Ufafanuzi: Kuvunjwa Halmashauri ya Jiji la Dar kuipandisha hadhi Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kuwa Jiji

Ufafanuzi: Kuvunjwa Halmashauri ya Jiji la Dar kuipandisha hadhi Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kuwa Jiji

Iteni vyovyote mnavyo jua, dar es salaam ni moja na itabakia moja.. uwe mwambe pande au kivukoni wote tupo dar.. mengine ni siasa tu.
 
Je matatizo vya Daresalaam ni kwasababu ya jiji kukosa sehemu mahususi?
Nafikiri issue kubwa hapo ni kuwa na halmshauri isiyo na eneo kiutawala na kuendesha halmashauri ni gharama kubwa. Kufuta halmashauri moja unnecessary kama hii ni jambo jema.
 
Kwa wasiolewa hebu nijaribu kuwaelewesha, ni hivi kwasasa tuna mkoa wa Dar es salaam ambao una manisapaa nne yaan kinondon, kigambon, temeke na ubungo na huo mkoa wa Dar es salaam una jiji moja Ilala. Kwahiyo mkoa wa Dar es salaam una wilaya tano, kt wilaya hizo tano, wilaya nne ni manispaa na wilaya moja ni jiji.
 
ILALA KUWA JIJI; RAIS AMEVUNJA KATIBA

Mnavunja SHERIA! Rais hana mamlaka chini ya Local Government (urban authorities) act kutengeneza urban authority. Hii ni mamlaka ya WAZIRI wa TAMISEMI.

Kifungu cha 7 cha SHERIA ya Local Government, Waziri anatakiwa kutoa NOTISI ya miezi 2 kwenye GOVERNMENT GAZETTE na gazeti jengine ili kuwapa wananchi muda wa KUPINGA hayo maamuzi.

Mnavunja SHERIA. Mtu asiye na mamlaka anafanya anavyotaka bila ya kufuata UTARATIBU uliyowekwa chini ya SHERIA. Magufuli akiambiwa AFUATE SHERIA na TARATIBU anapandisha HASIRA halafu anataka kuFIX watu! SHERIA ziko ili tusiwe na CHAOS! Anafanya CHAOS kwa maamuzi ya MAJUKWAA!

Wananchi wakipinga maamuzi ya Waziri, ni lazima Waziri asikilize malalamiko ya kupinga na ayachukuwe manani. Halafu anatakiwa kupeleka Maamuzi mbele ya Bunge!

Kwa mujib ya SHERIA, WAZIRI ana lazima ya kutumia DISCRETIONARY POWER yake JUDICIOUSLY! Ina maana kungekuwa na PAPER kutoka WATAALAM kueleza kwanini Halmashauri zivunjwe na itengenezwi 1! Mkiitwa STUPID mnahamamki! Kwanini lakini wakati hamuelewi UTAWALA wa SHERIA?

Fatma Karume.
 
Ilala imekuwa Dar city, kinondoni ikifikia viwango vya jiji itaitwaje? Inamaana ndani ya mkoa wa Dar kutakuwa Dar city, kino city, Tmk City etc itapofikia maeneo yote hayo yana viwango vya kuwa Jiji.
Mpaka Sasa hizo Kino, TMK ni majiji tosha. Ilala inaweza kua imeendelea kuliko TMK au Kino lakini TMK na Kino nazo zimeendelea kuliko labda Arusha au Mwanza ambayo ni Majiji
 
Hapana, Dar es Salaam kumbuka ni mkoa. Kwa maana ya Mkoa, ina idadi ile ile ya watu, kwa maana ya Jiji la Dar es Salaam ( Urban Proper eneo la Ilala) kweli itakua na watu wachache...
... shukran Mkuu umefafanua vizuri sana. Picha ninayoipata ni kwamba pale Feri upande wa Kigamboni, Magomeni, Masaki, Mikocheni, Mbezi Beach, Magomeni, Mwenge, Manzese, Sinza, Kijitonyama, Mwananyamala, Urafiki, Mabibo, n.k. ni viunga vya Dar-es-Salaam City while Chanika, Kajiungeni, Mongo la Ndege, n.k. ni Dar-es-Salaam City Center.

Kama idea ili kuwa ni kupata City Proper ya Dar-es-Salaam kulikuwa na umuhimu wa kupitia upya mipaka na kuamua ni maeneo yapi yawe Dar City Proper na yapi yawe Metro badala ya kuamua tu Ilala ndio iwe city proper na manispaa nyingine zote ziwe viunga.
 
Moja ya manufaa yake ni kulifanya Jiji la Dar es Salaam kuwa na sehemu yake mahsusi ya kiutawala tofauti na ilivyokuwa awali. Awali, jiji la Dar es Salaam ni kama lilikuwa likielea kuhusu eneo hasa la kiutawala.
Apo naona unataka sasa kuleta matango mkuu.Sema hii agenda setting ndiyo imetumika kufanya decision za mihemko.
 
Kwa mbaaali nimeanza kuelewa.....

Ila nina swali, kwa hiyo kumbe kuna wilaya nyingi tuu hapa Tanzania tunaweza kuzipa hadhi ya majiji? Mfano Moshi.
Ndio hivyo, mbona Arusha jiji inaundwa na wilaya moja tu ambayo ni Arusha mjini.
 
Ndiyo kusema, Jiji la Dar es Salaam kwasasa ni sehemu yote ya Wilaya ya Ilala na si vinginevyo. Wilaya za Kinondoni, Temeke, Ubungo na Kigamboni si sehemu ya jiji la Dar es Salaam. Hizo zimebaki kuwa Halmashauri za Manispaa. Katika kueleweka zaidi, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ya sasa imepakana na Halmashauri za Manispaa za Kinondoni, Temeke, Ubungo na Kigamboni. Kwahiyo, mtu wa Ubungo, Temeke, Kinondoni na Kigamboni hayupo ndani ya Jiji la Dar es Salaam.
Hicho ulichoandika siyo sahihi. Rejea maana ya miji na vijiji. Nchi ina miji, vijiji na mapori. Wananchi wanaishi aidha mijini au vijijini. Huko porini wanaishi wanyama pekee.

Miji ina madaraja yake (classification) kutegemea na ukubwa wake, idadi yake ya watu (population), miundombinu yake na maendeleo yake. Hayategemei mfumo wa utawala wake. Hivyo unaweza ukazifuta halmashauri zote nchini na miji ikabaki miji. Hili lilishatokea huko nyuma. Huwezi ukaifuta miji au ukaibadilisha miji kuwa vijiji. Miji itabaki miji. Unaweza kubadilisha wilaya au mikoa kutegemea na matakwa yako ya kiutawala wa maeneo ya nchi.

Hivyo mji wa Dar es Salaam wenye status ya jiji utabaki hivyo hivyo. Eneo lake liko pale pale na linaonekana kwa macho. Na eneo lake litaendelea kupanuka upende usipende. Kiutawala unaweza kuliita wilaya kama lilivyoitwa huko nyuma, unaweza kuliita mkoa kama linavyoitwa sasa, unaweza kuligawanya kwenye wilaya kadhaa kama linavoendelea kugawanywa sasa na kadhalika lakini jiji linabaki hilo hilo moja linaloonekana kwa macho. Watu watakushangaa kama utaligawanya jiji la Dar es Salaam kuwa na majiji matano - yaani majiji ya Ilala, Kinondoni, Kigamboni, Temeke etc.

Kilichofanyika ni kupunguza beurocracy za kiutawala. Mayor wa Ilala na wasaidizi wake wamekasimishwa tu heshima ya kuliwakilisha jiji lote la Dar es Salaam. Wakivurunda ataweza kupewa mayor mwingine mmojawapo kutoka maeneo mengine ya jiji la Dar es Salaam.
 
Hayo unayoita manufaa mimi naweza kuyaita ndio mapungufu....

Mwanzo ingeweza kuhakikisha resources zinagawanywa sawa kwa manispaa zote zilizopo bila upendeleo wala bila kusahaulika hata kule ambalo hakuna resources nyingi..., hivi sasa hiyo Ilala / Jiji itakusanya resources kwa manufaa yake na kila manispaa kivyake wakati mwanzo ingekuwa makusanyo ni kwa manufaa ya manispaa zote kulingana na uhitaji.., Huu naweza kuuita ni muendelezo wa kuondoa nadharia ya Umoja ni Nguvu....,
Sio kwamba hii italeta utendaji wenye tija kwa kila halmashauri na kuongeza maendeleo respectively!!?

Jiji la Dar ambalo ni Halmashauri ya Ilala itajisimamia katika ukuaji, same as Temeke, Kinondoni, Kigamboni na Ubungo. Kivuli cha jiji la Dar sasa kitaingia kiutendaji zaidi na si kujulikana kinadharia.
 
Sio kwamba hii italeta utendaji wenye tija kwa kila halmashauri na kuongeza maendeleo respectively!!?

Jiji la Dar ambalo ni Halmashauri ya Ilala itajisimamia katika ukuaji, same as Temeke, Kinondoni, Kigamboni na Ubungo. Kivuli cha jiji la Dar sasa kitaingia kiutendaji zaidi na si kujulikana kinadharia.
Mapato ya kila manispaa yapo sawa..., au ndio kila anayekusanya ale na kuzasa sio kuangalia kwenye uhitaji
 
Moja ya manufaa yake ni kulifanya Jiji la Dar es Salaam kuwa na sehemu yake mahsusi ya kiutawala tofauti na ilivyokuwa awali. Awali, jiji la Dar es Salaam ni kama lilikuwa likielea kuhusu eneo hasa la kiutawala.
Siku Kinondoni ikipandishwa kuwa jiji, Je kutakuwa na majiji mawili ndani ya mkoa mmoja wa Dar!?
 
HII INANILETEA PICHA YA MKuu WA MKOA ..mikoa kkosa sehem ya utawala wapo tu hapo juu nao wangevuliwa ukuu wa mikoa na kupewa wilaya ambayo ni makao makuu ya mkoa na yeye kwa kiongozi wa hao wengine.
 
Back
Top Bottom