Ufafanuzi mbovu wa Profesa Manyele, NEMC mko wapi? Waziri Jaffo huitendei haki wizara, JIUZULU

Jaffo ni corrupt sana tangu alipokuwa TAMISEMI,ni mwizi sana
 
Niliposikia mtu anayeitwa profesa anatoa mifano ya Lake Kivu, kule kwenye volcano, nikajua ni tapeli in action! Sasa aibu tuliyonayo ni ndani yake kuwa na mkurugenzi wa NEMC ambaye ana wataalamu lakini anashindwa kutunga uongo unaoendana na ukweli. Tunaambiwa matope mengi sana! Yamesimama njiani, samaki wakakosa hewa, au sijui walijigonga?

Baada ya tukio la kwanza nilitegemea profesa huyu agome kutumwa tena kusema uongo wa hadithi mbovu kama hii kwa waandishi habari, lakini jamaa akaona sasa ana hadithi nzuri inayokubalika.
 
Bongo ukiweza kuzoataka na kufagia wewe n afisa mazingira Msaidiz

Ukijua lugha na vifaa vya maabara ya mazingira wewe n injinia wa mazingira

Tumewapa mazuzu kusimamia taaluma

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Yaani mafuta yanayoelea juu ya maji yameibuka kwenye mimea inayooza! Dah! Nimekumbuka jiografia ya darasa la 5 iliyotufundisha mafuta ardhini yavyotokana na viumbe waliokufa miaka milioni kadhaa. Leo hii kumbe haihitaji miaka milioni nyingi! Dah! Profesaaa.......
 
Huyo porofesa ripoti yake imejaa speculations, yaani vitu vya kuhisia hisia tu..........haina strong scientific backing. Siku nilipoenda kihonda viwandani manispaa ya morogoro na kukuta kuna viwanda vinatumia magogo ya miti kama nishati ya kuendesha mitambo huku msururu wa magari hadi ya tani 40 yako nje ya kiwanda yakisubiri kushusha vipande vya magogo ya miti, tangu siku hiyo hao NEMC nawaona kama aina fulani ya comedians wanaojinasibu kushughulika na swala la uhifadhi wa mazingira...
 
Jafo, Makamba na Aweso wanalindwa na udini lakini siyo viongozi hata kidogo
 
Lakini nyie ndio tumewaamini tukawapa mamlaka inakuwaje tena tume ichunguzwe na tume nyingine.. tukianza tume ichunguzwe na tume nyingine hii itakuwa sasa ni mchezo wa kupokezana vijiti na mwisho wasiku kijiti hatutajua nani anacho maana wachezaji ni wengi
 
Basi kwenye report angependekeza wizara ya nishati na bodi zake wapeleke wataalam wakaona namna ya kuyachimba hayo mafuta, maana inaonyesha pana base nzuri ya mafuta na haitahitaji gharama.
 
Manyele maana yake ni KUJINYEA…. zingatia hilo.
 

Acha kumsumbua msomi, PhD
 
Kuweka rekodi sawa.
Madhara yapo hadi kwa mifugo, mimea na binadamu.
Hayaishii kwa samaki tu!
 
Hilo la magogo ya Kihonda nasikia kuna kipindi NEMC walitaka kuchukua hatua, Waziri mkuu Pinda akakinga kifua na hiyo mimi sioni ajabu ndo viongozi wetu hao. Viongozi wetu wana bei ndogo sana!
 
Watu wa jiolojia sijui wanasemaje juu ya ugunduzi wa huyu profesa mbombezi? Udhaifu wa maelezo yake na kumbukumbu kwamba aliwahi kuwa mkemia mkuu wa serikali, ni moja ya sababu ya nchi hizi kutoendelea. Kuna watu wa hovyo kabisa, lakini wamepewa nafasi kubwa za kiofisi.
 
Waziri Jaffo huitendei haki wizara yako! Sasa tume inasema maozea ya mimea yamesababisha mafuta kuelea juu ya maji!!! Na, mvua imeleta tope la kutisha na kuua samaki!!! [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hili taifa linapitia nyakati ngumu mno
 
Tatizo siasa zinaingilia Kazi za kitaaluma kulikuwa na huja gan wazir kuunda timu, wakati nemc ipo na inawataalamu wa kutosha. LKn kisiasa akaona akae front pagë za Magazeti kwa kuunda kamati
Tulipokosea ni pale tulipoipa siasa thamani kubwa kuliko taaluma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…