Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mimi nina client wangu anayefanya biashara hiyo. Ila vipodozi vyake ni ya asilia anatengeneza mwenyewe na si za nje. Kama utakuwa na interest ni pm, nitakupa contact zake.
Hakuna shida mkuu 😉shukran dr. sema mie naitaji vipodoz vya kawaida hiv ambavyo vinatengenzwa viwandan
Huwa nasikitika sana ninapoona mtu anaanzisha thread kama hii but hakuna mtu anayechangia , unakuta mtu yuko bissy anachangia siasa kutwa nzima thread imejaa watu wanajadili zito, mbowe, JPM, baba ridh1 etc huku tunaacha kuchangia ishu kama hizi za maana ili tujikwamue, ni hatari sana.Ujasiliamali ndiyo maisha ya leo, ukizingatia kuwa ajira ni janga kwa Tanzania na Dunia kwa ujumla. Nisiwachoshe sana kwa maneno mengi mnayoyajua.
Nina pesa kiasi cha Tshs milion 5(Tshs. 5,000,000/-). Ambayo ninafikiria kuitumia kuanzisha biashara ya "VIPODOZI" DODOMA MJINI, ili wife apate pakutokea badala ya kukaa nyumbani tu. Hapa lengo ni kuchanga nguvu ili tujikwamue kwa namna moja ama nyingine.
Ninaomba ushauri wenu wadau kwa mambo yafuatayo:-
1. Je, kiasi hiki cha pesa kinafaa kwa kuanzia?
2. Na kama 1 ni ndiyo, Je vitu gani vya mhimu kuvifanya ktk kuanzisha hiyo biashara? (namaanisha kama kuna documents za mhimu ninazopaswa kuwa nazo kama watu wa afya i.e maduka ya dawa)
3. Kama 1 ni ndiyo, ni wapi naweza nunua mzigo(bidhaa) nami nikapata chochote kama lengo lilivyo?
NB: Ushauri wako ni mhimu sana, pia kama hicho kiasi kitakuwa hakitoshi nishauri ni kiasi gani niongeze/nitafute ili kufikia lengo.
NAWASILISHA.
Kiongozi umelaumu wenzio nawee umafanya jambo hilohilo. Ungeanza na kumshauri huyo jamaa kisha ungewalaumu hao watu.Huwa nasikitika sana ninapoona mtu anaanzisha thread kama hii but hakuna mtu anayechangia , unakuta mtu yuko bissy anachangia siasa kutwa nzima thread imejaa watu wanajadili zito, mbowe, JPM, baba ridh1 etc huku tunaacha kuchangia ishu kama hizi za maana ili tujikwamue, ni hatari sana.
Nabaki kucheka tu maana na wewe umemlaumu aliyewalaumu, nawe ungeanza kumshauri mleta uzi kisha ukamlaumu jamaa. Kwa upande wangu sina uzoefu na hili hivo nami nimeingia kusikiliza ushauri pia karibuni wadau kuchangia tufaidike wote.Kiongozi umelaumu wenzio nawee umafanya jambo hilohilo....Ungeanza na kumshauri huyo jamaa kisha ungewalaumu hao watu
Ehee haya ndio maneno yanayotakiwa, mkuu Magnificient ubarikiwe sana kwa elimu uliyoitoa hapa maana hujui tu imesaidia wengi kaka. Mimi binafsi nitakutafuta kupitia PM ili unitumie hizo documents maana nategemea miezi kama mitano ijayo nianze hii biashara, ubarikiwe sana kwa msaada wako kwa jamii.Mimi nafanya biashara ya vipodozi, pia ni mtaalam wa masuala ya urembo, vipodozi na afya. Kwa sasa siuzi tena kupitia duka langu bali naviuza kwa njia zingine na nashukuru Mungu mambo mengi nayajua vizuri na biashara inaendelea vizuri.
1. UTARATIBU WA KUANZIA
Kwanza inabidi upate eneo zuri na lenye nafasi ya kutosha kuweka vipodozi vyako na kufanya biashara hii. Jengo liwe na mwanga wa kutosha na liruhusu mzunguko mzuri wa hewa
Pili inabidi uwe na namba ya mlipa kodi (TIN) kutoka TRA kwa ajili ya kulipia kodi biashara yako na kupatia leseni manispaa.
Tatu, inabidi uende wilayani/manispaa unakotaka kufanyia hiyo biashara au ofisi za TANZANIA FOODS AND DRUGS AUTHORITY (TFDA) kama ipo karibu yako. Hapo utaonana na watu wanaohusika na leseni za biashara za vipodozi kwa ajili ya ukaguzi wa eneo unalotaka kufanyia biashara ya vipodozi. Watakutoza ada ya ukaguzi.
Wakikagua na kukubaliana na eneo lako basi watakutaka ulipie kibali na leseni ili uweze kuruhusiwa kufanya biashara hiyo katika eneo hilo.
Taratibu zote za serikalini zikikubali basi hapo sasa utakuwa na baraka zote kuanza biashara hii.
2. MTAJI
Hakuna kiasi maalum cha mtaji ambacho unatakiwa kuanza nacho, cha msingi ni wewe mwenyewe unajiwezaje, duka lako ni size gani na unataka liwe la hadhi gani na kuwa na vitu gani.
Gharama kubwa zipo kwenye kodi ya jengo la biashara, shelf na makabati ya aluminium na vipodozi vya bei kubwa kama vile perfume original
Kwa hiyo nashindwa kusaidia kiasi cha mtaji cha kuanzia, lakini kwa kununua baadhi ya vipodozi vya kuanzia tu peke yake na kwa duka la ukubwa wa wastani basi million 5 inatosha. Cha msingi kuwa na plan kubwa na ya muda mrefu lakini unaianza mdogo mdogo bila kusimama.
3. CHANGAMOTO
Hakuna biashara isiyo na changamoto. Changamoto kubwa kwenye biashara ya vipodozi ni matakwa ya wateja na serikali.
Wateja wengi hupenda vipodozi ambavyo serikali imevipiga marufuku, feki/copy na vya bei ya chini kwa kuwa ndivyo huwaletea matokeo wanayoyataka haraka haraka japokuwa vinawaharibu sana baadae na kuathiri afya zao
Unatakiwa kutoa risiti kwa kila kipodozi utakachouza na kutunza kumbukumbu vizuri kwa ajili ya makadirio ya kodi
Ni marufuku kuweka vipodozi na bidhaa ambazo hazitakiwi, hata kama ndivyo vina wateja wengi na kukuletea faida kubwa
Kuna ukaguzi wa mara kwa mara na muda wowote unaweza ukapoteza biashara yako kama utakamatwa umeweka bidhaa zilizokatazwa
Kwa maelezo zaidi na ushauri wa kitaalam na kibiashara nawakaribisha ndugu na marafiki zangu nyote ambao mngependa kufanya biashara hii nzuri tuwasiliane ili niwape na documents zake muweze kuanza na kuendesha biashara hii vizuri.
Nipo Dar mkuu mm nauza cash kukopesha naona ni hasara tupu.Uko sehemu gani? Kuna rafiki yangu amewahi kufanya kazi hiyo maofisini akapata hasara sana kutokana watu kutokulipa pesa kwa wakati, japo wanashauri kushindwa kwa mtu mwingine sio kushindwa kwako. shida nyingine maofisini wamezoea kukopeshwa sio watu wa cash.
Nawe waeza toa mchango wako mkuu sio mbaya.Subiri waje[emoji124] [emoji124] [emoji124]
Kwa Dar itakulipa, ila jitahidi kuwa serious na biashara yako pamoja na kujiwekea malengo utafanikiwa. Kuwa social ila usijaribu kutumbukia kwenye mahusiano ya kimapenzi humo maofisini. Kila jambo ukilifanya kwa uthabiti na nia unafanikiwa mwisho wa siku utakua na framu zako.Nipo dar mkuu mm nauza cash kukopesha naona ni hasara tupu
Nashukuru kwa ushauri wako mkuu [emoji120] [emoji120] ila bado ninaomba mawazo jinsi ya kuanza.Kwa Dar itakulipa, ila jitahidi kuwa serious na biashara yako pamoja na kujiwekea malengo utafanikiwa. Kuwa social ila usijaribu kutumbukia kwenye mahusiano ya kimapenzi humo maofisini. Kila jambo ukilifanya kwa uthabiti na nia unafanikiwa mwisho wa siku utakua na framu zako.