Ufafanuzi: Kuvunjwa Halmashauri ya Jiji la Dar kuipandisha hadhi Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kuwa Jiji

Ufafanuzi: Kuvunjwa Halmashauri ya Jiji la Dar kuipandisha hadhi Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kuwa Jiji

Kiuhalisia hapa hujataja faida.

Kuelewa kulikua na madhara gani kiuendeshaji ana kiuchimi? Maana ilikuwepo toka mwanzo na kasi ya ukuaji ilikua juu pia.

Nafikiri ni suala la kupunguza matumizi yanayotokana na posho za vikao tu. sidhani kama kutakuwa na faida kubwa zaidi kivile!
 
Ndio kusema matukio yatakayotokea kinondoni, mwenge, magomeni, waandishi watasema "nje kidogo mwa jiji la daressalaam"
Watasema ni Manispaa ya Temeke Mkoani Dar es Salaam. Maana bado Dar es Salaam ni mkoa.
 
Mpaka Sasa hizo Kino, TMK ni majiji tosha. Ilala inaweza kua imeendelea kuliko TMK au Kino lakini TMK na Kino nazo zimeendelea kuliko labda Arusha au Mwanza ambayo ni Majiji
Kino kwa kuendelea itakua imeipita Mwanza, Dodoma, Arusha, Tanga na Mbeya. Anzia Sealander Bridge, Masaki, Kinondoni, Magomeni, Sinza, Mwenge, Kawe, Mikocheni, Msasani, Oysterbay, Mbezi Beach, Mbezi Chini,Tegeta, Mbweni, Bunju, Unonio, Bahari Beach, Jangwani Beach, Mabwepande, Goba, Salasala, Mivumoni.

Chukua mali zote, nyumba zote na biashara zote, utakuta Kinomdoni inagalagaza majiji mengi tuliyo nayo na hata kwa ukubwa siyo ndogo.

Mfano mdogo, kwa sasa eneo la kutoka Morocco hadi Kijitonyama, imezaliwa CBD moja ya maana ambayo kwa Majiji mengine tuliyo nayo yanagalagazwa vibaya. Hii ni kuanzia Arusha, Dodoma, Tanga na Mbeya, mpambano utakua kwa Mwanza maana nayo iko vizuri sana.
 
Nashindwa kujua ni kwanini hoi dhana inashindwa kueleweka.

Jiji la New York ( New York City kwa mujibu wa Wikipedia lina ukubwa wa Sq. Km 734 tu na liko katikati ya New York Metropolitan Area) lina watu milion 8+

New York Metropolitan area... Inajumuisha Long Island, Newark, New Jersey, nk. Hizo ni miji inayojitegemea lakini yenye uhusiano kibiashara na uchumi, usafiri, huduma etc na NEW YORK City.

Kilichofanyika Dar es salaam sio kipya. Ukiachilia kuwepo mipaka ya kiutawala ya jiji, na kupunguza gharama a za uendeshaji.. sasa kuna faida nyingi zaidi.

Lazima ili uwe na uwezo wa kuevaluate ukuaji wako uwe na mipaka. Kwa sasa hali inavyokwenda jiji la DSM linaendelea kufifisha mipaka yake na Halmashauri za mji wa Kibaha na Wilaya za Bagamoyo, Kisarawe na Mkuranga

Kama hatutabadilika tutakuwa na jiji linalokwenda tuuuuu bila kuwa na mwisho. Move ya kuziacha Manispaa za jiji zijiendeshe nje ya jiji zitasaidia kuondoa utegemezi na huduma za katikati ya jiji.. na kuongeza responsibility ya Council kwa wananchi.

Miaka nenda rudi soko kuu ni Kariakoo.. kwasababu kuna kutegeana..kwingi.. uboreshaji wa miundombinu, ujenzi wa maeneo ya huduma.. maboresho ya hospitali halmashauri zote zinategeana maana wana imaginary brother ..ambaye ni tajiri wa kwenye mawazo tuu.. (City council) hana hata pa kuishi.

Anatafuta shida za wadogo zake (Manispaa) ila anategemea mapato ya kutatua shida wamletee.. its a weird relationship.. na akishindwa hawezi kuwa accountable.. hana watu(population) hana ardhi.. hana hata vyanzo.. technically.. 🙂


Sasa Jiji la DSM linakuwa ilala kwa maana ya eneo la.kiutawala.. ila Catchment ya Jiji.. ( Metropolitan area inaweza siku moja kufika mpaka Bagamoyo, mkuranga, kisarawe na Mlandizi..

Kama ilivyo kwa New York jiji wana watu milioni 8 ila duniani wanatajwa kuwa na idadi ya watu milioni 20+ maana wanazingatia na wilaya zake au miji yake yote...

Kwa Dar hakuna kitakachobadilika
 
HII INANILETEA PICHA YA MKuu WA MKOA ..mikoa kkosa sehem ya utawala wapo tu hapo juu nao wangevuliwa ukuu wa mikoa na kupewa wilaya ambayo ni makao makuu ya mkoa na yeye kwa kiongozi wa hao wengine.
Sijakuelewa
 
Tangu Rais Dr. John Pombe Magufuli kuvunja Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na kuipandisha hadhi Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kuwa Jiji la Dar es Salaam, kumekuwa na mijadala kemkem kuhusu jambo hilo runingani, redioni na hata mitandaoni. Mjadala hasa unajikita katika kuelewa kilichofanyika jana. Wapo wanaosema kuwa kwasasa Mamlaka tu ya lililokuw...
Tofauti ni ipi,unakosa na unapata nini ukiwa ndani au nje ya Jiji?haya ni majina tu ya kulinda ugari wa watu Kijiogrsfia Dar es salaam ni Ubungo, Ilala, Kigamboni, Temeke, Kinondoni.

Sasa ukisema ile mamlaka ya Jiji la Dar inahusu Ilala tu,unakuwa ueleweki! Hapa nafikiri kama vile shughuri za Tanganyika zinavyofsnywa na Serikali ya muungano, basi shughuri za Manispaa ya Ilala,zitajumuishwa na kufanywa na hao ambao watakuwa wanasimamia shughuri za ki Jiji katika manispaa zote.

Sent from my TECNO CD6 using JamiiForums mobile app
 
Mkoa wa Mwanza una wilaya 5: Nyamagana,Ilemela,Misungwi,Magu na Sengerema. Jiji la Mwanza lina Wilaya 2: Nyamagana na Ilemela. Wilaya ya Nyamagana ndiyo halmashauri ya jiji la Mwanza, Wilaya ya Ilemela ni Manispaa lakini iko ndani ya jiji la Mwanza. Je Dar es Salaam?
Kwimba, Ukerewe na Buchosa sio sehemu ya Mkoa wa Mwanza?
 
Watangazaji wanasema mkoani Dar es salaam na sijijini Dar.
Ilala ni jiji IPO mkoa gani?
Kipi kilitangulia Ilala na Dar?

Inakuwaje Mbeya jiji then Dar mkoa?

Wataalum hebu mnisaidie Mimi STD 7 mbona mwanichanganya.
 
Watangazaji wanasema mkoani Dar es salaam na sijijini Dar.
Ilala ni jiji IPO mkoa gani?
Kipi kilitangulia Ilala na Dar?

Inakuwaje Mbeya jiji then Dar mkoa?

Wataalum hebu mnisaidie Mimi STD 7 mbona mwanichanganya.
Mbona kawaida mzee,mkoa ni mkubwa kuliko wilaya,wilaya ikikuwa inaeeza kuwa jiji.
Unavyosikia jiji la Mbeya ni pale central tu sio huko Tukuyu,sikui Kyela wala vijijini. Arusha nako hivyo hivyo.

Hata DAR mkoa jiji ilala hata Bukoba inaweza kuwa jiji ndani ya mkoa wa Kagera, Moshi inaweza ndani ya Kilimanjaro kwa sababu ni miji mikubwa tayari.
 
Watangazaji wanasema mkoani Dar es salaam na sijijini Dar.
Ilala ni jiji IPO mkoa gani?
Kipi kilitangulia Ilala na Dar?

Inakuwaje Mbeya jiji then Dar mkoa?

Wataalum hebu mnisaidie Mimi STD 7 mbona mwanichanganya.
Mwendazake alipokoroga mambo mlishangilia sana, vumilieni hivyo hivyo
 
Watangazaji wanasema mkoani Dar es salaam na sijijini Dar.
Ilala ni jiji IPO mkoa gani?
Kipi kilitangulia Ilala na Dar?

Inakuwaje Mbeya jiji then Dar mkoa?

Wataalum hebu mnisaidie Mimi STD 7 mbona mwanichanganya.
Kilimanjaro mkoa - manispaa Moshi
Rukwa mkoa - manispaa Sumbawanga
Kagera mkoa - manispaa Bukoba
Pwani mkoa - manispaa Kibaha.
Hiyo ni mifano sawa na Dar mkoa jiji Ilala.
Siyo mikoa yote yenye mji wenye jina sawa na mkoa.
 
Ufafanuzi mzuri sana,wengi wanajua mkoa unaweza kuwa jiji😁
Kilimanjaro mkoa - manispaa Moshi
Rukwa mkoa - manispaa Sumbawanga
Kagera mkoa - manispaa Bukoba
Pwani mkoa - manispaa Kibaha.
Hiyo ni mifano sawa na Dar mkoa jiji Ilala.
Siyo mikoa yote yenye mji wenye jina sawa na mkoa.
 
Ufafanuzi mzuri sana,wengi wanajua mkoa unaweza kuwa jiji😁
Inawezekana pale penye jina la mji na mkoa kuwa moja, mfano Morogoro, Dodoma, Arusha, Tanga na mingineyo. Dar es salaam walipounda zile wilaya tatu za awali kuwa manispaa, tayari umeshavua hadhi ya Dar kama jiji, maana huwezi kuwa na jiji ndani ya jiji.
 
Back
Top Bottom