Ufafanuzi na Mchanganuo Kuhusu Biashara ya Vipodozi na Urembo

Ufafanuzi na Mchanganuo Kuhusu Biashara ya Vipodozi na Urembo

Ndugu msomaji wetu, mfanyabiashara na Mjasiriamali.

Leo tunataka kukujuza juu ya undani wa biashara ya vipodozi hapa Tanzania. Biashara ilioyoenea sana lakini wengi kwa kutokutambua, huifanya bila kufuata utaratibu..na matokeo yake huwa si rafiki hata kidogo kibiashara.

ELIMU hii, kama si wewe, basi inaweza kumsadia ndugu, rafiki au jamaa.

KARIBU SANA.

Kwa Tanzania, na kwingineko duniani, vipodozi hujumuishwa ndani ya kundi kubwa la bidhaa za afya (Healthcare products). Biashara ya vipodozi ni moja kati ya biashara zinazodhibitiwa kisheria (regulated business), na usimamizi wa biashara ya bidhaa hizi kwa Tanzania bara unafanywa na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA).

Biashara hii ya vipodozi pia ni moja kati ya biashara zilizoenea sana hapa nchini; karibu kila mtaa (hasa maeneo ya mijini), hutapita hatua chache bila kukuta duka la vipodozi. Na ni biashara ambayo soko lake ni kubwa na linaendelea kukua siku hadi siku.

Kwa bahati mbaya, maduka haya mengi yamekuwa yanauza vipodozi ambavyo havijasajiliwa na TFDA, ukiachilia mbali maduka yenyewe pia mengi kutokutambuliwa na Mamlaka.

Na kama nilivyogusia hapo juu, biashara hii ni “regulated business” hivyo kwa mujibu wa sheria na kanuni za Tanzania, kuuza vipodozi visivyosajiliwa ama kuuza vipodozi bila kibali ni kosa kisheria. Mimi na wewe ni mashaidi kwani mara nyingi tumeona na kusikia maduka mengi ya vipodozi yakifungwa na bidhaa kuharibiwa na Mamlaka husika, sababu mojawapo ikiwa ni kufanyika kwa biashara hii kinyume na taratibu.

Mbali na uvunjaji wa sheria, pia ni muhimu tukajua ya kwamba, uuzaji huu wa VIPODOZI visivyosajiliwa una madhara makubwa sana yakiwemo yale ya kiafya kwa jamii yetu ya watanzania.
Kwa haraka haraka, inaweza kuonekana kwamba kukwepa kufuata utaratibu na kuifanya biashara hii kinyemela haina shida sana, LAKINI shida ipo, tena kubwa sana; mojawapo ni hiyo ya kukamatwa kwa kuvunja sheria na biashara yako inaweza ikawa ndo mwisho wake.

Njia pekee ya kuepukana na haya yote ni kuhakikisha UNARASIMISHA biashara yako.

Sasa basi, pamoja na kupata TIN na lesseni ya biashara, mchakato wa urasimishaji wa biashara ya vipodozi una mambo mengine mawili (02) muhimu ya kufuata.

(1) JAMBO LA KWANZA: Kusajili bidhaa zako, ama kuhakikisha unauza bidhaa zilizosajiliwa na TFDA.
(2) JAMBO LA PILI: Kupata kibali cha biashara kutoka TFDA.

Ukifanikiwa kuyafanya mambo haya mawili, basi utafanya biashara yako raha mustarehe bila bugdha yoyote ile.

Hata hivyo, utafiti wetu mfupi ulionesha kwamba, UGUMU uliopo katika zoezi zima la usajili wa bidhaa hizi za afya pamoja na upatikanaji wa vibali ndiyo umekuwa sababu kuu ya wajasiriamali na wafanyabiashara wengi kushindwa kusajili bidhaa zao na kurasimisha biashara zao pia.

Kufuatia changamato hii, tumeona, kama kampuni ni vyema kufanya juhudi za dhati kutoa elimu, ufafanuzi na msaada wa kitaalamu utakao kusaidia wewe msomaji wetu na mfanyabiashara katika zoezi zima la usajili wa biashara yako na bidhaa zako.

Makala hii ni ndefu sana, hatuwezi kuiweka yote hapa, hata hivyo usijali ndugu msomaji wetu tunanjia mbili za wewe kuweza kuipata kwa urefu wake;

(1) Ya kwanza, fuata hii link inakupeleka moja kwa moja.. http://pharmaregtz.com/sites/default/files/Mambo Makuu 2 lazima kuyajua..pdf

(2) Ya pili-- Comment email address yako au tutumie kwenye sms au email yetu ya support@pharmaregtz.com nasi tutakutumia makala yote ndani ya muda mfupi. Pia, tukipata email yako tutakuunganisha moja kwa moja na mtandao wetu wa email na hivyo utakuwa unapata taarifa mbalimbali zitakazo kusaidia wewe, au jamaa yako katika biashara hii ya VIPODOZI na bidhaa nyingine za afya (kama vile dawa, vifaa tiba na vyakula).
 
Punguzeni siku za kupata kibali cha kuingiza mafuta kutoka nje ndio maana mengi yanaingia kinyemela siku 45 upate kibali na umelipa kwa USD kwa kila item wakati wenzenu SA wanatoa bure siku ya pili unapata biashara zinakua kwa mtindo huo urasimu unaongeza kiwango cha watu kuvunja sheria mimi siuzi hayo ila vijana wanaobeba mafuta naona tabu wanayoipata.
 
Habari zenu wakuu,

Husika na kichwa cha habari hapo juu, nimewaza nifanye biashara ya urembo i.e. mikufu, hereni, shanga, other wearables et al za kina dada kwa jumla na reja reja maeneo ya Kkoo.

Naombeni ushauri wenu wapi naweza pata mzigo mzuri kwa bei nafuu ili nipate faida nzuri nikiuza hapo Kkoo (Uwezo wa kusafiri china na kwingine kufwata mzigo ki ukweli bado bado, ila taratibu tutafika)

Naomba kwa wanaojua faida na changamoto za hii biashara kama kuna umuhimu wa kupata goli la kuuzia maeneo husika. Uzuri mmoja niliopenda hii business ni portability ya mzigo (haichukui space kubwa so lower storage costs).

Karibuni Wandugu.
 
Punguzeni siku za kupata kibali cha kuingiza mafuta kutoka nje ndio maana mengi yanaingia kinyemela siku 45 upate kibali na umelipa kwa USD kwa kila item wakati wenzenu SA wanatoa bure siku ya pili unapata biashara zinakua kwa mtindo huo urasimu unaongeza kiwango cha watu kuvunja sheria mimi siuzi hayo ila vijana wanaobeba mafuta naona tabu wanayoipata..

Mkuu Isanga family,

kwanza kabisa tukushukuru kwa comment yako, Pili naomba utupe nafasi tujieleze hasa sisi ni wakina nani na tunafanya.

Kama inavyojieleza hapo juu, kampuni yetu inajulikana kwa jina BB Pharma Consultancy Limited, ni kampuni inayotoa ushauri na msaada wa kitaalamu kufanikisha usajili wa bidhaa na huduma za afya hapa nchini. Katika safari yetu ya career tumewahi kufanya kazi Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania. Moja ya changamoto tulizoziona ni kuchelewa kukamilika kwa usajili wa bidhaa za afya (Dawa, vifaa tiba, vipodozi, vyakula n.k) kulingana na muda uliyowekwa na Mamlaka yenyewe.

Moja ya sababu kubwa inayopelekea uchelewaji huu (delays) ni mapungufu yaliyo kwenye nyaraka (documents) zinazopelekwa kwa Mamlaka kwa ajili ya usajili wa bidhaa hizi. Mapungufu haya yanatokana hasa na kutokueleweka kwa undani mahitaji (requirements) za Mamlaka kwa ajili ya usajili wa bidhaa.

Summary:

Sisi tuna translate requirements za Mamlaka kwa wateja wetu (ambao ni Manufacturers, Makampuni na wafanyabiashara binafsi) pamoja na kuwapa mwongozo unaowawezesha kupata usajili wa bidhaa zao kwa wakati.

Baada ya maelezo hayo, naomba sasa nikujibu swali lako... Sisi kama kampuni hatuna uwezo wa kubadilisha timelines zilizowekwa na Mamlaka. Isipokuwa, sisi tunawasaidia wateja wetu kufanikisha usajili kwa wakati.

Hata hivyo, nikusaidie kitu kimoja;

Kwa mujibu wa taratibu za Mamlaka, upatikanaji wa vibali vya kuingiza dawa, vipodozi na hata vyakula ni ndani ya masaa 48 unakuwa umeshakipata kibali. LAKINI, vibali hivi hutolewa kwa bidhaa ambazo zimeshasajiliwa tayari. Na zoezi la usajili wa bidhaa hizi ndiyo kama nilivyoligusia kwenye maelezo yangu hapo juu. Hii inaamanisha nini?? kabla hujawaza kuingiza mafuta yako hapa nchini, lazima kwanza uyasajili. Baada ya hapo utaweza sasa kuwa unafanya importation kwa kadri utakavyo mwnyewe na vibali ni ndani ya masaa 48 tu unakuwa umepata.

Kama utakuwa na swali, au unahitaji maelezo mengine karibu sana mkuu.

Asante.
 
Okay, sawa nimekuelewa Mkuu nimechukua contact zako ntatuma sample ya mafuta ya mgando sijajua unahitaji kupeleka sample kopo ngapi hapo umesema kibali kinapatikana ndani ya masaa 48 na gharama zako zipoje na kuhusu madawa ya binadamu na chemicals za migodini hizo pia vibali vyake unatoa?
 
Okay sawa nimekuelewa Mkuu nimechukua contact zako ntatuma sample ya mafuta ya mgando sijajua unahitaji kupeleka sample kopo ngapi hapo umesema kibali kinapatikana ndani ya masaa 48 na gharama zako zipoje na kuhusu madawa ya binadamu na chemicals za migodini hizo pia vibali vyake unatoa?

Ndugu Isangi Family,

Kwanza kabisa niendelee kukushukru kwa kuvutiwa na mada hii. Naomba nikutaarifu BB Pharma Consultancy Ltd hatutoi vibali wala usajili bali tunasaidia wafanyabiashara (mfanyabiashara) wa bidhaa tajwa hapo juu kupata usajili na vibali kutoka mamlaka huska (TFDA na mamlaka zingine) ili kumuwezesha kufanya biashara kiharali na kirahisi. Nafikiri hapo utakuwa umeelewa kazi yetu hasa nini katika mchakato huu.

Kuhusu dawa za binadamu:

Ndio, kampuni yetu inatoa ushauri elekezi juu ya usajili and uendeshaji mzima wa biashara ya dawa zote za binadamu na za mifugo.

Kemikali (chemicals for industries and mining):

Huduma hii hatujaanza kutoa kwa sasa lakini mda sio mrefu tutaanza.

Gharama:

Gharama zetu ni rahisi sana (affordable), kwa vile umesema umechukua mawasiliano yetu basi tutawasiliana na kuona jinsi ya kufanya kazi pamoja.

Ahsante na karibu sana.
 
Nahitaji kufanya biashara ya duka la vipodozi je ?niwe na mtaji wa sh ngapi na naombeni idea kwa wenye ujuzi maana sijawai kufanya hii biashara na naipenda mi niko mkoani Mbeya.
 
Habari zenu wakuu

Husika na kichwa cha habari hapo juu. Nimewaza nifanye biashara ya urembo i.e. mikufu, hereni, shanga, other wearables et al za kina dada kwa jumla na reja reja maeneo ya Kkoo.

Naombeni ushauri wenu wapi naweza pata mzigo mzuri kwa bei nafuu ili nipate faida nzuri nikiuza hapo Kkoo (Uwezo wa kusafiri china na kwingine kufwata mzigo ki ukweli bado bado, ila taratibu tutafika)

Naomba kwa wanaojua faida na changamoto za hii biashara, kama kuna umuhimu wa kupata goli la kuuzia maeneo husika. Uzuri mmoja niliopenda hii business ni portability ya mzigo (haichukui space kubwa so lower storage costs).

Karibuni Wandugu.
HAbari naweza kukuunganisha na supplier wa bidhaa za urembo bei nafuu toka uarabuni nichek inbox.
 
Naomba mwenywe uelewa na biashara hii anipe dondoo nataki kufungua kibanda mtaji nilionao ni million1 nifikiri kufata mzigo Uganda japo sijawai kufika, wala cjui maduka pamoja na bei za huko na je nilileta mzigo inalipa mm npo mwanza Msaada wenu.
 
Bora kutafta furasa kama hizi kuliko kuwaza kufanya wanayofanya wale wanywa gongo, safi sana ngoja waje wakupe ujuzi.
 
  • Thanks
Reactions: RRD
Tatizo LA vipodozi usipouza yale yasiyotakiwa hupati ela mzuri
 
Habari za leo ndugu zangu! Nina imani mko salama kwa upendo wa Allah. Ninaomba msaada wa kujua biashara ya vipodozi inalipa endapo nitaifanya kwa rejareja??? Vipodozi vinapatikana wapi na kwa bei gani kwa jumla kulingana na aina na ujazo wake. Nini changamoto kuhusu biashara ya vipodozi, pia maeneo gani yanafaa zaidi kufanyia biashara hii ili kuweza kupata faida? Nina mtaji wa sh 2M je inatosha kuanzisha biashara hii? Natanguliza shukrani zangu za dhati kwenu wadau!! Thnx
 
Mkuu, search humu ndani kuna nyuzi nyingi sana zinazungumzia maswala ya biashara ya vipodozi

-Kama upo Dar, vipodozi kwa jumla unapata kariakoo
- huwezi kuuliza vipodozi vinapatikana kwa bei gani bila kuwa specific maana kuna vipodozi vingi
- changamoto kubwa ni kwamba vipodozi vinavyopendwa zaidi na watu ndio vipodozi ambavyo serikali inakataza
- Biashara hii ni kama biashara nyingine yoyote ile, inahitaji sehemu yenye mzunguko wa watu au sehem yenye saloon nyingi za kike ili wateja walengwa wawe wateja wanaoenda saloon au wakitoka saloon hata wamiliki wa saloon pia

Maswali mengine angalia threads zilizopita
 
Back
Top Bottom