Ufafanuzi na Mchanganuo Kuhusu Biashara ya Vipodozi na Urembo

Ufafanuzi na Mchanganuo Kuhusu Biashara ya Vipodozi na Urembo

Habari wana JF, napenda kuuliza na kupata ushauri toka kwenu kuhusu soko la vipodozi nataka kuchukua toka Tunduma nilete Dar kuuza kwa jumla kwa maduka nitakayochukua oda. Je naweza pata mchanganuo wa hii biashara maana ndio nataka nijalibu na mtaji wangu wa kuunga unga. Natanguliza shukrani na mawazo yenu.


Ni PM faster tufanye biashara.
 
Habari wana JF, napenda kuuliza na kupata ushauri toka kwenu kuhusu soko la vipodozi nataka kuchukua toka Tunduma nilete Dar kuuza kwa jumla kwa maduka nitakayochukua oda. Je naweza pata mchanganuo wa hii biashara maana ndio nataka nijalibu na mtaji wangu wa kuunga unga. Natanguliza shukrani na mawazo yenu
Kaka Mimi juzijuzi nilikuwa kariakoo kuulikuulizi bei ya vipodozi nataka kuanzisha biashara ya vipodozi vya rejareja. Sasa sijakuelewa unataka mchanganuo upi bse vipondozi ni vya aina Nyingi sana na vina bei tofauti. Ila kulingana na research yangu hiyo niashara inalipa ukipata wateja
 
Heri ya Mwaka Mpya wana JF

Kutokana na ugumu wa maisha na changamoto za ajira tulizonazo nimeshawishika kufanzisha biashara ndogo ya kuuza vipodozi yaani Cosmetics. Hata hivyo, kwa kuwa sijawahi kufanya biashara kabisa wazo langu hili limekumbana na changamoto zifuatazo ambazo kwa unyenyekevu naomba ushauri toka kwenu wadau.

a) Wapi naweza kupata (sourcing) vipodozi kwa bei nafuu ili niuze kwa faida.
b) Taratibu za kufungua biashara hii ni zipi ukiacha kuwa na leseni na TIN,
c) Nimetenga Tsh. 5.0 M kwa biashara hii je itatosha kuanzisha hii biashara.
d) Soko naliona lipo kwa maeneo ninayo ishi ila kama kuna lingine maeneo ya DSM unaweza kunishauri.

Nakaribisha ushauri mwengine wowote toka kwenu.

Ahsanteni.
 
Biashara ni nzuri hiyo changamoto ni kabla ujanunua vipodozi angalia kama vimeruhusiwa kisheria ili usije ukachomewa moto vipodozi.

Lakini cha ajabu wadada upenda vipodozi vilivyopigwa marufuku hivo shop nyingi uwa wanaficha hivo mtu akiitaj unamtolea.
 
Ndugu kama hujafungua hii biashara nakushauri usifungue.

~90% wanataka vilivyopigwa marufuku.
~wakipita hao jamaa TFD wakikuta kipodozi ambacho hakijasajiliwa,hakina tarehe,wanaondoka navyo na unalipa na fine.
~Hawa jamaa TFD hawatoi elimu kwa wanunuzi na hata wauzaji ili ujue nini cha kufanya.

Usiombe wakukute!!!
 
Hata ikitoka lotions mpya hadi waisajili ndio uuze, sina hamu na hii biashara.
 
Wengi hununua kariakoo! Kwani wale wa kariakoo huagiza kwa makontena kutoka nje (dubai na sehemu) nyingine nyingi tu!

Oppst fill station ya big born, kuna maduka, il wewe ingia kwenye uchochoro mmoja utakaotokezea mtaa mwingine wa nyuma! Huo uchochoro ni maarufu kwa jina la sabasaba! Ukiumaliza tu, nedna duka la kwanza mkono wa kulia kwako....linamilikiwa na dada anayeitwa sharifa. Hata kama yeye hayupo, vijana wake watakusaidia hata mawazo vipodozi gani uanze navyo kununua!

Nunua kwnza mzigo wa 60% ya mtaji wako, kisha kavipange dukani kwko, with time utaua vipodozi gani hukuchukua (base on demand ya wateja katika eneo lako)! Ukiona umepata mahitaji ya kutosha, nenda kanunue mzigo wa 40% uliobakia!

Kuwa mwangalifu na expire date hasa isiwe ya mda mfupi ujao maana usipo uza itakuwa kwako!

Kuhusu vipodozi feki, sina jinsi ya kukushauri zaidi ya kukuambia. Kila aina ya kipodozi (mwazni) chukua kiasi kidgo kwanza. Taratibu utavizoea

Kila la kheri
 
Biashara ni nzuri hiyo changamoto ni
Kabla ujanunua vipodozi angalia kama vimeruhusiwa kisheria ili usije ukachomewa moto vipodozi.

Lakin cha ajabu wadada upenda vipodozi vilivyopigwa marufuku hivo shop nyingi uwa wanaficha hivo mtu akiitaj unamtolea.

Ahsante money stuna kwa ushauri wako mzuri nitaufanyia kazi
 
K.Msese
Nashukuru kwa mawazo yako nitayafanyia kazi
 
Ndugu kama hujafungua hii biashara nakushauri usifungue.

~90% wanataka vilivyopigwa marufuku.
~wakipita hao jamaa TFD wakikuta kipodozi ambacho hakijasajiliwa,hakina tarehe,wanaondoka navyo na unalipa na fine.
~Hawa jamaa TFD hawatoi elimu kwa wanunuzi na hata wauzaji ili ujue nini cha kufanya.
usiombe wakukute!!!

Marire.
Hakuna namna ya kujua au kupata list ya vipodoz ambavyo vimehalalishwa ili kuepuka kuuza hivyo ambavyo TFDA wanakataza
 
Habari wana JF, jamn napenda kuuliza ukitaka kufungua duka la biashara ya vipodozi kima cha chini kwa kuanzia inaweza kuanzia na shilingi ngapI? Na pia biashar ya chips ambazo ni standard unatakiw uwe na mtaji wa shilingp? Msaada wenu jamn!
 
Mkuu vipodozi kiwango cha kuanzia inategemea zaidi na demand ya hiyo huduma yako pia na kiwango chako cha mwisho ulichonzcho ukiachana na kodi ya pango, mtaji anaotakiwa kuanza nao mfanya biashara wa dar, si sawa na mtaji utakao mlazim kuwa nao mtu wa Zanzibar!

Mtaji wa chipsi nao hauhitaji mambo mengi unapaswa kuanza na sahani chache, baada ya hapo utajiongeza mwenyewe kutokana na kuongezeka au kupungua kwa wateja wako!
 
Kwahiyo mkuu mtaji wa vipodoz unawez kuwa kam shilling ngp kw makadilio?
 
Kiongozi mi sijajua ww unahitaji kuwekeza wapi

Ila kwa duka la kawaida huku DAR uswahilini unawza kuanza na mil 2 baada ya hapo utaongeza mtaji kutokana na bidhaa wanazohitaji wateja wako!

Nakutakia mafanikio mema mkuu!
 
Kwa kuongezea kuwa makini sana na vipodozi fake jamaa wa TFDA wasije kukumaliza. Kila la kheri mkuu.
 
Kwa kuongezea kuwa makini sana na vipodozi fake jamaa wa tfda wasije kukumaliza kila la kheri mkuu

Yah! Ni kweli ila hawa huwa wanafatilia sehem na sehem mfano maeneo ya Mwenge au sinza hawakauki, kila baada ya mwaka wanapitiapitia. Ukiwapoza wanatulia!
 
Pamoja na yote hii biashara itakupa faida kwa wakati. Endapo utafanya utafiti wakazi wa eneo husika, wanatumia aina gani ya bidhaa inayoendana na hali yao ya kiuchumi. Nasema hivyo kwa sababu mara nyingi bidhaa zinazotumiwa na watu wa mji fulani zinaweza kuwa tofauti na za mji mwingine, hii ni kutokana na kila kipodozi kina bei yake kutokana na ubora wake. Kwa mfano, usitegemee bidhaa zitakazotumiwa au kupendwa na wakazi wa Masaki zinaweza fanana na zile za wakazi wa Tandale.

Usiingie kichwa kichwa lazivyo bidhaa zitasumbua kuuzika na utaiona hii biashara inakunyima pumzi!
Naomba niishie hapa mkuu!
 
Na milioni 30 nataka kufungua duka la vipodozi(clasic cosmetic),sina uzoefu na biashara hii,naomba msaaa kwa yoyote mwenyeuelewa kuhusu ya fwatayo:-
1.Vinapatikana vipi kwa bei rahisi?
2.Kwa mtaji huu naweza kuagiza mwenyewe? na kama inawezekana vinapatikana nchi gani?
3.Faida,hasara na risk zake
4.Soko la biashara hii kwa ujumla wake? maana nimepanga kufungulia sinza au kinondoni
5.Naweza kupata kampuni ya kuuza brandi zake?kama ina wezekana njia za kuwasiliana nikipata nitashukuru
Nitashukuru kwa msaada wenu atakama kunamengine ya muhimu nimesahau na muhimu kwa mimi kufahamu mkinijuza nitashukuru,Nawakilisha
 
Dah! Mkuu kwa huo mtaji ningeupata mimi ningefungua duka la vifaa vya ujenzi. Vipodozi ni biashara nzuri ila ina risk sana , hasa wakija wakaguzi na ujue pia asilimia 90 ya vipodozi vinavyouzika ni vile vilivyopigwa marufuku na mamlaka ya chakula na dawa Tanzania!

Wengi huletewa mzigo toka zambia na kongo na watu wenye mitaji mikubwa ,wanaojuana na wakubwa serikalini
ukitaka kufungua , jaribu kufanya utafiti na mwenge!

Nakutakia maamuzi yenye mafanikio mema!
 
Wakuu habari za mida?

Nadhani tu wazima wengiwetu, na kwawenye matatizo ya Afya nawatakia uponaji wa haraka ili tuendelee na mishe zeru necessario. Ndugu yenu kwamuda mrefu nimekua na ham ya ku change biashara kutoka Hard wear ambayo ndio nadili nayo kwa sasa nakuangalia issue nyingine.

Sasa katika fikra zangu limenijia wazo la cosmetic, hii biashara nimeonelea kwa huku nilipo inasoko sana. Lakini tatizo sina uzoefu na biashara hiyo (vipodozi) hivyo basi ninaomba kwamwenye uzoefu na ufam kuhusu biashara hiyo. Upatikanaji wake, kiwango gani cha msingi kinafaa kuanzia, changamoto zake namengine mengi kutoka kwenye biashara hiyo. Natanguliza shukrani zangu kwenu wajasilia mali wenzangu.
 
Back
Top Bottom