robinson crusoe
JF-Expert Member
- Oct 22, 2020
- 762
- 1,236
Natoa wito Waziri Jaffo ajiuzulu.
Mstaafu Mwinyi aliwahi kusema kichaa akichukua nguo zako, busara ni kuchutama (loosely)
Waziri Jaffo na watalaamu wake wa mto Mara wanagoma kuchutama, na kadri wanavyogeuza ripoti wizara inazidi kupoteza pesa kwa waandishi habari na kuanza kueleza mambo ambayo siyo sayansi ya dunia hii.
Kinachoendelea ni utapeli kwa watanzania. Aibu zaidi yumo hata mkurugenzi mkuu wa NEMC ambaye ana wataalamu kibao ofisini mwake lakini yaonekana uwezo ni mdogo!!!! Je, huo ndo utendaji wa kila siku wa NEMC? Au Waziri anaikanyaga NEMC?
Waziri Jaffo huitendei haki wizara yako! Sasa tume inasema maozea ya mimea yamesababisha mafuta kuelea juu ya maji!!! Na, mvua imeleta tope la kutisha na kuua samaki!!!
Mifano iliyotolewa huko duniani, haina uhusiano wowote na hili. Hii unalazimisha taarifa ya tume ieleweke kwa wa-TZ milioni 60! Btw., kwa nini uliteua Tume badala ya kuitumia NEMC?
Uhusiano wako na huyo mwenyekiti wa tume ni upi? Yaani injinia wa mitambo anageuka kuwa mtaalamu wa mazingira!
Je, baada ya kutoa taarifa hovyo, utamfanyaje wakati siyo mwajiliwa wako? Huo ni uzembe mkubwa kwako waziri.