Ufafanuzi: Kwanini tuliona Lissu anafaa urais 2020 na sasa hafai Uenyekiti?

Yeriko katika sakata hili amejivua nguo kabisa na kujitambulisha kuwa yeye ni chawa wa Mbowe wala si mwana chadema, hili povu analomwaga kama amesukutua omo ni dhahiri ana masilahi binafsi na Mbowe kuwa Mwenyekiti vinginevyo angekaa kimya na kusubiri wakati wa uchaguzi akachague mtu anayemtaka lakini siyo kuanza kumshambulia Lissu kana kwamba Lissu amevunja Katiba kutangaza nia.Nimemdharau sana huyu mtu ni wa hovyo kabisa.
 
Uchanga wa Lissu ni upi? Ni wapi Lissu ameshambulia wenzake?
Soma hoja za wadau humu.

Hiyo ndio premise yangu JF posts.

Sasa either unikosoe point zangu za kuwakosoa wenzake, kuliko kunipa maswali.
 
Upo sahihi mkuu,mm hoja yangu kwa yeriko ameonesha kuwa biased yeye kama mwandishi ,Kazi ya mwandishi ni kuelimsha jamii, hapo yeye hajafanya,
 
sikuwa ninajuwa kuwa wewe Nyenyere ni wa hovyo hivyo.

JESUS IS LORD&SAVIOR
 
Ukiona kiongozi kakaa muda mrefu kwenye uongozi, anapopata mpinzani ili aachie hiko cheo. Na maneno yanakuwa mengi na kumpinga sana huyo ajaye.

Basi jua kuwa, hapo kuna ulaji na maslahi makubwa sana. Pia kuna madudu makubwa, hawataki wengine wayajue.

Sisi tusio na vyama, wenye kupenda haki kote. Mbowe ni muda wa kupumzika, ije fikra mpya na mawazo mapya. Chadema ya sasa haina jipya, ipo kama nusu kujifia na nusu haijulikani.

Labda mseme ni chama boya, kilianzishwa kuwahadaa wananchi, kuwa kuna upinzani Mkuu Tanzania. Zaidi ya hapo, anahitajika Mwenyekiti mpya. Kila mwenye akili timamu, hawezi pinga hili. Ila wenye maslahi yao watapinga.
 
Cdm ni ccm c currently….busara ni kukaa kimya dingii…. Unaonekana huna tofauti na machawa ya ccm
 
Yeriko ( mizim ) inaanza kukukataa nenda katubu tena , wenda unalo chaguo lako ila sioni afya egemea upande mmoja , Hivi kweli wenda lissu yupo na mapungufu kama binadam ,je wafikiri Mbowe hana mapungufu kama binadam.

Nimependekeza Lissu na Mbowe wote wapigwe chini , John Heche achukue form na wajumbe wamuunge mkono kumpa kura ya ndio katika nafasi ya Mwenyekiti.

Mkuu unaeshimika sana ila sijui huu utoto unatoka wapi , unaweza kuwa unamkubali mgombea flani kaa kimia kura zitaamua ,sera za wagombea zitaamua ,shida ipo wapi sasa
 
Viongozi wa afrika huwa hatumii katiba bali wanatumia utashi wao, kwa ssb ya egoism
 
Upo sahihi mkuu,mm hoja yangu kwa yeriko ameonesha kuwa biased yeye kama mwandishi ,Kazi ya mwandishi ni kuelimsha jamii, hapo yeye hajafanya,
Asante kwa kunielewa. Kwenye hili Yeriko anaongea kama mwanachama wa Chadema na sio mwandishi. Ni wajibu wa wanachama wenzake kuamua kama yale anayosema yana m-disqualify Lissu kuwa Mwenyekiti wa Chadema. Wakiona mazuri yake yanazidi yale yanayodaiwa kuwa ni mapungufu yake watampigia kura. Wakiona la, watampigia kura mwengine.

Amandla...
 
Viongozi wa afrika huwa hatumii katiba bali wanatumia utashi wao, kwa ssb ya egoism
Katiba inaingiaje kwenye ilani yao ya uchaguzi.

Viongozi hawatekelezi katiba katika muda wao, ahadi ya kazi yao ni Ilani yao ya uchaguzi.

Someni siasa, hata elementary politics hamjui.
 
K
Kwa hiyo CHADEMA chini ya utawala wa MBOWE mnapo panga mipango ya kuingia kwenye michuano ya uchaguzi wa Rais huwa mnaingia kujaribu tu huku mkijua hamtoshi? Nyie watu mnachezea vichwa vya Tanzania kabisa, Yaani baadhi ya watu wamepoteza maisha katika kuunga mkono harakati zenu kumbe nyie mnafanya tu majaribio? Kweli nimeamini ukiamua kuwa chawa hata uwe na Elimu ya PhD lazima ujizime data ujivike Ujuha au ujivike elimu ya Chekechea
 
Unafiki na double standard ni vitu vibaya sana! Leo hii mnaona Mbowe anafaa kuwa Mwenyekiti wa maisha kwa sababu mnamuona anafaa!

Mbona kipindi cha Magufuli mliwapinga wale wapambe wake waliomtaka aongezewe muda baada ya kumuona anafaa kama ilivyo kwa huyu Mwenyekiti wenu asiye na mbadala?

Je, na hawa wafuasi wa CCM wanaofikiri chama chao kinastahili kuendelea kutawala nchi, wana tofauti gani na nyinyi mnaofikiri Chadema haiwezi kwenda bila ya Mbowe?
 
Hahahaah huyu jamaa kujiandikia vinovel vya kisanii basi alishagajiona mwanausalama kwelikweli yani CIA, MOSAD, MIA 17 nk. 😛

Hoja zilazile za mwashambwa na tlaalaaah😎
 
Mbowe ndiye mtu sahihi kabisa kuendelea kuiongoza CHADEMA.Lissu Amefanya ukurupukaji tu katika nafasi ambayo hana kabisa Uwezo nayo
Ipo hoja inaendelezwa kutoka kwenye Makala yangu ya juzi licha ya kuijibu vizuri katika makala ile ya kwanini Tundu Lissu hana sifa ya kuwa Mwenyekiti wa Chadema taifa,



Wanajenga hoja ya kujirudia Kwamba Lissu chama kilionw anafaa kuwa Rais wa Jamhuri yenye Majeshi JWTZ, Usalama wa Taifa, TRA, TPA n.k ila mimi Yericko naona atapwaya kuwa Mwenyekiti wa chama chenye kanda 10 na majimbo kadhaa?



Wajibu wangu ni kutoa shule ya siasa na utawala bure kabisa, Narudia kuwajibu nikisema,



“Exactly, I can say, the methods za kuongoza chama cha upinzani Afrika ni tofauti kabisa na kugombea Urais kupitia chama cha upinzani Afrika ndio maana chadema imedumu licha ya vyama 28 vilivyosajiliwa kuanzia 1992 vimekufa vyote ikiwemo vyama vya juzi kama ACT kimeshindwa kujiendesha kimeamua kujisalimisha mikononi mwa Dola.



Urais kwa chama cha upinzani Afrika ni unpredictable kuupata ni 50/50 na ni tukio la siku 60 tu baada yapo mnarudi kujenga chama kwaajili ya miaka mitano ijayo, Hivyo uhakika wa uimara wa chama unatakiwa usijaribiwe, Ukuu wa chama ulindwe for Unlimited and Unwaveringly high standards, So we will protect the party with a much higher strength than anything.



Kwamaoni yangu Lissu hana sifa na ubora wa kuongoza chama kulingana na mapungufu yake mengi sana ambapo mengine niliyaeleza katika makala ile, Anayo nafasi ya kukua huko mbele akabadilika na kufaa kukiongoza chama cha siasa kinachokaribia kushika madaraka kama Chadema! Niwape siri, ndiomaana Chama kilikuwa tayari kumpa Lowasa kugombea Urais lakini KAMWE kisingeweza kumpa Lowasa uenyekiti wa Chama abadani…., Now i can tell you, Sir Mbowe will lead this party until CCM comes out of power and then its mission will be completed….



Mwezi August mwaka huu wa 2024 Lissu alitangaza kugombea nafasi ya Makamu
Kwa hiyo chadema chini ya utawala wa Mbowe mnapo panga mipango ya kuingia kwenye michuano ya uchaguzi wa Rais huwa mnaingia kujaribu tu huku mkijua hamtioshi? Nyie watu mnachezea vichwa vya Tanzania kabisa yaani baadhi ya watu wamepoteza maisha katika kuunga mkono harakati zenu kumbe nyie mnafanya tu majaribio? Kweli nimeamini ukiamua kuwa chawa hata uwe na Elimu ya PhD lazima ujizime data ujivike elimu ya Chekechea
 

Uelewa wa wabongo una shida sana mkuu, huyu naye katolea wapi habari ya kupita bila kupingwa?
 
Hapa ndio tunaona rangi zenu kuwa ni Kama hizi tu Sema huwa mnajificha pahala ili kutuhadaa
 
Utapeli unaofanyika CCM,ni uleule mnaoufanya...kiufupi wote mpo kwaajili ya maslahi yenu binafsi.......sasa mtu akigusa pale mnaponufaika mnapambana......sasa mnatofauti gani na Kessy aliyesema JPM awe aongezewe muda? Makala nyingi lakini sababu kubwa ni njaa
 
Kumbe yericko nyerere ni msisiemu? Sasa kama mnaona lissu hafai kwa nafasi hiyo ni nani anafaa nje na mbowe mnayeshadidia aendelee kuwa mwenyekiti?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…