UFAFANUZI: Rais kuingia na kiti chake Kanisani Mkoani Kagera

UFAFANUZI: Rais kuingia na kiti chake Kanisani Mkoani Kagera

Hayo maelezo yanamkanganyiko;

Kama kanisani kuna viti tayari, basi ni heshima na staha kwa watu wa imani ile endapo utakalia viti walivyokuandalia, hata kama unacho cha kwako
Mkuu kama umesoma vizuri nimejaribu kueleza maana ya kuingia na kiti.

Rais hakwenda yeye binafsi, alikwenda kwa kofia ya Urais. Na hilo limetanabaishwa na uwepo wa kiti cha Rais.
 
Pamoja na maelezo ya kina, sijakubaliana na utetezi/ ufafanuzi huo kwa mantinki hii, Nyerere day kama ilivyo ni public holiday, ni tikio la kitaifa na tukio la kiserikali.
Nafikiri namna bora zaidi ya kuienzi siku hii ni kuandaa sehem tofauti na nyumba ya ibada, tukio liendeshwe katika sura ya shughuli ya kitaifa, hili la kanisani liachwe kwa familia, binafsi naona ni utaratibu wa kifamilia zaidi.
Lakini pia, tunasema serikali haina dini, isipokuwa, wananchi wake wana dini, kwa mantiki hii, yafaa tukio la kiserikari liendeshwe kiserikali kwa namna yake iwe kwa njia ya kongamano, zipo namna nyingi sana za kuenzi siku hii kitaifa/ kiserikali.
 
Kila anapokwenda Rais lazima mamlaka yake yaomekane. Hapa umetudanganya Kwa makusudi au Kwa kutaka kumbeba Huyo unayemtetea. Kama Magufuli hakwenda na kiti kanisani na sababu unayotoa ni kwamba Magufuli alikuwa Mkristo,
Mkuu msingi upo kwenye shughuli inayofanyika, Hayati Magufuli alikwenda ibadani hasa siku za Jumapili hivyo alikwenda yeye na si Rais. Hakukuwa na haja ya kuonesha mamlaka ilhali amekwenda yeye binafsi.
Sasa hayo mamlaka yake alikuwa anayaacha wapi?
Hili ni swali la kipumbavu sana, hebu fikiria.
Kama Kila anakokwenda Rais lazima yawepo Mamlaka Choo anachotumia kina nembo ya Rais?
Na hili pia,
Kwenda kuonyesha supremacy kwenye mamlaka nyingine ni uchokozi.
Lengo si kuonesha Ukuu mkuu, lengo ni kuonesha aliyekwenda si Samia, aliyekwenda ni Rais wa Tanzania na hiyo ndiyo sababu ya uwepo wa kiti cha rais…
Kiti cha rais sio cha Samia, ni cha yeyote anayeshikilia mamlaka ya Rais.
Samia yeye binafsi hana sababu za kwenda kanisani sababu yeye ni muislam, ila kama rais, anaweza kwenda kwa kofia ya Urais.
Kama kweli Rais ni Mkuu wa Kila mahali Kwa nini alipoingia kanisani Askofu hakumpisha kiti?
Umebadili maana yangu, lengo si kuonesha Ukuu, lengo ni kuonesha aliyekwenda si Samia, bali ni RAIS SAMIA.
Imeandikwa ya Kaisari mpe Kaisari na ya Mungu mpe Mungu, Sasa yeye anapoingia kwenye ibada na Mamlaka ya kidunia anataka Mungu ndo amnyenyekee yeye?
Umepoteza maana,

Ulipopotea ni pale ulipodhani kiti kuonesha Ukuu juu ya kanisa, hapana.

Kiti ni kuonesha kofia aliyoingia nayo.
 
Naona binafsi hakuna tatizo coz kwanza ijumaa hyo sio siku ya ibada kama sijakosea !!(kama ni wrong mniambie) basi kukaa hapo hakuna tatizo lolote maana imekuwa kama siku ya hafla kama siku ya kufungisha ndoa tu hutumika kama emergency na occasional events ,ingekuwa siku ya ibada kama kawaida ingekuwa tofauti.

Hata sisi swala ya maiti tunaswali random sio katika utaratibu wa kawaida ,hata ishu ya kufungisha ndoa ndo maana siku iyo mtu yeyote anaweza kuingia hata mpiga picha.
 
Pamoja na maelezo ya kina, sijakubaliana na utetezi/ ufafanuzi huo kwa mantinki hii, Nyerere day kama ilivyo ni public holiday, ni tikio la kitaifa na tukio la kiserikali.
Nafikiri namna bora zaidi ya kuienzi siku hii ni kuandaa sehem tofauti na nyumba ya ibada, tukio liendeshwe katika sura ya shughuli ya kitaifa, hili la kanisani liachwe kwa familia, binafsi naona ni utaratibu wa kifamilia zaidi.
Lakini pia, tunasema serikali haina dini, isipokuwa, wananchi wake wana dini, kwa mantiki hii, yafaa tukio la kiserikari liendeshwe kiserikali kwa namna yake iwe kwa njia ya kongamano, zipo namna nyingi sana za kziwe uenzi siku hii kitaifa/ kiserikali.
Samahani mkuu kwa kujua hili! Sina maana mbaya ila tambua lazima nyerere aenziwe kanisani kwa vile ndie aliyeupigania vita ukatoliki hapa Tanzania mpaka ukasambaa kila kona ..sina maana mbaya ila nakupa sababu tu..
 
Na Mpango ni mkristo kwann hajakaa kwenye benchi mpk aingie na kiti
Ni dharau tu, na mbwembwe za sisi Wakristo. Upande wa pili, likifika suala la imani, wote huwa sawa.
Nakumbuka mwili wa Hayati, DR Omari Juma (Makamu wa Rais) ulipofika Zanzibar, uliingizwa msikitini ukiwa kwenye (sjui jina lake kamili) lile kama machela, lililokuwa linatumiwa na watu wengine. Likafunikwa na kama shuka hivi, likiwa limechakaa, na limetoboka toboka
Hapa, nimetolea mfano wa wenzetu Waislamu, kwenye ibada hawana ubaguzi, wala cheo chako!
 
Naona binafsi hakuna tatizo coz kwanA ijumaa hyo sio siku ya ibada kama sijakosea !!(kama ni wrong mniambie) basi kukaa hapo hakuna tatizo lolote maana imekuwa kama siku ya hafla kama siku ya kufungisha ndoa tu hutumika kama emergency na occasional events ,ingekuwa siku ya ibada kama kawaida ingekuwa tofauti.

Hata sisi swala ya maiti tunaswali random sio katika utaratibu wa kawaida ,hata ishu ya kufungisha ndoa ndo maana siku iyo mtu yeyote anaweza kuingia hata mpiga picha.
Naam, na msingi upo hapo Mkuu, shukran.
 
Samahani mkuu kwa kujua hili! Sina maana mbaya ila tambua lazima nyerere aenziwe kanisani kwa vile ndie aliyeupigania vita ukatoliki hapa Tanzania mpaka ukasambaa kila kona ..sina maana mbaya ila nakupa sababu tu..
Kwa misingi ipi unayotumia kusema kuwa nyerere aliupigania ukatoliki mpaka kuenea Tanzania kila kona? Kwako wewe, kuhistoria unamaanisha ukatoliki uliibuka na kuanza kusambaa miaka ya 1960's?
Kurudi katika hoja yangu, nimekubaliana na utaratibu wa kumuenzi kanisani, lakini, hilo lifanyike kifamilia katika utaratibu unaotumika kulingana na dhehebu lao.
 
Kwa misingi ipi unayotumia kusema kuwa nyerere aliupigania ukatoliki mpaka kuenea Tanzania kila kona? Kwako wewe, kuhistoria unamaanisha ukatoliki uliibuka na kuanza kusambaa miaka ya 1960's?
Kurudi katika hoja yangu, nimekubaliana na utaratibu wa kumuenzi kanisani, lakini, hilo lifanyike kifamilia katika utaratibu unaotumika elekulingana na dhehebu lao.
Nyerere amepambania ukatoliki kabla ya hapo elewe hiyo inatambulika na mchango wake ni mkubwa sana huku kuenziwa Haina shida .
 
Ndiyo, sote tunajua athari za kuvunja taratibu za kidini

Fikiria, Rais Samia si ni Muislam? Vipi angeamuru kanisa libadili utaratibu kwa siku moja badala ya viti wamuwekee kapeti yeye akae.

Ila kwa kuheshimu hilo kiti hakikuharibu chochote Mkuu.

Tofauti ya viti vilivyokuwepo na cha Rais ni ile nembo na heshima inachobeba.
unatetea ujinga kweny nyumba ya ibada kafuata nn , hawawez mwambia ila hawajapenda , ukifikq msikitin fuata utaratib wa msikitini na hivyo ukifika kanisan bas fuata taratib za kanisan , kuna mtu amewai ingia na kiti chake kanisan ? kama haviamin viti vya kanisa bas angetuliza mshon asiende. Huu ujinga tunatetea ndan ya ccm ipo siku atakuja kiongoz mkristo atalipiza ndan yq msikiti na mtalalamika sana badala ya kukomesha hii tabia leo nyie mnailea , WAAFRIKA BADO HATUJUI KUZUIA MATATIZO YASITOKEE BADALA YAKE TUNASUBIR YATOKEE TUOMBEE MSAADA KWA MABEBERU
 
Na Jumakilumbi,
15.10.2022

Kile kilichotokea siku ya tarehe 14/10/2022, huko Kagera siku kumbukizi ya miaka 23 tangu alipotutoka Mzee wetu na Mkombozi wetu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kimezua mjadala mzito kwa waumini wa dini ya kikristo na wakosoaji wa serikali na Rais Samia, hapa nimekusudia kutoa ufafanuzi mfupi wa kitendo kile.

UFAFANUZI
Kiti cha rais ni nembo ya mamlaka ya Rais, mahali popote nchini awapo kwa shughuli rasmi ya kiserikali kiti chake huwepo kuashiria urasmi wa shughuli hiyo.

Kabla ya yote jambo mambo kadhaa lazima tuyaelewe na tuyakubali

* Rais Samia ni Muislam, lakini ni rais wa waTanzania wote.

* Rais huvaa kofia nyingi, ni M/kiti wa CCM, Rais wa Nchi, Muislam (binafsi yake), ni Mke (kwa mumewe) na ni Mama (kwa wanawe).

Shughuli ile ilimlalizimu kuingia kanisani katika ibada ambapo yeye kama Muislam kanisani si mahala pake pa ibada, ila yeye aliingia kwa kofia ya KIONGOZI WA NCHI, na hili lilibainishwa wazi kwa uwepo wa kiti chenye nembo ya bibi na Bwana.

Hivyo kuingia kwake na kiti chake kanisani haikuwa dharau kwa dini ya kikristo kama inavyotafsriwa na wakosoaji wake, bali ni ishara ya kofia aliyoingia nayo - Kofia ya Urais.

Maswali yaulizwayo mara kwa mara

1) Mbona Magufuli hakuingia na kiti Msikitini?
Misikitini hakuna viti, ila kuna makapeti… na kama kungekuwa na kapeti rasmi la Rais (lenye nembo ya bibi na bwana) nina hakika angeingia nalo kuonesha kofia aliyoingia nayo

2) Mbona Magufuli hakuingia na kiti Kanisani?
Hayati alikuwa Mkristo, hivyo aliingia kanisani kwa kofia yake binafsi kama Mkristo na si kama Rais.

3) Mbona Rais Samia hakuingia na kiti Msikitini?
Kwakuwa yeye ni Muislam, aliingia Msikitini kwa kofia ya Uislamu wake.
Pia Misikitini hakuna viti, ila kuna makapeti. Kama kungekuwa na kapeti rasmi ya Rais bila shaka angeingia nalo.

3) Mbona Makamu wa Rais Dr. Mpango hakukalia kiti kama cha Rais?
Kiprotokali hatuna kiti rasmi chenye nembo ya kimamlaka kwaajili ya Makamu wa Rais, ila kingekuwepo angeingia nacho.
Pia Dr. Mpango ni Mkristo, ameingia kwa kofia ya Ukristo wake.

NB: Haya ni maoni yangu Binafsi na ninawajibika kwayo.
Haina mantiki hii.
Nilikuwa na sali ST Peter's Oyster Bay J2 na kila siku ya wiki na Mwl. Julius Kambarage. Katu sikuwahi kuona akiwa na kiti chake ila ilikuwa inatengwa benchi mbili za mbele ndio anakaa na mlizi wake Nyumba.
Hii ya Sasa ni hadithi !!
 
Naona binafsi hakuna tatizo coz kwanA ijumaa hyo sio siku ya ibada kama sijakosea !!(kama ni wrong mniambie) basi kukaa hapo hakuna tatizo lolote maana imekuwa kama siku ya hafla kama siku ya kufungisha ndoa tu hutumika kama emergency na occasional events ,ingekuwa siku ya ibada kama kawaida ingekuwa tofauti.

Hata sisi swala ya maiti tunaswali random sio katika utaratibu wa kawaida ,hata ishu ya kufungisha ndoa ndo maana siku iyo mtu yeyote anaweza kuingia hata mpiga picha.
Naona unazungumzia utaratibu wa ibada wa kanisa katoliki pasipo kujua utaratibu halisi ukoje.
Kwa kifupi tu, ni utaratibu wa kanisa kuendesha misa kila asubuhi 6a.m-1.a.m, hii ni kwa kila siku za wiki. Huo ndo utaratibu wa kanisa.
Sio kweli kusema kwamba kwa kuwa ni ijumaa, ibada iliendeshwa kwa dharura tu.
 
Kama maoni yako binafsi si ungejitumia kwenye ni yako ingine?
 
Back
Top Bottom