa Dar) waliweza kukaa kikao cha kujadili mpango wa usafi wa maeneo ya Ilala.

Wakati huo huo, madiwani wa manispaa ya Ilala nao waliweza kukaa kikao cha kujadili mpango wa usafi kwenye eneo lao la Ilala. Sasa hapo kwa akili ya kawaida tu unaona kuna duplication ya majukumu. Hivyo lazima tu kuna mmoja atakula ugali wa bure.

Pia kwenye issue ya kodi na ushuru kuna ahueni mwananchi atapata kwa sasa. Zamani mfanyabiashara wa Ilala kwa mfano angeweza kutozwa ushuru na watu wa manispaa, na kisha akatozwa tena na watu wa Jiji wakati manufaa ya shughuli hayajizidishi kwa mpangilio huo.

Kwa sasa mfanyabiashara wa Ilala atalipa kodi moja tu kwa halmashauri ya jiji la Dar es Salaam ambayo zamani ilikuwa ikiitwa halmashauri ya manispaa ya Ilala. Kwa sasa hakuna tena manispaa ya Ilala.
 

Umeeleza vizuri sana.
Lakini, kwa mantiki hiyo ya kutafutia utawala ardhi yake. Kwa mbaaali kuna sauti inalia NYIKANI ya ardhi kutafuta utawala wake pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…