Mpaka Sasa hizo Kino, TMK ni majiji tosha. Ilala inaweza kua imeendelea kuliko TMK au Kino lakini TMK na Kino nazo zimeendelea kuliko labda Arusha au Mwanza ambayo ni Majiji
Kino kwa kuendelea itakua imeipita Mwanza, Dodoma, Arusha, Tanga na Mbeya. Anzia Sealander Bridge, Masaki, Kinondoni, Magomeni, Sinza, Mwenge, Kawe, Mikocheni, Msasani, Oysterbay, Mbezi Beach, Mbezi Chini,Tegeta, Mbweni, Bunju, Unonio, Bahari Beach, Jangwani Beach, Mabwepande, Goba, Salasala, Mivumoni.
Chukua mali zote, nyumba zote na biashara zote, utakuta Kinomdoni inagalagaza majiji mengi tuliyo nayo na hata kwa ukubwa siyo ndogo.
Mfano mdogo, kwa sasa eneo la kutoka Morocco hadi Kijitonyama, imezaliwa CBD moja ya maana ambayo kwa Majiji mengine tuliyo nayo yanagalagazwa vibaya. Hii ni kuanzia Arusha, Dodoma, Tanga na Mbeya, mpambano utakua kwa Mwanza maana nayo iko vizuri sana.