UFAFANUZI: Rais kuingia na kiti chake Kanisani Mkoani Kagera

UFAFANUZI: Rais kuingia na kiti chake Kanisani Mkoani Kagera

Ndiyo, sote tunajua athari za kuvunja taratibu za kidini

Fikiria, Rais Samia si ni Muislam? Vipi angeamuru kanisa libadili utaratibu kwa siku moja badala ya viti wamuwekee kapeti yeye akae.

Ila kwa kuheshimu hilo kiti hakikuharibu chochote Mkuu.

Tofauti ya viti vilivyokuwepo na cha Rais ni ile nembo na heshima inachobeba.
Angekalia cha kawaida ingekuwaje
 
Kanisa katoliki halinaga matabaka.
Ila katika hili kuna tatizo la kiufundi sehemu.
 
Rais ni mamlaka ni sahihi.
Kiti cha Rais kinaonyeaha mamlaka yake ni sahihi.
Kila anapokwenda Rais lazima mamlaka yake yaomekane. Hapa umetudanganya Kwa makusudi au Kwa kutaka kumbeba Huyo unayemtetea. Kama Magufuli hakwenda na kiti kanisani na sababu unayotoa ni kwamba Magufuli alikuwa Mkristo, Sasa hayo mamlaka yake alikuwa anayaacha wapi? Kama Kila anakokwenda Rais lazima yawepo Mamlaka Choo anachotumia kina nembo ya Rais? Kwenda kuonyesha supremacy kwenye mamlaka nyingine ni uchokozi. Kama kweli Rais ni Mkuu wa Kila mahali Kwa nini alipoingia kanisani Askofu hakumpisha kiti? Imeandikwa ya Kaisari mpe Kaisari na ya Mungu mpe Mungu, Sasa yeye anapoingia kwenye ibada na Mamlaka ya kidunia anataka Mungu ndo amnyenyekee yeye?
Ndo maana walivyoenda kwa kwini wakapakizwa kwenye bus la king msukuma.mwanza to bariadi. Mzungu aliona mbali.
 
Mkuu kama umesoma vizuri nimejaribu kueleza maana ya kuingia na kiti.

Rais hakwenda yeye binafsi, alikwenda kwa kofia ya Urais. Na hilo limetanabaishwa na uwepo wa kiti cha Rais.
Mbona unajichanganya? So mtu kama jpm alipokuwa akienda sehemu kama hizo na kutumia viti alivyovikuta mamlaka ya kiti chake alikuwa akiyaacha wapi? Usitundandanye hapo haikuwa sawa.
 
Ukitaka kujua hii nchi ni ngumu muulize Shabani Kaoneka yule bondia.
 
Na Jumakilumbi,
15.10.2022

Kile kilichotokea siku ya tarehe 14/10/2022, huko Kagera siku kumbukizi ya miaka 23 tangu alipotutoka Mzee wetu na Mkombozi wetu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kimezua mjadala mzito kwa waumini wa dini ya kikristo na wakosoaji wa serikali na Rais Samia, hapa nimekusudia kutoa ufafanuzi mfupi wa kitendo kile.

UFAFANUZI
Kiti cha rais ni nembo ya mamlaka ya Rais, mahali popote nchini awapo kwa shughuli rasmi ya kiserikali kiti chake huwepo kuashiria urasmi wa shughuli hiyo.

Kabla ya yote jambo mambo kadhaa lazima tuyaelewe na tuyakubali

* Rais Samia ni Muislam, lakini ni rais wa waTanzania wote.

* Rais huvaa kofia nyingi, ni M/kiti wa CCM, Rais wa Nchi, Muislam (binafsi yake), ni Mke (kwa mumewe) na ni Mama (kwa wanawe).

Shughuli ile ilimlalizimu kuingia kanisani katika ibada ambapo yeye kama Muislam kanisani si mahala pake pa ibada, ila yeye aliingia kwa kofia ya KIONGOZI WA NCHI, na hili lilibainishwa wazi kwa uwepo wa kiti chenye nembo ya bibi na Bwana.

Hivyo kuingia kwake na kiti chake kanisani haikuwa dharau kwa dini ya kikristo kama inavyotafsriwa na wakosoaji wake, bali ni ishara ya kofia aliyoingia nayo - Kofia ya Urais.

Maswali yaulizwayo mara kwa mara

1) Mbona Magufuli hakuingia na kiti Msikitini?
Misikitini hakuna viti, ila kuna makapeti… na kama kungekuwa na kapeti rasmi la Rais (lenye nembo ya bibi na bwana) nina hakika angeingia nalo kuonesha kofia aliyoingia nayo

2) Mbona Magufuli hakuingia na kiti Kanisani?
Hayati alikuwa Mkristo, hivyo aliingia kanisani kwa kofia yake binafsi kama Mkristo na si kama Rais.

3) Mbona Rais Samia hakuingia na kiti Msikitini?
Kwakuwa yeye ni Muislam, aliingia Msikitini kwa kofia ya Uislamu wake.
Pia Misikitini hakuna viti, ila kuna makapeti. Kama kungekuwa na kapeti rasmi ya Rais bila shaka angeingia nalo.

3) Mbona Makamu wa Rais Dr. Mpango hakukalia kiti kama cha Rais?
Kiprotokali hatuna kiti rasmi chenye nembo ya kimamlaka kwaajili ya Makamu wa Rais, ila kingekuwepo angeingia nacho.
Pia Dr. Mpango ni Mkristo, ameingia kwa kofia ya Ukristo wake.

NB: Haya ni maoni yangu Binafsi na ninawajibika kwayo.
View attachment 2387854
Hamna hoja hapa. Ufafanuzi wako hauna mashiko Bro. Kajiandae upya uje na uchambuzi wa masuala mengine tu, sio lazima ya hizi Mamlaka
 
Viongozi wa sasa wanachanganya mambo tu. Hakuna haja ya Rais mwislamu kuingia kanisani wala Rais Mkristo kuingia msikitini.
Hasa hasa kusali. Hayo ni madhehebu tofauti na imani tofauti. Mkatoliki akisali msikitini anakiuka Kanuni ya Imani ya Kanisa Katoliki.
Kama ni shughuli ya kiserikali inayohitaji sala inafanyika eneo la wazi au ukumbi wa wazi bila kuhusisha msikiti au kanisa.
Kwenye tukio la Bukoba Mama Samia angeenda kusali msikitini ambako pia waislamu walisali kumuombea Hayati Nyerere, sala yake ingepokelewa Mbinguni kwa kuwa ndio imani yake.
 
Ndiyo, sote tunajua athari za kuvunja taratibu za kidini

Fikiria, Rais Samia si ni Muislam? Vipi angeamuru kanisa libadili utaratibu kwa siku moja badala ya viti wamuwekee kapeti yeye akae.

Ila kwa kuheshimu hilo kiti hakikuharibu chochote Mkuu.

Tofauti ya viti vilivyokuwepo na cha Rais ni ile nembo na heshima inachobeba.
Na hata angebadili utaratibu kwa siku moja tusingekubali utaratibu wake ,Kila kitu kisivuke mipaka ,yeye niraisi lakini hawezi kupaswa kuingilia taratibu za dini za watu,tungekataa kwa herufi KUBWA,madam atujabreak the law tungekataaaaa
 
Basi aache kujikweza kila mtu anajua yeye ni rais hata akikaa kwenye mkeka
Kwamba vile vitu vya kanisani sio stahiki yeyey kukalia ndo mana akabeba kiti,Yani uyu bibi sijui anajikuta nani jaman......kwaiyo ametuonaje sisi Christianity of low status au?
 
Hamna hoja hapa. Ufafanuzi wako hauna mashiko Bro. Kajiandae upya uje na uchambuzi wa masuala mengine tu, sio lazima ya hizi Mamlaka
little things ,lakini vina make sense a lot....tunagundua vitu kwaishara ndogo ndogo kama hizi...
 
Mbona unajichanganya? So mtu kama jpm alipokuwa akienda sehemu kama hizo na kutumia viti alivyovikuta mamlaka ya kiti chake alikuwa akiyaacha wapi? Usitundandanye hapo haikuwa sawa.
Hayati alikwenda kuabudu, Samia hakwenda fanya hivyo.

Tofauti ni dhahiri.
 
Hamna hoja hapa. Ufafanuzi wako hauna mashiko Bro. Kajiandae upya uje na uchambuzi wa masuala mengine tu, sio lazima ya hizi Mamlaka
Una hoja mbadala? Ziweke hapa tujifunze Mkuu.

Sio mbaya kukosoa ila inasaidia kama utakosoa na kuleta hoja mbadala kama alivyofanya Countrywide na bwana Congo
 
Empty headed, yaani unasema kiti ni ishara ya mamlaka na kuweka urasmi wa shughuli halafu hapohapo unasema msikitini hamna viti ndio maana haendi nacho.
Anachomaamnisha ni kwamba kama msikitini kungelikuwa na viti, basi Rais angekuwa anapelekewa kiti chake huko. Kwa sababu hamna viti msikitini, hawezi kupelekewa kiti. Au uliatka wampelekee kiti akakae kwrnye kiti yeye peke yake?
 
Back
Top Bottom