JumaKilumbi
JF-Expert Member
- Sep 7, 2022
- 432
- 507
Na Jumakilumbi,
15.10.2022
Kile kilichotokea siku ya tarehe 14/10/2022, huko Kagera siku kumbukizi ya miaka 23 tangu alipotutoka Mzee wetu na Mkombozi wetu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kimezua mjadala mzito kwa waumini wa dini ya kikristo na wakosoaji wa serikali na Rais Samia, hapa nimekusudia kutoa ufafanuzi mfupi wa kitendo kile.
UFAFANUZI
Kiti cha rais ni nembo ya mamlaka ya Rais, mahali popote nchini awapo kwa shughuli rasmi ya kiserikali kiti chake huwepo kuashiria urasmi wa shughuli hiyo.
Kabla ya yote jambo mambo kadhaa lazima tuyaelewe na tuyakubali
* Rais Samia ni Muislam, lakini ni rais wa waTanzania wote.
* Rais huvaa kofia nyingi, ni M/kiti wa CCM, Rais wa Nchi, Muislam (binafsi yake), ni Mke (kwa mumewe) na ni Mama (kwa wanawe).
Shughuli ile ilimlalizimu kuingia kanisani katika ibada ambapo yeye kama Muislam kanisani si mahala pake pa ibada, ila yeye aliingia kwa kofia ya KIONGOZI WA NCHI, na hili lilibainishwa wazi kwa uwepo wa kiti chenye nembo ya bibi na Bwana.
Hivyo kuingia kwake na kiti chake kanisani haikuwa dharau kwa dini ya kikristo kama inavyotafsriwa na wakosoaji wake, bali ni ishara ya kofia aliyoingia nayo - Kofia ya Urais.
Maswali yaulizwayo mara kwa mara
1) Mbona Magufuli hakuingia na kiti Msikitini?
Misikitini hakuna viti, ila kuna makapeti… na kama kungekuwa na kapeti rasmi la Rais (lenye nembo ya bibi na bwana) nina hakika angeingia nalo kuonesha kofia aliyoingia nayo
2) Mbona Magufuli hakuingia na kiti Kanisani?
Hayati alikuwa Mkristo, hivyo aliingia kanisani kwa kofia yake binafsi kama Mkristo na si kama Rais.
3) Mbona Rais Samia hakuingia na kiti Msikitini?
Kwakuwa yeye ni Muislam, aliingia Msikitini kwa kofia ya Uislamu wake.
Pia Misikitini hakuna viti, ila kuna makapeti. Kama kungekuwa na kapeti rasmi ya Rais bila shaka angeingia nalo.
3) Mbona Makamu wa Rais Dr. Mpango hakukalia kiti kama cha Rais?
Kiprotokali hatuna kiti rasmi chenye nembo ya kimamlaka kwaajili ya Makamu wa Rais, ila kingekuwepo angeingia nacho.
Pia Dr. Mpango ni Mkristo, ameingia kwa kofia ya Ukristo wake.
NB: Haya ni maoni yangu Binafsi na ninawajibika kwayo.